Mbona kisomali kabisa hiki?Basodawe = Ziwa la Usiku
Kibarbaig: Ziwa = Basod + Usiku = Awed
Kuna maneno kadhaa ya Kidatoga yanafanana na ya Kisomali.Mbona kisomali kabisa hiki?
Keep in zero (waswahili kiponzelo)Hivi umepata kujiuliza unapopita katika mitaa mbalimbali ya mjini Dar au mji mwingine wowote Tanzania, jina la mtaa au eneo husika limetokana na nini?
Kwa mfano, Kijito Nyama limetokana na nini? Au Mlalakuwa, Au Mtoni kwa Aziz Ali n.k, n.k. Labda utadhani imetokea tu ... just ipo ipo, hapana! Baadhi ya majina ya mitaa yana historia ndefu na yenye kukumbukwa hata kwa vizazi vijavyo.
Hapa napenda kuwahabarisha maana ya mtaa au eneo la nje kidogo ya jiji la Dar liitwalo Gongo la Mboto.Jina hili limetokana na nini? Nakumbuka nilipata kusimuliwa na mwalimu wangu mmoja miaka ile pale Tambaza Sekondari nikiwa kidato cha pili.
Alisema palikuwa na mzee mmoja mashuhuri ambaye alipata kuishi katika eneo hilo.Huyu jamaa alikuwa mkulima. Jina lake aliitwa Mboto. Siku moja alijilawa kwenda katika konde lake kwa ajili ya kujipatia riziki.
Wakati ule, maeneo yale yalikuwa na giza la mapori na vichaka kadhaa. Jioni yake asirudi nyumbani. Kesho yake hadi mchana Mboto haonekani.
Mbiu ikapigwa watu wakakusanyika,kilichofuata ni msako mkali wa kumtafuta mzee huyu.Baada ya siku kadhaa wakakuta nyayo za mnyama mkubwa mithili ya Simba na ishara ya purukushani kadhaa.
Walipochunguza zaidi wakafanikiwa kukuta Gongo ambalo alipenda kutembea nalo mzee huyu.Wakahisi kuwa Mboto huenda amekutwa na maafa ya kuliwa na Simba. Walichokiona pale ni Gongo lake,Ndipo hilo eneo hadi leo lajulikana kama Gongo la Mboto.
Tuhabarishane maana ya maneno mengine kama Msasani, Mikocheni,Mto wa Mbu n.k.
Ha haaaaaKiboriloni...keep rolling
Arusha... rarusa(kimaasai) mzungu akashindwa kutamka
Mzumbe...ensumbe mzungu alishindwa kutamka..hii inahistoria kidogo mpaka naona uvivu kuandika.
Olduvai...Oldupai
Cairo....gailo kimaasai(sina uhakika)
umenikumbusha home kbs KB nimepamis mnoKiboriloni...keep rolling
Arusha... rarusa(kimaasai) mzungu akashindwa kutamka
Mzumbe...ensumbe mzungu alishindwa kutamka..hii inahistoria kidogo mpaka naona uvivu kuandika.
Olduvai...Oldupai
Cairo....gailo kimaasai(sina uhakika)
Lukuledi ni Masasi Mkoani MtwaraMkuu huo mto upo wapi? bado lediz wanaoneshwa?
MasasiMkuu huo mto upo wapi? bado lediz wanaoneshwa?
Mmmmhh siyo cow way =kawe???Duh, uzi wa siku nyingi huu! Inawezekana kuna wachangiaji wa huu uzi wamesharest in peace hapa! Live longer mliopo hai, R. I. P waliokufa. Shekilango=sheikh kilango. Kawe=car way.
Pangani linatokana na lugha ya kizigua, "wapangani hano" yaani wapangeni hapa( watumwa)Pangani: Mwaka 1873 Sultani wa Zanzibar alipotiliana sahihi na Serikali ya Uingereza mkataba wa kusimamisha biashara ya utumwa, eneo la Pangani ya sasa ilitumika kama soko la magendo la utumwa kwa kupitia Kisiwa cha Pemba ilikukwepa manowari za Kiiingereza. Hivyo wakati watumwa wanapangwa kwa kuuzwa waliamriwa "jipangeni" Tunaambiwa hiyo ndiyo asili ya Pangani.