Asili ya jina Tanzania na mwasisi wake: Mohammed Iqbal Dar

jamaa ni jembe jina tamuuu! Idumu tanzania na itadumu.....uamsho!
sijui kama itadumu ....bado ina uhai kidogo sana siku si nyingi kila mtu na lwake.....nchi mbili zitazaliwa upya na moja itazaliwa kwa mara ya kwanza
 
matatizo yetu yanaanzia mbali aisee, yaani nchi tunamoishi haina hata jina bali lilibuniwa na mtu wa kuibuka tu!!!
Ama kweli.
Katika misemo ya kwetu hapa kuna mmoja unasema kuwa daima jina lina reflect mwenye nalo (eibala libi lita nyinalyo). Mbona wenzetu wna majina ya asili zao mfano kenya, uganda, malawi/nyasa, rwanda, burundi na hata congo walilirejesha kutoka zaire.
majina ya asili yatarejea baada ya kuvunjika muungano usihofu ndugu
 
anataka watanzania wathamini vpi mchango wake..? Yeye anaishi huko uk.. Halafu alilipwa kwa kazi aliofanya.. Na isitoshe muda ci mrefu jina lenyewe la tanzania litakufa..
ni kweli hili jina halina uhai mrefu kutoka sasa
 
sijui kama itadumu ....bado ina uhai kidogo sana siku si nyingi kila mtu na lwake.....nchi mbili zitazaliwa upya na moja itazaliwa kwa mara ya kwanza

Kwa kweli kwa jinsi UAMSHO ilivyo ikalia vibaya..haina siku nyingi, Juzi nilimsikia alijificha na kuibuka kuwa alikamatwa na kuchapwa bakora na polisi anasema mpaka tone la damu ya mwisho lazima visiwa vijitawale..!
 
Hongera kaka. Sisi wenzako wakati huo hata kuzaliwa ilikuwa bado. Kwa bahati mbaya jina Tanzania linatishiwa kutoweka pia kutokana na Zanzibar kutaka kujitenga
Mwaka 1964, wakati nipo darasa la 8, nilisoma gazeti la the Standard na kulikuwa Shindano hili la kulipa jina nchi yetu. Wakati huo nchi yetu ilikuwa inaitwa the United Republic of Tanganyika & Zanzibar. Wakati ule, shuleni tulikuwa tunasoma jiografia ya Australia na nakumbuka kisiwa cha Tasmania. Hii ilinipa hint ya jina la Tanzania. Mimi niliandika barua wizara ya Habari. Nakumbuka kupokea hundi ya Sh. 12.50 ikiwa ni share yangu ya kuipa jina Tanzania.

Maelezo katika barua ya Katibu Mkuu ilisema: Kwa sababu kulikuwa washindi 16, kwa hiyo hizo zawadi ya Sh. 200 itagawiwa miongoni mwa washindi. Pia, barua hiyo iliniambia kwamba jina hasa lililokubaliwa ni United Republic of Tanzania and sio Tanzania, kama nilivyoandika mimi.

Nakumbuka pia kwamba gazeti la September 1, 1964 au October 1, 1964 ilikuwa na headline, " From today, we are Tanzanians"

Huyo Mohamed Iqbal kama ni katika watu 16, basi anaweza kukubaliwa. Lakini kama anasema ni peke yake aliyechagua jina hili, basi ni mwongo. Best solution ni kwa Wizara ya Habari kupekua file zao na kujua ukweli. I am pleased to be part of history of Tanzania. Ikiwa wengi katika hao 16 walikuwa watu wazima mwaka 1964, basi wengi watakuwa wameshaaga dunia na itakuwa mushkeli kujitokeza. Mimi wakati huo nilikuwa kijana wa miaka 13 lakini nilikuwa na bahati kusoma gazeti la kiingereza kwa sababu ya baba yangu, ambaye alikuwa anapenda sana kusoma magezeti.

Asili yangu ni kihindi na nilisoma Chuo cha Sokoine 1974. Sasa hivi nipo Marekani na imekuwa bahati tu kusoma forum hiyo kwa sababu ya mambo ya Lowasa.

Ahsante,
Mustafa Yusufali Pirmohamed
 
Kwa kweli kwa jinsi UAMSHO ilivyo ikalia vibaya..haina siku nyingi, Juzi nilimsikia alijificha na kuibuka kuwa alikamatwa na kuchapwa bakora na polisi anasema mpaka tone la damu ya mwisho lazima visiwa vijitawale..!
muungano ukivunjika nchi mbili zinarudi katika uso wa dunia nazo ni TANGANYIKA NA ZANZIBAR baada ya hapo Zanzibar itagawanyika na kupata Zanzibar Republic and pemba republic maana ndicho wanachokitafuta uamsho
 
Hongera kaka. Sisi wenzako wakati huo hata kuzaliwa ilikuwa bado. Kwa bahati mbaya jina Tanzania linatishiwa kutoweka pia kutokana na Zanzibar kutaka kujitenga
pemba wanataka kujitenga
 
muungano ukivunjika nchi mbili zinarudi katika uso wa dunia nazo ni TANGANYIKA NA ZANZIBAR baada ya hapo Zanzibar itagawanyika na kupata Zanzibar Republic and pemba republic maana ndicho wanachokitafuta uamsho

Bwana Mpalu, Nyerere aliwahi kusema watu wanapata jeuri ya kujiita mimi ni Mzanzibari na yeye ni Mtanganyika kwa sababu wako ndani ya Muungano, ukivunjika muungaano wataaanza mimi Mpemba na yeye Muunguja, na kwa jinsi UAMSHO wa kina Mohammed Said na wenzie wanvyoutaka watakuja juta kwanini walivunja muungano! ngoja tuone...TIME SHALL TELL>>>>>>>.
 
Bwana Mpalu, Nyerere aliwahi kusema watu wanapata jeuri ya kujiita mimi ni Mzanzibari na yeye ni Mtanganyika kwa sababu wako ndani ya Muungano, ukivunjika muungaano wataaanza mimi Mpemba na yeye Muunguja, na kwa jinsi UAMSHO wa kina Mohammed Said na wenzie wanvyoutaka watakuja juta kwanini walivunja muungano! ngoja tuone...TIME SHALL TELL>>>>>>>.
hili swala mbona liko wazi sana wapemba walio wengi wanataka muungano uvunjike na waunguja wengi wanataka muungano uendelee...uamsho walichoma maskani za ccm(OFISI) na wala sio za cuf kwa nini?kwa sababu ccm haitaki muungano uvunjike na chama hiki kinaungwa mkono na waunguja zaidi kuliko wapemba wanaounga mkono zaidi cuf ...ukitaka kujua waunguja na wapemba wanatofautiana tembelea mtandao wa MZALENDO NET HUKO wanatukanana mpaka basi
 
Mohamed Iqbal Dar kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la jumapili wiki hii.

Bado kidogo wenye jina (wenye IMANI WALE!) watakuja kudai Nyerere si baba wa Taifa bali (in red) kwa sababu ndo alibuni jina na si NYerere! na kwa jinsi wanavyoendelea kudai JKN si baba wa Taifa wako kwenye mkakati wa kumtafuta baba wao!
 
Jamani wana JF habari za mda huu,

Naskitika sana kuona mmoja wawaasisi wa taifa hili la Tanzania MOHAMMED IQBAL DAR kasahaulika kabisa katika vitabu vya historia ya TANZANIA kwani vinasema kua neno 'tanzania' limetokana na kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar tu bila kutaja ninani aliyebuni jina hili la 'TANZANIA' Kiukweli jina "TANZANIA"limebuniwa na ""MHAAMMED IQBAL DAR" "baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Alibuni jina hili akiwa na umri wamiaka 18 akiwa mwanafunzi washule ya sekondari mzumbe mwaka1964 baada ya kutolewa shindano la kutafuta jina litakalotumika badala ya Tangayika na Zanzibar na baba wataifa mwalim NYERERE katika gazeti la Daily News wakati huo likiitwa The Standard akizungumzia jinsi alivyounda TANZANIA Mohamed Dar anasema:

'Nilichukua neno TAN kutoka Tanganyika nakuchukua neno ZAN kutoka Zanziba nikapata TANZAN baada ya kuona halijatimia vizuri, ndiponikagundua kua nchi nyingi za Afrika zinamalizia na herufi "IA" kama ZambIA EtjiopIA NamibIA nanyingine nyingi hivyo na mimi nikaamua kumalizia na herufi "IA"nakupata "T A N Z A N I A".n

Na watanzania wengi wanelewa kua babawataifa malim Nyerere ndie aliebuni jina TANZANIA kumbe sivyo bali kuna mwasisi wa jina TANZANIA ambae ni MOHAMMED IQBAL DAR anayeishi England kwasasa.Inafaa sana sasa kumkumbuka nakumweka ktk vitabu vya historia ya Tanzania kwani bila MOHAMMED DAR tusingeitwa waTANZANIA tungeitwa vingine tofauti na TANZANIA tuache tabia ya kuwa kumbuka tu watu wachache kwani TANZANIA haikuasisiwa na watu wawili watatu tu.

Nalishukuru sana gazeti la MWANANCHI Jumapili kwa kutukumbusha/kutuelimisha historia sahihi ya jina TANZANIA

KagomaBhihusi.
 
huyu mtu alipewa tuzo, na pia pesa, serekali ilishamtambua toka awali, hakuna mahali ambapo palisema nyerere ndio mwanzilishi wa jina tanzania, sasa sijui ni nini anakitaka kila siku kulalama kwenye vyombo vya habari, mimi naona anataka umaarufu tu, mtu mwenyewe alishaukana uraia wa tanzania so what?, anataka amiliki copyright ya jina la tanzania?, au?, amesahaulika kivipi, muda sio mrefu tanzania yenyewe itatoweka na kubaki tanzania kwa hiyo atafanyaje?
 
Makubwa, kwa nini taifa limemsahau??


MOHAMMED IQBAL DAR.jpg

Mohammed Iqbal Dar (picha hapo juu) ndiye aliyebuni jina la Tanzania, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 akiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari. Mohammed anasema alikuwa Maktaba akijisoma gazeti la Tanganyika Standard, siku hizi Daily News, akaona Tangazo linasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana kwa hiyo Wananchi wote wakaombwa Washiriki kwenye shindano la Kupendekeza jina moja litakalo zitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar Mohammed Iqbal Dar anasema aliamua kuingia kwenye Shindano na hivi ndivyo alianza Safari ya Kubuni Jina la Muungano.

Kwanza anasema alichukua karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na Imani yake na baada ya hapo akaandika jina la Tanganyika baada ya hapo akaandika Zanzibar halafu akaandika jina lake Iqbal halafu akaandika jina la Jumuiya yake ya Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili apate jina zuri kutoka katika majina hayo aliyokuwa ameyaandika. Baada ya hapo Mohammed Iqbal Dar alichukua herufi tatu kutoka Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua Herufi tatu za Mwanzo ZAN ukiunganisha unapataTANZAN alivyoona hivyo akachukua I herufi ya kwanza katika jina lake la Iqbal na akachukuaA kutoka jina la dini yake yaani Ahmadiyya kwa maana hiyo ukiongeza herufi hizi mbili I na Akwenye TANZAN unapata jina kamili TANZANIA akalisoma jina akaliona ni zuri lakini akajiridhisha pia kwamba akiongeza herufi hizo za I na A kwenye TANZAN italeta maana kwakuwa nchi nyingi za Afrika zinaishia na IA, mfano EthiopIA, ZambIA, NigerIA, TunisIA, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA, MauritanIA alivyoona hivyo akaamua apendekeze kuwa jina TANZANIA ndio litumike kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka majina manne majina hayo ni Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na Ahmadiyya.

Mohammed Iqbal Dar baada ya kupata jina hilo akalituma jina hilo kwenye kamati ya kuratibu Shindano. Baada ya Muda mwingi kupita baba yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea barua nzito kutoka Serikalini akijulishwa kuwa alikuwa ni mmoja ya wabunifu 16 walioshinda jumla ya Tshs 200 na mgao wake ilikuwaTshs 12.50 na alilipwa kwa hundi zama hizo (1964).
 
Baada ya Muda mwingi kupita baba yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea barua nzito kutoka Serikalini akijulishwa kuwa alikuwa ni mmoja ya wabunifu 16 walioshinda jumla ya Tshs 200 na mgao wake ilikuwaTshs 12.50 na alilipwa kwa hundi zama hizo (1964).
Sio siri kuna hoja anataka kujenga, kama walikuwa 16 walioshinda wakagawana hundi, hivyo sio peke yake aliyetunga hilo jina, wengine pia waliweza kutoa wazo kuwa iitwe tanzania, je hao wengine ndio wanaoheshimiwa kuliko yeye au yeye anataka heshima zaidi?.

Hapa anataka kujenga hoja ya kuwa amesahaulika lakini haina uzito alitaka apewe nchi aongoze?, mbona waliobuni nembo na mambo mengine ya kitaifa hawalalamiki?, sio siri kuna kitu huyu mzee anatafuta
 
Back
Top Bottom