Asili ya jina Tanzania na mwasisi wake: Mohammed Iqbal Dar

NI VIZURI KUFAHAMU HASA KWA WALE TUSIOFAHAMU HILI


Huyu bwana aliyebuni jina la Tanzania ni Muhindi na Dini yake ni AHMADIYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA majina yake ni MOHAMMED IQBAL DAR.

Mohammed alizaliwa Mkoani Tanga miaka ya 1944, Baba mzazi wa Mohammed alikuwa Daktari huko mkoani Morogoro alikuwa anaitwa Dr. T A DAR alikuwa Tanganyika kuanzia mwaka 1930.

Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya Msingi Mkoani Morogoro shule ya Msingi H H D AGHAKHAN kwa sasa ni Shule ya Serikali na baada ya hapo alikuja baadae kujiunga na Chuo cha Mzumbe akasoma Kidato cha Kwanza mpaka cha Sita.
 




REPRESENTED BY THE
MINISTRY OF INFORMATION AND TOURISM,TANZANIA
TO
MOHAMED IQBAL DAR
IN RECOGNATION OF THE ACHIEVEMENT OF CHOOSING THE NEW NAME FOR THE
UNITED REPUBLIC OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR NAMELY
“REPUBLIC OF TANZANIA”
DURING THE NATIONAL COMPETITION DAY IN 19TH NOVEMBER 1964
I A WAKAL
MINISTER FOR INFORMATION AND TOURISM


Iwekwe hiyo barua humu jamvini, kisha tunaomba wenye ufahamu watujuze maana wengine tumezaliwa baada ya Muungano.
 
Big up sana ndugu kwa jitihada zako za kutufanya watanzania tuijue historia ya nchi ye2, kiukweli nikiwa miongoni mwa wale ambao 2likua hatujui chimbuko la jina la nchi yetu (TANZANIA) umeniondolea kiza kinene kilichokuwa kimetanda machoni mwangu. GOD BLESS YOU.
 
Nasikia Mwl. Nyerere alipata kusema jina TANZANIA lilitokana na TAN (Tanganyika), ZA (Zanzibar), NIA (nchi hizi ziliundwa kwa NIA moja) hence TAN-ZA-NIA (TANZANIA). Hii ndio tafsiri sahihi iliyotolewa na serikali kipindi hicho. Inawezekana kweli katika mchakato huo wa kupokea mapendekezo ndio serikali ikapata tafsiri sahihi ya NIA moja.

swali langu 200 ya kipindi hicho ni sawa na shilingi ngapi kwa sasa? Je, Milion 5 za Katanzania?

 
Watu wengine bwana, masharti ilikuwa mshindi apewe 200/- haikusema mshindi atapewa tuzo ingine yoyote zaidi ya hiyo. Sasa yeye leo analia lia anataka apewe nini tena? Kama ana njaa zake aseme sio kutuletea mitafaruku ya kidini au alitaka jina lake liiingizwe kwenye mitaala ya primary skul ndio aridhike?
 
matatizo yetu yanaanzia mbali aisee, yaani nchi tunamoishi haina hata jina bali lilibuniwa na mtu wa kuibuka tu!!!
ama kweli.
Katika misemo ya kwetu hapa kuna mmoja unasema kuwa daima jina lina reflect mwenye nalo (eibala libi lita nyinalyo). Mbona wenzetu wna majina ya asili zao mfano Kenya, Uganda, Malawi/Nyasa, Rwanda, Burundi na hata Congo walilirejesha kutoka Zaire.
 
200 kipindi hiko unanua bicycle 1 tu....sasa hiyo ndiyo kubwa? zomba unaweza kutusaidia 200/- wakati huo unapata nini?

Enzi zile pesa hiyo ilikuwa inatosha kununua ng'ombe watatu au zaidi. Bati moja lilikuwa linauzwa shilingi moja tu. Mwalimu wa shule ya msingi alikuwa analipwa chini ya hizo.
 
200 kipindi hiko unanua bicycle 1 tu....sasa hiyo ndiyo kubwa? zomba unaweza kutusaidia 200/- wakati huo unapata nini?

Ukiwa selfish huwezi kukosa kitu cha ku-complain. Lakini ni imani yangu kuwa 200 by then ilimtosha kabisa kununua Quran mpya kabisa. Was not that a good deal?
 
Ukiwa selfish huwezi kukosa kitu cha ku-complain. Lakini ni imani yangu kuwa 200 by then ilimtosha kabisa kununua Quran mpya kabisa. Was not that a good deal?



Mndengereko mieeeeeee! Nitafilisika kila kitu lakini siyo MANENO.
 
Back
Top Bottom