Asasi zataka Katiba mpya

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MTANDAO huru wa asasi za kiraia zilizojikita kufanya uangalizi wa Uchaguzi Mkuu Mkuu 2010 (TACCEO), umetoa ripoti kuhusu uchaguzi huo huku ukipendekeza mabadiliko ya katiba na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.
Wakati waangalizi hao wakitoa ripoti hiyo yenye kurasa 300 ambayo imeeleza kwa kirefu upungufu uliojitokeza na kupendekeza mabadiliko ya katiba, serikali ya Kenya imesema jukumu la kudai Katiba ni la wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Balozi wa Kenya nchini, Mutinda Mutiso, alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya haki za binadamu dunia yaliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na na Haki za Bindamu (LHCR) na kuadhimishwa jjijini Dar es Salaam jana.

Mutiso alisema ingawa Kenya ilichukua muda wa miaka 20 kupata katiba mpya, Tanznaia kazi hiyo inawezekana na muda huo unaweza kupungua kwa kutumia uzoefu toka Kenya
“Sisi tunamshukuru Mungu tumepata Katiba mpya mchakato wa ni mgumu na huchukua muda mrefu, lakini hilo kwa hapa linawezekana tena muda unaweza kupungua,” alisema Mutiso.

Mutiso alipongeza Watanzania kwa kufanya uchaguzi na kumaliza kazi hiyo kwa amani na utulivu na kuomba, hali hiyo iendelee kuenziwa.
Kwa upenda wake, Mwenyekiti wa (Tacceo), Martina Kabisama, alisema kasoro nyingi zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu, zilitokana na upungufu uliopo kwenye Katiba na Tume ya uchauzi.

“Tumefanya kazi ya uangalizi wa uchaguzi nchi nzima, tusema bila wago kuwa katika baadhi ya maeneo watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi waliegemea chama tawala na kusahau majukumu yao,” alisema Kabisama na kuongeza:
“Wapo waliochelewa kutangaza matokea makusudi kwa lengo la kuchezea haki za watu na hata kusababisha vurugu maeneo hayo, hiyo ilitokana na matokeo ya watendaji wa tume kuwa waajiriwa na wakati mwingine kuwajibika kwa aliowateua.”
Kabisama alisema inatakiwa kuundwa Tume huru ya uchaguzi itakaoyoajiri wafanya kazi wake kila majimbo na kwamba, watu hao watashughuka na uchaguzi pekee.
Naye Salumu Bar’wan, Mbunge wa Lindi Mjini kupitia CUF, alisema watu wanaopinga mabadiliko ya katiba wana masilahi binafsi.

Bar’wan alisema katiba hiyo ina upungufu mkubwa ambao kimsingi inatakiwa kuandikwa upya.
Naye Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Sengondo Mvungi, alisema kazi iliyopo hivi sasa ni kwa wanaharakati na wapenda mabadiliko kutoa elimu kwa Watanznaia juu ya umuhimu wa katiba mpya.
Dk Mvungi alisema kama Watanznaia wataelewa maana ya katiba na umuhimu wake, watashiriki kikamilifa kuidai.
 
Back
Top Bottom