Asha Mkwizu Hauli-Na kesi ya kumuua hawara wa mumewe

Hii inasikitisha, nimesoma kisa chote hadi mwili umenisisimka. Kweli mapenzi ni hatari.
 
Inasikitisha kwa kweli. Sheria nayo haiko fair,kwa nini chanzo cha yote hayo(wanaume) hawaguswi?
Unachosahau ndugu yangu ni kuwa, hii ni kesi ya mauaji na wala si ya mapenzi. Yawezekana ni kweli mwanaume ndio alisababisha jambo hili litokee lakini mwisho wa siku aliyeua ndio mwenye hatia!!
 
Jamani mmenikumbusha mbali, nilikuwa mdogo sana, nakumbuka mummy alikuwa akifuatilia thru magazeti. Na hata hiyo ya simbaulanga naikumbuka sana.

Ali Maumba was very recent case I suppose. Jamani almost 30 years.
 
Mkuu hii kitu inasisimua sana, pamoja na hiyo ya Maumba naomba kama unaweza kupata na kesi ya Babu Seya pia-mengi yanasemwa mitaani kuhusiana nayo, tungependa kuona mwenendo wa kesi na ushahidi uliotolewa
 
Mahusiano... Mapenzi na ndoa ni entities ambazo ni ngumu mno! Ni vitu ambavo hudharaulika kua ni kawaida na haviwezi mchanganya mtu.... Inasikitisha saana. Inahitaji reasoning ya hali ya juu saana.... Ila tu bahati mbaya reasoning in matters concerning the heart in most cases it has proved kua ni Impossible. Hii story imenikumbusha story moja iliwahi tokea wakati nipo mdogo.

Kuna baba alikua ana mwanamke ambae walikua karibu kama wapenzi.... Hizo habari zikamfikia mkewe na mkewe huyo akafanya jitihada zote ili kuhakikisha anapata ushahidi huo. Mungu si Athumani kweli akafanikiwa kuwakuta Live. Akarudi kwake.... mumewe pia akarudi na kumuomba msamaha mkewe; Ambae bila hiana akakubali kwa makubaliano kua amuache...... Mwanamke huyo the next day akategea mumewe kalala, kamchemshia mafuta ya kupikia na kumwagia sehemu zake za siri..... Baba wa watu akapiga yoooowe na kulia kama mtoto mdogo... majirani wakakusanyika pale... Analia na kutaja majina ya watoto wake na kuwaambia msiingie chumbani nipo uchi... (akiwa hataki kabisa watoto wamuone uchi); Hata hivo alizimia dakika chache baadae.... na kuwafanya majirani kuingia ndani na kumpeleka Hospitali.... Masaa machache baadae aliaga dunia.

Hio case nayo ilipelekwa mahakamani.... Ila good or bad thing watoto walikua wana say... Kua mama yao asamehewe ama Lah! (Katika process zile za kukata rufaa or whatever!) Watoto waligoma kabisaaaa! Wakasema mama kamuua baba.... She deserves to die too.... Naamini pia alinyongwa.
 
Kesi kama hii na ya mume wa Josephine kwa upande wa pili wa shillingi zinaumana. Hii ilikuwa ni mwanamke kuingilia ndoa na Josephine na Slaa ni ya mwanamme kuingilia ndoa! likitokea la kutokea siku ya siku, tusiseme tulikuwa hatujui.
 
Hii story inasikitisha sana! Nimesoma story yote na huku machozi yakinitiririka! Mapenzi kweli ni zaidi ya atomic yanapokwenda kombo!
 
Asante sana, baada kusoma nimejikuta na maswali/shaka na time frame ya matukio. Inawezekana kweli Bi Asha alifanya mauaji lakini kwa kupitia dhana ya beyond reasonable doubt, je mlolongo wa matukio yote unafit kwenye time frame?
 
kesi kama hii na ya mume wa josephine kwa upande wa pili wa shillingi zinaumana. Hii ilikuwa ni mwanamke kuingilia ndoa na josephine na slaa ni ya mwanamme kuingilia ndoa! Likitokea la kutokea siku ya siku, tusiseme tulikuwa hatujui.

mkuu huyo uliyemgusa sasa ni kipenzi cha watu hapa jf, hata akitoa ushuzi kwenye kikao wafuasi wake hao watasema hakujamba, bali mwili wake automatically unatoa 'natural perfume' jiandae na mashambulizi dhidi yako mkuu kwani watakuja punde tu.
 
Kesi kama hii na ya mume wa Josephine kwa upande wa pili wa shillingi zinaumana. Hii ilikuwa ni mwanamke kuingilia ndoa na Josephine na Slaa ni ya mwanamme kuingilia ndoa! likitokea la kutokea siku ya siku, tusiseme tulikuwa hatujui.

Hii ni tofauti mkuu acha kuleta za kuleta hapa, Josephine na mumewe walikuwa wametengana kipindi kirefu mume hajui mke anakula nini, analala wapi, anavaa nini, huwezi sema hapo kuna ndoa- bahati mbaya dini yao hairuhusu talaka otherwise ingekuwa imeshatolewa zamani.Slaa alikuwa demu yuko loose mkuu hakuna lawama hapo
 
Thanks Mtambuzi kwa kutujuza. Wengine tulikuwa wadogo hivyo hii story sijawahi isikia.

Nimesoma mwanzo mwisho na kwa kuwa mi si mwanasheria na najua sheria si mala zote iko fair nimebaki na maswali mengi na nimejaribu kuwa kwenye viatu vya muuaji.

Kwanza inaonyesha familia ya mume walikuwa wanaingilia maisha yao ya ndoa.
Pili inaonyesha huyo muuaji na mumewe hawakuwa na watoto
Tatu inaonyesha huyo mwanaume alikuwa na wanawake wengi (imeripotiwa hivyo sehemu fulani ya hii ruling)

Nachoshangaa sijaona hata sehemu moja mume wa muuaji akitoa ushaidi. Wangemwita atoe ushaidi wa uzinzi wake ili naye japo apate hukumu walau ya kupata aibu!

Natoa wito kwa akina mama hasa kipindi hiki cha kubadili katiba kushinikiza Bunge wanaume wanaopelekea wake zao kuua nao wapigwe mvua. Love kills kwa hiyo mi simshangai wala kumlaumu muuaji kwani hata hadithi za Shakespeare zimethibitisha kuwa kucheza na love feelings za mtu ni kuchezea kifo.
 
Asante kwa kesi hii ndefu, nimeipitia kwa haraka haraka ila nitaisoma vizuri jioni nikiwa nimetulia.
Kuna ya mama Liundi pia, aliua watoto sababu ya wivu wa mapenzi pia. Wanaume kama kawaida yenu chanzo cha matatizo.

Da asante sana mtambuzi umekuwa mwenye mchango mkubwa hapa jf hasa kutokana na hivi visa vya kuelimisha unavyotuwekeaga hapa jamvini.kwani unatoa elimu kwa njia ya pekee.ninapenda kusema kuwa ninafurah sana ninaposomaga mikasa hii.
 
Mtambuzi wewe ni kiboko, nilikuwa nasoma kila nikisema nitaishia hapa najikuta naendelea mpaka nimemaliza..

Kwa kweli Mungu atujalie moyo wa uvumilivu wanawake sie, yaani mume kuchukuliwa mpaka unaua!
Chonde chonde wanaochukuwa wame za watu, wanawake wengine hawana uvumilivu jamani, ama zake ama zako...
 
Matambuzi asante aise, enzi hizo mimi nilikuwa primary, hivi kesi ya Sarah Simbaulanga ilishaje enzi hizo
 
Mkuu ninaomba kama kuna mwenye kuikumbuka ile kesi ya mauaji ya kijana mmoja aliyemuua dada yake hapo Upanga karibu na Palm Beach miaka ya 80 nadhani - mtoto wa Mzee Nombo atuhabarishe. Ilisikitisha sana.
 
Back
Top Bottom