Asemavyo Mkapa Kupitia BBC

Duble Chris

JF-Expert Member
May 28, 2011
3,481
564
Hi JF members

Leo asubuhi kupitia BBC Mkapa Rais wa awamu ya 3 wa JMT amezungumza yafuatayo;

Wengi hawajui katiba mpya inaandikwaje wanafikiri tunachukua plane paper tunaanza kuandika kila kitu Nooo hatufanyi hivyi isipo kuwa marekebisho makubwa yanafanyika nchi nyingi zinafanya hivyo

Tulipo anzisha mfumo wa vyama vingi tulitegemea kuona vyama vipya vinakuja na mfumo,sera tofauti na CCM lakini sasa vyama vingi vina mfumo na muundo sawa na CCM.

Wengi wanafiri katiba mpya ikianza kutumika tu basi upinzani utashina Nooo si rahisi kuishinda CCM

Wengi wanalalamika kuwa tume ya Uchaguzi si huru ukiwauliza si huru kivipi hawasemi wanashindwa kueleza

Alikuwa akijibu maswali ya mtangazaji wa BBC. Mazungumzo haya yataendelea wiki ijayo ikiwa ni sehemu ya maadhamisho ya miaka 50 ya UHURU wa Tanganyika

Nawasilisha
 
Huyu mzee kwanza akae kimya maana hatujasahau alivofanya biashara akiwa ikulu kinyume na katiba!! halafu bila aibu ansema watu hawawezi kueleza kwa nini tume sio huru?? Alimuuliza nani akashindwa simply tume inayoteuliwa na rais wa jamhuri ambaye pia ni mwenyeketi wa CCM na mgombea urais kwenye uchaguzi utakaosimamiwa na tume aliyoteua, tume hiyo itakuwaje huru??

Katiba inasema matokeo ya urais yakishatangazwa na tume hakuna mahali au taasisi yoyote inayoweza kuyahoji hata mahakama, tume ipo juu ya mahakama?? huko nako ni kuvunja katiba maana katiba hiyohiyo inasema mahakama ndicho chombo pekee cha kusimamia na kutoa haki!!

Mzee anatetea katiba mbovu na CCM maana anajua siku ikiondoka madarakani lazima afikishwe mahakamani kujibu tuhuma za ANBEM, EPA, RADA, KIWIRA n.k kweli sasa amekuwa mvivu wa kufikiri!!
 
Anazeeka vibaya huyu hana hoja bora akae kimya tu au ajibu maswali kuhusu ufisadi alioufanya yeye na mkewe alipokuwa madarakani.
 
Kweli la kuvunda halina ubani. HIvi mtu na akili yake anaweza kuanzisha kampuni halafu akaiita kwa majina yake na mkewe tena akiwa madarakani? Afu anwani yake anaandika IKULU. Tena kampuni hiyo hiyo ilisajiliwa silu ya tarehe 1/5 ambayo kwa kawaida ni sikukuu. Sasa mtu kama huyo anaweza kusema nini wakati huu. Mi ningekuwa yeye ningekaa kimya ana nisingependa kuonekana popote au kusema chchote.
 
Jamani nyie mlitegemea aseme nini !! kula yake na wastaafu wenzake wanaidhinishiwa na serikali hii hii na wamekuwa mzigo mkubwa kwa taifa letu. Ni bora wangepewa kiinua mgono tukaachana nao leo hii wasingekuwa na mawazo mgando kiasi hiki.
 
Tulipo anzisha mfumo wa vyama vingi tulitegemea kuona vyama vipya vinakuja na mfumo,sera tofauti na CCM lakini sasa vyama vingi vina mfumo na muundo sawa na CCM.

Wengi wanafiri katiba mpya ikianza kutumika tu basi upinzani utashinda

Wengi wanalalamika kuwa tume ya Uchaguzi si huru ukiwauliza si huru kivipi hawasemi wanashindwa kueleza

...Ameongea ukweli sana katika haya...
 
Mzee anazeeka vibaya apumzike kwa amani. Bora aende kusimamia hoteli zake kule Lushoto kuliko anavyokosa staha na kubwabwaja. Na kwa nini aseme kuishinda ccm ni vigumu?!
 
Jamani nyie mlitegemea aseme nini !! kula yake na wastaafu wenzake wanaidhinishiwa na serikali hii hii na wamekuwa mzigo mkubwa kwa taifa letu. Ni bora wangepewa kiinua mgono tukaachana nao leo hii wasingekuwa na mawazo mgando kiasi hiki.
Hastahili hata hicho kiinua mgongo. Huyu alitakiwa apelekwe mahakamani kwa ufisadi aliotufanyia akafie jela. Tazama tunavyogharimia wezi wengine kama Lowasa eti waziri mkuu mstaafu wakati tunashindwa hata kutoa mikopo ya elimu kwa wanavyuo.
 
anajua kuwa katiba ikibadilishwa kama wanavyotaka wananchi basi yeye atakuwa ni victim namba moja
 
...Ameongea ukweli sana katika haya...

aaah siyo kweli nawe sawa na mr clean, ama ni kibaraka wake? huu nao ni upotoshaji mkubwa. Wewe unatarajia sera tofauti na zilizokuwepo kwa 100% wkt watu ni walewale na nchi ileile? Tatizo la ccm sio sera bali utekelezaji wake. Zaidi ya hapo angalia cdm wana mipango na miundo tofauti na ya gamba, eg. Uongozi wa majimbo ambao utafutilia mbali makada wa gamba kama maDc,RC wanaofanya siasa kila kukicha. Unazjua sera za cdm wewe? Kalagabaho!
 
jaman mkapa mi simfahamu. Hivh ndo yule mzee;
1. Mfupi sana
2. Mnene sana
3. Anakipara
4. Mwenye matisho ktk hotuba zake
5. Mwenye lugha ya kihuni.
Kama ndo huyo nampata.
 
Huyu mzee kwanza akae kimya maana hatujasahau alivofanya biashara akiwa ikulu kinyume na katiba!! halafu bila aibu ansema watu hawawezi kueleza kwa nini tume sio huru?? Alimuuliza nani akashindwa simply tume inayoteuliwa na rais wa jamhuri ambaye pia ni mwenyeketi wa CCM na mgombea urais kwenye uchaguzi utakaosimamiwa na tume aliyoteua, tume hiyo itakuwaje huru?

Katiba inasema matokeo ya urais yakishatangazwa na tume hakuna mahali au taasisi yoyote inayoweza kuyahoji hata mahakama, tume ipo juu ya mahakama?? huko nako ni kuvunja katiba maana katiba hiyohiyo inasema mahakama ndicho chombo pekee cha kusimamia na kutoa haki!!

Mzee anatetea katiba mbovu na CCM maana anajua siku ikiondoka madarakani lazima afikishwe mahakamani kujibu tuhuma za ANBEM, EPA, RADA, KIWIRA n.k kweli sasa amekuwa mvivu wa kufikiri!!
Pia ndiye aliyeweka ripoti ya Mzee Paul Sozigwa kapuni kama alivyosema EL hayo yote yanayofanyika sasa yasingekuwepo kama ile ripoti ingetumika.

Pia ndie alimbeba EL kwa kumpa unaibu Waziri wa Ardhi wakati anajulikana ni mpenda rushwa (na hakuchukua muda mrefu EL akataka kufanya maujanja na kiwanja kile cha shule ya chekechea kilicho karibu na CMC motors opp na Maktabu Kuu bahati Mzee Sabodo ambaye nafikiri alikuwa mwenyekiti wa hiyo shule alipinga kwa nguvu zote.

Bila hivyo hapo sasa pangekuwa ofisi za CMC), akadai eti ni wazeee wamshinikize na hata kusema chaguo ni Kikwete ni huyo huyo baada ya kutishwa.

Sasa mtu kama huyo ANAYETISHWA NYAU na akina EL na wazee hana ujasiri wa kusema ukweli si ajabu kuna wazee wammtisha na kumwambia kasema hayo aliyoyasema, kwanza hana hadhi ya kuwazungumzia Watanzania ni MCHAFU
 
Ama kweli fainali uzeeni na ukistaajabu ya JK utayaona ya mkapa
 
Mkapa acha kudanganya ulimwengu. Unajua fika mwaka jana 2010 ni chama gani ilishinda. Kwanza ushukuru jinsi mnavyoendeleza wizi wa kura kwa sababu bila ivyo wengi mngekuwa ndani. Huwezi sema kuwa ccm hawawezi kushindwa katika chaguzi, Ni uongo ambao mmezoea ili kuwapumbaza walimwengu na wananchi ijulikane kuwa ccm inakubalika sana.

Wekeni tume huru uone ngoma yake. Mfano wenyewe umeona Igunga bila wizi ungeadhirika kwa kukipigia debe, ilibidi wizi lifanyike ili ccm ishinde, kukulindia heshima yako.

Ila kwa mawazo haya ustahili heshima hata kidogo ngoja tuone kama hutahama nchi hapo badae, kwa ajili ya matumizi mabaya ya madaraka. Ccm wazee wamezidi ili kulindana bora kuwachia vijana pia wakaongoza.
 
Back
Top Bottom