Asanteni Madaktari; mmetuonesha hatupaswi kutaliwa kwa ubabe tena!

Ukilitazama swala la sakata la mgomo wa madaktari juu juu unaweza kuwalaumu na kuwaita watu wasio na huruma na hawawatendei haki wagonjwa,wauaji,wasaliti,wamekiuka kiapo cha udaktari n.k. Kitu ambacho serikali JK na utawala kwa ujumla katika propaganda na porojo zao wanataka tuamini hivyo.

Ukilitazama kwa ndani,wakualaumiwa na kubeba lawama zote ni Mh.Rais JK,serikali na chama Tawala CCM kwa sababu zifuatazo JK katika uteuzi wa mawaziri na nafasi mbalimbali katika serikali na taasisi mbali mbali hazingatii uwezo,uzoefu na sifa za mchaguliwa bali uswaiba na masilahi katika makundi ndani ya chama tawala.

Hali ambayo inampa hali ngumu ya kutoa uamuzi wa kuwawajibisha wanapofanya ndivyo sivyo.Tatizo lingine kwa vile serikali na utawala hauna dhana ya kuwatumikia wananchi hivyo kauli nyini na ahadi wanazozitoa zinatoka katika ulimi na kubaki katika makaratasi bila kufanyiwa utekelezaji kwa maana ya kua za kisanii na porojo ili muda upite. Hakuna anaewajibika kwa kauli au ahadi serikali au JK inazozitoa kwa hali hii kutegemea ufanisi ni ndoto ya mwendawazimu.

Mambo mengi yametokea(ufisadi,rushwa,uzembe n.k) katika serikali na viongozi katika serikali na taasisi za serikali hakuna anaejiuzulu au kuwajibishwa tume baada ya tume imekwisha.Hata huko katika CCM viongozi wanaopatikana huko ni kwa njia ya rushwa na ufisadi ambapo hao ndio viongozi baadae katika serikali.

NENO KUJIUZULU KUWAJIBIKA KATIKA UTAWALA HUU HALIMO KATIKA MSAMIATI WAO.NJIA PEKEE YA KUWALAZIMISHA WAWAJIBIKE NI MIGOMO NA MANDAMANO HIVYO MGOMO WA MADAKTARI UMEONYESHA NJIA JINSI YA KUIBANA SERIKALI ITIMIZE AHADI ZAKE NA SIO POROJO.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Ukijaribu kuitazama tz ukaitafakari kwa makini kweli inafadhaisha sana huko inapoelekea.
Bado tuko nyuma kielimu lakini atlst kidogo ukilinganisha na tulipotoka licha ya kua idadi yetu pia imeongezeka.Kimtazamo ni bora ya tz ya zamani ya wakati elimu ilipokua chini kuliko hii tunayo iandaa leo.
Vijana ndio serikali na watendaji wa tz ya kesho na ya sasa lakini tumekua wazuri sana ktk porojo.
Sisi vijana wa leo tumejawa na ubinafsi na tamaa kitu ambacho ni sawa na kulichimbia hili taifa letu kaburi,nikweli hata hapo nyuma tumeyashuhudia mabaya kama meremeta richmond nk lakini bora huko tuliko toka kuliko tunapoelekea.Ukisoma post zinazotumwa humu JF zinatia moyo lakini the most tunapaswa kujitafakari je ni wasafi kiasi gani,vp uhalisia wetu ktk utendaji na mchango wetu ktk taifa?vp dhamira yetu ktk kubadili mapungufu tunayo yaona leo?Lakini hatuna dhamira yoyote zaidi ya wizi,unafiki,uzandiki na ubifsi.Sera kubwa ya vija ni chukua chako mapema lakini post ze2 humu jf ni hongereni madaktari,tumechoka kuibiwa,kwanini nchi jirani kama Rwanda wanaendelea?
kwa hali hiiiiii!
 
Watanzania mmerogwa na nani??????????? Yaani leo hii ni 2012 lakini bado majority wanafikiria Raisi ana mamlaka ya kifalme, nini maana ya RAISI na JAMUHURI in that matter???????????
 
Kila mtu ana mtazamo wake na sii vibaya kupingana japokuwa inategemea na picha uloiweka kichwani. Binafsi yangu nachukia sana Magaidi na Ugaidi upo wa aina nyingi mojawapo ikiwa ni hii ya kuchukua watu MATEKA na kuwafanya hostage ili madai yako yafanikiwe.

Na Dunia nzima tunachukia Ugaidi huu sii kwa sababu hawana madai ya hakim bali kutumia watu wasiokuwa na hatia kama ngao ya kufikisha ujumbe wako, iwe wale magaidi wa Kipalestina waliochukua wachezaji wa Israel ktk uwanja wa Olimpiki Ujarumani au Magaidi wapigania Uhuru wa Sandinista huko Nicaragua, hoja nyuma ya pazia hili ni kwa nini wanachukua wananchi wasiokuwa na hatia kabisa kuwa hostage kuhatarisha maisha na uhai wao kwa mgogoro usiowahusu ila baina ya serikali na wapambanaji..

Binafsi yangu sina matatizo kabisa na madai ya madaktari maana ni haki yao na watanzania wote kwa ujumla. Utawala huu umekuwa dhalimu sana kiasi kwamba hawajali lolote kuhusiana na utawala bora, lakini majawabu hayawezi kupatikana kwa kuwachukua wananchi mateka na hata kuhatarisha maisha yao tukihesabu vifo baada ya vifo ili machungu haya yawaumize serikali na ikubali kushindwa.

Ikumbukwe tu zipo serikali zinazosema hawawezi kusalimu amri kwa magaidi na kama haya yatakuwa maamuzi ya serikali ya JK pamoja na kwamba hatupendezewi sote, basi vifo vya raia waliokufa na wanaokufa bure na sii kwa kujitoa mhanga na vita hii vitawa hunt maisha yao yote...
Mkuu Mkandara, nakubaliana na wewe, tusema no kwa aina zote za ugaidi, hata ukipakwa siagi na jam kwa jina la mgomo!. Infact hii ni genocide dhidi ya watu masikini wa kutupwa wanaotegemea hospitali za umma!.
 
Naam!

Nimesoma na kurudia mara kadhaa taarifa ya chama cha madaktari kuhusu kusitisha mgomo na niseme kwamba nimeipenda upeo na heshima yangu kwa madaktari wetu imezidi mara elfu zaidi. Yeyote aliyesoma taarifa hiyo anaweza kuiona kuwa ni taarifa ya kutokusalimu amri (non-surrender) bali ni kauli ya kamikaze kukataa kuchukuliwa mateka. Uamuzi wa madaktari kusitisha mgomo kufuatia agizo la mahakama kuu kuwataka warudi kazini ni uamuzi ambao unahitaji kukubaliwa na kupongezwa na wale wote ambao walisimama na madaktari toka mwanzo wa mgomo huu. Binafsi na kutoka moyoni kabisa nasema madaktari wetu asanteni na heshima yangu kwenu imeinuliwa juu zaidi sasa kuliko wakati wowote ule mwingine!
Kwa kukubali kusitisha mgomo baadaya kukutana na Rais madaktari wametuonesha nani anastahili kuwajibika. Natumaini naye amejitambua hivyo.

MMM-BGM
Mkuu Mzee Mwanakijiji, nakupongeza kwa uwezo wako mkubwa wa kosoma na kuchambua in between the lines, mimi nilikuwa pale ukumbini nikirekodi kile kipindi changu cha TV, statement hii niliiona, ila kwa uwezo wangu, niliona sentensi moja tuu, "madaktari kurejea kazini" unconditional, yaani macho yangu hayakuona conditions yoyote!.

Nakushauri, uchambuzi makini na mahiri kama huu, unahitajika zaidi kule kwenye lile jumba kuu letu, hivyo natao mwito kwako kufikiria kuzogeza mapambano ground zero!.

Asante

Pasco.
 
Genocide hii inasababishwa na nani? Nachelea haujaelewana na Mkandara...
Mkuu Mkandara, nakubaliana na wewe, tusema no kwa aina zote za ugaidi, hata ukipakwa siagi na jam kwa jina la mgomo!. Infact hii ni genocide dhidi ya watu masikini wa kutupwa wanaotegemea hospitali za umma!.
 
Madaktari wamefanya kitu kikubwa sana kwa kuwaamsha watanzania na pia wametuma ujumbe mzito na wa ukweli kwa raisi kikwete. Wasiwasi wangu ni kama kikwete atazingatia tamko la madaktari juu ya wateule wake.

Sidhani kuwa Kikwete atazingatia tamko la madaktari juu ya wateule wake kwa sababu moja kubwa, hajali maisha ya wananchi na pia sio mtu serious wa kuweza kutatua matatizo magumu!!
 
Mkuu Mkandara, nakubaliana na wewe, tusema no kwa aina zote za ugaidi, hata ukipakwa siagi na jam kwa jina la mgomo!. Infact hii ni genocide dhidi ya watu masikini wa kutupwa wanaotegemea hospitali za umma!.

Pasco ni jambo la busara kuhakikisha kuwa unaelewa vizuri maana ya maneno na uhalisia wake kabla ya kuyatumia; hapa kwenye post yako unasema kuwa kitendo cha madaktari kugoma ni sawa na genocide!!! Ili kuwe na mauaji ya kimbali[ genocide] ni lazima kuwe na intention to eliminate a specific targeted group of people na pili hiyo intention itekelezwe. Je madhumuni ya madaktari yalikuwa kumueliminate nani na kwanini? Je hiyo intention ilikuwa executed? Madtari walikuwa wanadai better working conditions to save the lives of poor people instead of pretending to save lives when people die because of lack of basic equipment!! To you Pasco that is genocide!!
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, nakupongeza kwa uwezo wako mkubwa wa kosoma na kuchambua in between the lines, mimi nilikuwa pale ukumbini nikirekodi kile kipindi changu cha TV, statement hii niliiona, ila kwa uwezo wangu, niliona sentensi moja tuu, "madaktari kurejea kazini" unconditional, yaani macho yangu hayakuona conditions yoyote!.

Nakushauri, uchambuzi makini na mahiri kama huu, unahitajika zaidi kule kwenye lile jumba kuu letu, hivyo natao mwito kwako kufikiria kuzogeza mapambano ground zero!.

.
Bolded red. ndo mwisho.
Mwanakijiji asitake kuuaminisha umma hisia zake.
Ni mara ngapi Mzee Mwanakijiji anajadili speculation, tetesi, classifieds?
Acha kupotosha.
 
Hapana siyo kuheshimu madaraka ya mkuu wa nchi kwani hakuna mahali popote ambapo Ikulu iliwataka madaktari kurudi kazini mara moja bali mahakama ndiyo imefanya hivyo?

Naona sigma ameshai'elaborate hii hoja hapo juu, Pia kama unakumbuka Mzee Mwanakijiji majibu ya MAdaktari kufuatia tamko la Mahakama kuu ilikuwa ni kwamba lile tamko halikufuata taratibu kadhaa hivyo lilibaki kuwa ushauri wa Mahakama na sio ORDER ya mahakama!...On top ya alichosema Sigma ni kwamba Mh. Presidaa alimwamuru mwanasheria mkuu Immediately aliondoe lile tamko(wakati wa kikao na maDR)--(hizi ni habari za ndani)..
Kwenye kikao cha maDr cha kusitisha mgomo, hakuna mahali ilipokuja hoja ya mahakama Kuu, hoja zilikuwa ni mazungumzo ya Ikului...Hivyo Ieleweke kwamba Mgomo ulisitishwa kwa kuheshimu Mamlaka ya Mh Raisi na sio kwa Tamko la mahakama Kuu!
 
Could the Doctors move be called the people's power? can the people's power make the giants bend?
 
Madaktari wamefanya kitu kikubwa sana kwa kuwaamsha watanzania na pia wametuma ujumbe mzito na wa ukweli kwa raisi kikwete. Wasiwasi wangu ni kama kikwete atazingatia tamko la madaktari juu ya wateule wake.
JK aamue kuzingatia tamko la madaktari au aache kikubwa ujumbe umefika na kwangu mimi dalili ya mabadiliko yaja sasa, naomba na sekta zingine tuamke ili hatimaye tuweze kufurahia kuitumikia nchi yetu badala ya Tanzania kugeuka kiwanda cha kuzalisha wataalam wanaoenda kuendeleza nchi zingine.
 
Sijui ni kwa nini kulikuwa na kusudio la kukutana na wazee (wa ccm).

Tunajua rais ni mtu wa maneno matamu na mjuzi wa kutoa ahadi, kwenye hili la madaktari ujanja huo hautamsaidia. Madaktari wameonyesha msimamo thabiti na hawakujiingiza kwenye jazba hata pale waziri mkuu alipokuja na hoja za kushambulia watu binafsi.

Ni wakati wa rais kutenda na ionekane hivyo kwa wasaidizi wake
Akutane na Wazee wa Dar.Jumatatu na atumie jukwaa hilo kutangaza kuvunja baraza la mawaziri au kuwafukuza kazi waziri wa Afya na naibu wake hapa kidogo atakua ameeleweke.Akienda kupiga soga na usanii atakua amejiwekea kitanzi.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
mkuu uliyeandika thread shukran,kuna kipindi roho yangu ilinisuta kwa maamuzi ya kugoma but i believe it was for the best ya watanzania....wale ambao wanaponda kwamba tuliacha watu wafe kwaajili ya kusikilizwa kumbukeni siye sio malaika ili tufanye kazi tunahitaji vifaa na vipimo,yaani inshort watanzania wengi wamekufa kutokana na uzembe wa viongozi husika ila hamkuvisikia wala kuvijua coz hatuvitangazi.jamani viongozi hawa tumewachagua siye na hiyo ina maana wanatufanyia kazi siye,so wakiteleza ni lazima tuwawajibishe.....
 
inabidi tuanze kutangaza hadharani kila kifo kinachotokea hospitali. Maana vifo vinavyotokea siku zote wananchi hawaoni ni sababu ya viongozi waliojigeuza wao watawala wa nchi hii.
 
Binadamu yeyote ana nafasi ya kufanya chochote ili mradi tu awe jasiri, mvumilivu, mchapakazi na asiyeridhika mapema. Kama watanzania tutakuwa na tabia hii hata kwa siku 5 tu, nchi hii itaanza mabadiliko kuelekea tunapotaka
by Godbless Charles(mjumbe wa jumuia ya madaktari)
 
Ukilitazama swala la sakata la mgomo wa madaktari juu juu unaweza kuwalaumu na kuwaita watu wasio na huruma na hawawatendei haki wagonjwa,wauaji,wasaliti,wamekiuka kiapo cha udaktari n.k. Kitu ambacho serikali JK na utawala kwa ujumla katika propaganda na porojo zao wanataka tuamini hivyo.

Ukilitazama kwa ndani,wakualaumiwa na kubeba lawama zote ni Mh.Rais JK,serikali na chama Tawala CCM kwa sababu zifuatazo JK katika uteuzi wa mawaziri na nafasi mbalimbali katika serikali na taasisi mbali mbali hazingatii uwezo,uzoefu na sifa za mchaguliwa bali uswaiba na masilahi katika makundi ndani ya chama tawala.

Hali ambayo inampa hali ngumu ya kutoa uamuzi wa kuwawajibisha wanapofanya ndivyo sivyo.Tatizo lingine kwa vile serikali na utawala hauna dhana ya kuwatumikia wananchi hivyo kauli nyini na ahadi wanazozitoa zinatoka katika ulimi na kubaki katika makaratasi bila kufanyiwa utekelezaji kwa maana ya kua za kisanii na porojo ili muda upite. Hakuna anaewajibika kwa kauli au ahadi serikali au JK inazozitoa kwa hali hii kutegemea ufanisi ni ndoto ya mwendawazimu.

Mambo mengi yametokea(ufisadi,rushwa,uzembe n.k) katika serikali na viongozi katika serikali na taasisi za serikali hakuna anaejiuzulu au kuwajibishwa tume baada ya tume imekwisha.Hata huko katika CCM viongozi wanaopatikana huko ni kwa njia ya rushwa na ufisadi ambapo hao ndio viongozi baadae katika serikali.

NENO KUJIUZULU KUWAJIBIKA KATIKA UTAWALA HUU HALIMO KATIKA MSAMIATI WAO.NJIA PEKEE YA KUWALAZIMISHA WAWAJIBIKE NI MIGOMO NA MANDAMANO HIVYO MGOMO WA MADAKTARI UMEONYESHA NJIA JINSI YA KUIBANA SERIKALI ITIMIZE AHADI ZAKE NA SIO POROJO.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Umenena kweli mkuu,Kitendo cha rais kukutana na madaktari na wakakubali kusitisha mgomo wao kinadhihirisha kuwa lawama zote za mgomo huu wa pili zimwendee rais mwenyewe.Alikuwa wapi mpaka hali ifikie hapo alipoikuta? Baada ya watu wake kushindwa kuwatuliza alitakiwa atamke neno mapema kama baba mwenye nyumba.Ni vema rais akawa anafuatilia mambo na kunusuru kabla hali ya jambo haijawa mbaya.NAWAPONGEZA MADAKTARI KWA KURUDI KUWAHUDUMIA WANANCHI.
 
Ndugu yangu naona uanchanganya kuchukua mateka na kugoma! Hivi waalimu wanapogoma kufundisha wanamchukua nani mateka? Na je polisi wakigoma kuripoti wanakuwa wamemchukua nani mateka? Sasa daktari yeye akitaka kugoma ili asikilizwa afanyeje? akalale na maiti? Nadhani ungetafuta neno zuri kutetea hoja yako kuliko kudai kwamba mtu anachukuliwa mateka katika swala hili!
Mkuu wangu nadhani hunielewi na hutanielewa ikiwa utachukulia maoni yangu juu juu. Hakuna mtu anayepinga mgomo ikiwa taratibu zimechukuliwa kuhakikisha mgomo huo hautaathiri wadau wengine kwa kiwango kikubwa bali mlengwa ambaye ni serikali. Kwa mfano Ma pilot wakigoma hutazama hasara watakayo wapa shirika la ndege zaidi ya Wasafiri wenyewe. Nikiwa na maana mlengwa wa ujumbe huu wa mgomo au hata maandamano ni yule aliyeshindwa kukubali madai hayo.

Na hakika chombo pekee cha Umma ambacho kilifikia hatua ya kuanza mgomo kilikuwa Jumuiya ya watumishi wa Umma (TUCTA) ambao mwajiri wao kupitia menejimenti ya utumishi wa Umma (rais) alitoa majibu ya kwamba hawezi kuongeza mishahara ya watumishi wake hasa wenye kipato cha chini. Wakati nikitazama mgomo huu wa madaktari kwa uhalisia wake haukufikia ngazi yoyote ya kushindikana mazungumzo baina ya wadau. Isipokuwa kulikuwa na mawasiliano mabaya na jeuri baina ya viongozi wa juu ndio ulosababisha kutokuwepo kwa mazungumzo yoyote ya pande mbili.
Na nina mashaka makubwa kama wadau wengine walihusishwa kwa mfano CSSC au Ofisi ya rais - Menejimenti ya utumishi wa Umma (kule kwa Hawa Ghasia) ambao wote hawa wanahusika kulingana na mfumo wetu wa kiutawala ambao ulijengwa kuhakikisha kwamba jamii ya Watanzania inapata huduma inayokusudiwa kutoka kwa serikali kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali..

Na ndio maana wengine mnashangaa mbona imekuwa rahisi hivi ilipofika kwa rais! lakini kiundani rais ni mtu wa mwisho kabisa na maadam tumejichanganya toka nyuma madai ya haki yakageuka kuwa baina ya mashindano ya watu, ndio maana rais alitazama tu huu mgomo kama vile watu wasiojua walitendalo. Huko nyuma Jazba na hasira zimetumika zaidi ya hekima na busara na haiondoi ukweli kwamba baadhi ya viongozi wa serikali na hata madaktari waliuvua Uzalendo wao ktk kulitumikia Taifa wakachukua Uhuni na wakavua mashati yao kama kuonyesha nani mwenye nguvu. Na nilichokitaza mimi mkuu wangu sio kugoma kwa Walimu au Polisi dhidi ya serikali hii bali sura nzima ya kuonyeshana nani mwenye nguvu baina ya vyombo hivi na ndio maana siwapongezi madaktari wala serikali yenyewe hata kidogo. Ni sawa kabisa na kuanzisha vita japokuwa kuna sababu ya maana lakini kama itawagharimu wananchi kama ilivyowagharimu Somalia, sina sababu ya kuunga mkono upande wowote isipokuwa kutazama athari za vita hiyo.

Binafsi yangu mzozo mzima wa madaktari na serikali ilikuwa mchezo wa Puta... kakutukania mama yako basi mstari unapigwa na watu wananza kurushiana makonde - Bila shaka, someone will pay for this! na ninajua fika JK hiyo kesho au baadaye kuna watu watapoteza ajira zao na kibaya zaidi haitaleta nafuu yoyote kwa wananchi kwa sababu vita ilofanywa na madaktari haikulenga kubomoa mfumo ulosababisha hali hii isipokuwa baadhi ya WATU walo wakwamisha. Hata kama Mponda na Nkya wakiondolewa madarakani haitasaidia chochote ikiwa tumeshindwa kuutazama mfumo mzima wa kiutawala. Hadithi ni ile ile ya kina Lowassa, Msabah, Karamagi, Meghji, Brandina Nyoni, Diallo yaani hawa wote ni reflection ya who we are for real!..Akitoka Mponda ataingia mjinga mwingine ambaye atafuata mfumo ule ule wa dharau, uheshimiwa na kuchumia tumbo...Tatizo lenu nyote humu JF mna attack WATU badala ya MFUMO ulotufikisha hapa!
 
Mkuu Mkandara, nakubaliana na wewe, tusema no kwa aina zote za ugaidi, hata ukipakwa siagi na jam kwa jina la mgomo!. Infact hii ni genocide dhidi ya watu masikini wa kutupwa wanaotegemea hospitali za umma!.

Genocide hapa mr. Pasco ni debatable

watawala hawawajibiki ipasavyo wakijua kuwa madaktari hawataweza kugoma, hivyo watawala wanatumia ngao ya 'huruma' ya madaktari kwa wagonjwa, upande mwingine watawala wanajua kabisa wananchi wengi watakuwa kinyume na madaktari

Genocide hapa wanao ifanya ni watawala
 
Back
Top Bottom