Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Huku Tanga hatunaga shikamoo.. Iwe mtu mzima wa umri gani..salamu yetu ni Asalam aleikum..
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Toa heshima we ni bwana mdogo husilewe cheo!!!Ila mazoea acha just wape heshima yao lakini swala kuwabana kazini usililetee heshima OVer!!!
Bado unatoka nje ya mada...Nawapa heshima zao sana tu BT sio Shikamoo mkuu
 
Ni salamu ha kiarabu enzi za utumwa! Akimaanisha niko chini ya miguu yako( mweusi to mwarabu) but mwenyewe kwa wenyewe hawakusalimiana hvy. Hao hao wanaolilia shikamoo ukiwaambia good morning wanakuwa wapole
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Tatizo waswahili tunaupenda utumwa sana kupitiliza. Mtu mzima ukimwambia "habari za asubuhi" atawaka eti huna heshima eti umwambie shikamoo. But huyo huyo ukimwambia "Goodmorning" atakujibu kwa furaha .....mpk wajiuliza sisi tuna matatizo gani??? Nani katuroga!?
 
Huku Tanga hatunaga shikamoo.. Iwe mtu mzima wa umri gani..salamu yetu ni Asalam aleikum..

Sheikh hiyo itakua ni Tanga mjini na maeneo ya Muheza. Kule kwetu Korogwe neno shikamoo lipo palepale! mbaya zaidi kwa wenzetu wadada na wamama wanapoolewa basi hawana budi kuwasalimia wakwe zao(baba mkwe na mama mkwe) kwa neno hili ''Mwinyi!!'' halafu baba mkwe/mamamkwe anaitikia ''Mwinyi wa Said!!'' ha ha ha ha ha!

Hapo unatakiwa kila utakapokuwepo kule basi kila asubuhi uanze kupitia nyumba moja baada ya nyingine na kuwasalimia ndugu wa ukoo wako hasa wale waliokuzidi umri, kinyume cha hapo hueleweki! utaonekana u mtoto mkaidi maana huko ndiko kule milimani ambako watu wanaishi kikoo.
 
Habar zenu wadau wa JF ,Mm n mwajiriwa ktk Taasisi fulani ktk position nliopo tupo vijana wachache majority n watu wazima na wazee(40 to 55) kulingana na nature ya kaz yangu wengi wao wanahitaji usimamiz wangu kazini na pale wanapokosea sina budi kuwaadabisha sasa inakuja mahala mtu anataka umwamkie kitu ambacho nlijifunza mahala nlipokua nafanya kaz mwanzon nlikua nawasalimu wakubwa kwangu bt wote walikuja kunidharau na pale nlipotaka kutoa adhabu walinibeza na vijineno" katoka juz shule sie tunajua maisha wazazi wako " nlitafta ushaur kwa wakubwa zangu kazini nliambiwa nmeharibu kumwambia shikamoo aliyeko chini yangu badala yake nisalimie "HABARI ZA SAHIZI,ZA LEO,ZA ASBH N.K... Tangia hapo nlistop kutoa shikamoo kwao mpk nmehamia Taasisi ingne .Huku ndio wananibeza kusalimia japo msimamo wangu ni uleule SITOI SHIKAMOO TENA.. nimekua nashangazwa sana pale MTU anapolazimisha salamu japo nawaheshimu kama wanaonizidi ...Swali::Je Shikamoo ndio ishara ya heshima kwa MTU au nn zaidi nifanyeje??Tushauriane wadau
Tatizo sio shikamoo. Ninachokiona mimi unapoingia sehemu mpya lazima uwasome watu, unapojifanya mjuaji itakuumiza. Wasikilize, wahoji kirafiki baadaye wabadilishie kibao lakini usichelewe. Wasije wakajenga mazoea.

Shikamoo: I am kneeling before you.
Marahaba: not enough (hata mara ngapi)
 
Shikamoo maana yake nini kwa Kiingeleza?
Maana waingeleza wana Good Morning
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Tatizo sio shikamoo. Ninachokiona mimi unapoingia sehemu mpya lazima uwasome watu, unapojifanya mjuaji itakuumiza. Wasikilize, wahoji kirafiki baadaye wabadilishie kibao lakini usichelewe. Wasije wakajenga mazoea.

Shikamoo: I am kneeling before you.
Marahaba: not enough (hata mara ngapi)
Thanks mkuu kwa mchango wako....iko haja pia kwa wadau Wa lugha kuangalia matumiz ya neno SHIKAMOO
 
Aisee nilikuwa sifahamu maana ya shikamoo. Now that I know hamna shikamoo tena hata uwe nani au umenizidi umri kiasi gani
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Kwa nilivyosikia mimi neno shikamoo maana yake ni "niko chini ya miguu yako.

Pia nimesikia hilo neno ni la kitumwa na lilikuwa linatumiwa na watumwa kuwaonyesha heshima wakuu wao.

Kuna baadhi ya watu nawajua hawapendi kupewa shikamoo na hata wakipewa hawajibu marahaba.

Je kama hili neno ni la kitumwa, kwanini sisi tuendelee kulitumia kama neno linaloashiria heshima?

Kama lilitumika kuwakandamiza mababu zetu kwanini na sisi tulipe nafasi? Au tunalitumia kama wenzetu Wamarekani weusi wanavyo tumia neno "nigga" ambalo lilitumika kudharau mababu zao na kulifanya la kwetu sasa?

Aisee kwanza nikupe hongera kwa kutupa ufahamu juu ya huu utumwa mambo leo,mimi mwenyewe nimekuwa najiuliza sana kwanini sisi waswahili tumekuwa tunafwata kila jambo ambalo tumelikuta babu zetu wakitumia na fika tukijua kuwa babu zetu walikumbana na utumwa,nadhani ifikie mahali TAKI wafanyie marekebisho baadhi ya maneno ya kiswahili hasa haya yanayo endeleza utumwa mambo leo.
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Babu zako wenye nguvu na akili kiduchu waliwauza babu zako waliokuwa mapunguani.

Kama hilo ni neno la kitumwa vipi na ile mila ya wanawake kupigia magoti wanaume wakiwaamkua?

Isitoshe, utumwa haujaisha hadi leo hii na Tanzania ni moja ya nchi zilizo juu juu kwenye list ya nchi zenye kuendeleza utumwa duniani.
 
Mbona povu linakutoka bibi kutetea shikamoo??? Au sababu limetokea kuleeee?? Kwa waleee??? Maana wewe wakiguswa tu wale unakuwa mbogoo sana

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
MwanaFalsafa1 said: ↑

Nakubaliana wewe kwa 100% kwa sababu maana ya shikamoo haijabadilika Ni ile ile ya "niko chini ya miguu yako", lazima tuukubali ukweli kuwa shikamoo haina maana yoyote ya kiheshima.
 
MwanaFalsafa1 said: ↑

Nakubaliana wewe kwa 100% kwa sababu maana ya shikamoo haijabadilika Ni ile ile ya "niko chini ya miguu yako", lazima tuukubali ukweli kuwa shikamoo haina maana yoyote ya kiheshima.

Hapana, si kweli. Hiyo si maana ya neno shikamoo.

Kiswahili kitamu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom