Ashindwa Kutongoza Mademu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Kijana mwenye umri wa miaka 20 wa nchini Marekani ambaye alikuwa akilalamika kuwa anashindwa kumwaga sera za kuwavutia mabinti, aliamua kumpiga nyundo ya kichwa bibi yake ili apunguze haja zake za kimapenzi.
Samuel Dye alimfuata bibi yake na kuanza kulalamika kuwa ameshindwa kabisa kutongoza wanawake hivyo ameshindwa kupata mpenzi.


Taarifa za polisi zinasema kuwa Samuel baada ya kutoa malalamiko yake kwa bibi yake mzaa baba yake, alimuambia kuwa lakini ukame wake wa mapenzi angeumaliza siku hiyo kwake yeye.


Samule alishusha nguzo zake na kumuonyesha bibi yake nyeti zake kabla ya kumpiga nyundo ya kichwa ili aweze kutimiza azma yake ya kumaliza ukame wa mapenzi.


Taarifa zaidi zilisema kuwa Samuel alizuiliwa na baba yake asimbake bibi yake baada ya baba yake kusikia kelele za mama yake mwenye umri wa miaka 61 akiomba msaada baada ya kupigwa nyundo ya kichwa.


Baba mtu alimkuta mwanae akiwa ameshusha suruali yake akiendelea kumpiga na nyundo bibi yake.


Samuel alizidiwa nguvu na baba yake na alifungiwa kwenye chumba huku polisi wakiitwa waje kumchukua.


"Alikuja nyumbani saa 10 usiku akiwa na nyundo mkononi na kuanza kulalamika ameshindwa kupata mpenzi na leo ndio angemaliza tatizo hilo", alisema bibi yake Samuel na kuongeza "Nilimuomba asifanye chochote na tukae pamoja tusali tumuombe mungu".


Samuel ametiwa mbaroni na amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua na kujaribu kubaka.
 
Astaghafrulah laana tu lah! kwa nini asingeomba msaada nimsaidie kutongoza, hebu mpe namba zangu tuwasiliane huko lupango
 
Back
Top Bottom