nderingosha
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 4,281
- 3,243
Mifumo na sera nyingi TZ kwenye sekta ya afya wala haina shida sana(on paper).....tatizo kubwa tulilo nalo TZ ni usimamizi na utekelezaji mbovu wa mifumo/sera....na watekelezaji/wasimamizi wa mifumo/sera hizi ni WATU.....huwezi kushughulikia mifumo pasi kuwahusisha WATU......WATU ndio wanaovuruga mifumo/sera.....mfano..madaktari wanapolalamika kuwa vitendea kazi hamna mahospitalini au madawa hamna.....wanaohusika na uwepo/upatikanaji wa vitendea kazi/madawa etc ni WATU(decision makers)na si mfumo...wanaohusika na ununuzi wa vifaa feki ni WATU na si mfumo...wanaoamua wagonjwa kwenda kutibiwa nje ni WATU na si mfumo....wanaotengeneza mfumo/sera ni WATU......Mkuu wangu nadhani hunielewi na hutanielewa ikiwa utachukulia maoni yangu juu juu. Hakuna mtu anayepinga mgomo ikiwa taratibu zimechukuliwa kuhakikisha mgomo huo hautaathiri wadau wengine kwa kiwango kikubwa bali mlengwa ambaye ni serikali. Kwa mfano Ma pilot wakigoma hutazama hasara watakayo wapa shirika la ndege zaidi ya Wasafiri wenyewe. Nikiwa na maana mlengwa wa ujumbe huu wa mgomo au hata maandamano ni yule aliyeshindwa kukubali madai hayo.
Na hakika chombo pekee cha Umma ambacho kilifikia hatua ya kuanza mgomo kilikuwa Jumuiya ya watumishi wa Umma (TUCTA) ambao mwajiri wao kupitia menejimenti ya utumishi wa Umma (rais) alitoa majibu ya kwamba hawezi kuongeza mishahara ya watumishi wake hasa wenye kipato cha chini. Wakati nikitazama mgomo huu wa madaktari kwa uhalisia wake haukufikia ngazi yoyote ya kushindikana mazungumzo baina ya wadau. Isipokuwa kulikuwa na mawasiliano mabaya na jeuri baina ya viongozi wa juu ndio ulosababisha kutokuwepo kwa mazungumzo yoyote ya pande mbili.
Na nina mashaka makubwa kama wadau wengine walihusishwa kwa mfano CSSC au Ofisi ya rais - Menejimenti ya utumishi wa Umma (kule kwa Hawa Ghasia) ambao wote hawa wanahusika kulingana na mfumo wetu wa kiutawala ambao ulijengwa kuhakikisha kwamba jamii ya Watanzania inapata huduma inayokusudiwa kutoka kwa serikali kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali..
Na ndio maana wengine mnashangaa mbona imekuwa rahisi hivi ilipofika kwa rais! lakini kiundani rais ni mtu wa mwisho kabisa na maadam tumejichanganya toka nyuma madai ya haki yakageuka kuwa baina ya mashindano ya watu, ndio maana rais alitazama tu huu mgomo kama vile watu wasiojua walitendalo. Huko nyuma Jazba na hasira zimetumika zaidi ya hekima na busara na haiondoi ukweli kwamba baadhi ya viongozi wa serikali na hata madaktari waliuvua Uzalendo wao ktk kulitumikia Taifa wakachukua Uhuni na wakavua mashati yao kama kuonyesha nani mwenye nguvu. Na nilichokitaza mimi mkuu wangu sio kugoma kwa Walimu au Polisi dhidi ya serikali hii bali sura nzima ya kuonyeshana nani mwenye nguvu baina ya vyombo hivi na ndio maana siwapongezi madaktari wala serikali yenyewe hata kidogo. Ni sawa kabisa na kuanzisha vita japokuwa kuna sababu ya maana lakini kama itawagharimu wananchi kama ilivyowagharimu Somalia, sina sababu ya kuunga mkono upande wowote isipokuwa kutazama athari za vita hiyo.
Binafsi yangu mzozo mzima wa madaktari na serikali ilikuwa mchezo wa Puta... kakutukania mama yako basi mstari unapigwa na watu wananza kurushiana makonde - Bila shaka, someone will pay for this! na ninajua fika JK hiyo kesho au baadaye kuna watu watapoteza ajira zao na kibaya zaidi haitaleta nafuu yoyote kwa wananchi kwa sababu vita ilofanywa na madaktari haikulenga kubomoa mfumo ulosababisha hali hii isipokuwa baadhi ya WATU walo wakwamisha. Hata kama Mponda na Nkya wakiondolewa madarakani haitasaidia chochote ikiwa tumeshindwa kuutazama mfumo mzima wa kiutawala. Hadithi ni ile ile ya kina Lowassa, Msabah, Karamagi, Meghji, Brandina Nyoni, Diallo yaani hawa wote ni reflection ya who we are for real!..Akitoka Mponda ataingia mjinga mwingine ambaye atafuata mfumo ule ule wa dharau, uheshimiwa na kuchumia tumbo...Tatizo lenu nyote humu JF mna attack WATU badala ya MFUMO ulotufikisha hapa!