Asanteni kwa mawazo yenu

sweetlady kuondoka rahisi dear lakini sharti lake unajua huyu bwana anasema watoto atawachukua na watoto wangu wote wa kike maskini nimewazaa kwa tabu na mama angu na ndugu zangu wote wamenisamehe mama angu ananiambia niachane nae ni mnyama huyu mara nyingi tu nimetolewa humu ndani nafukuzwa bila viatu kisa ukimtell kama y unarudi alfajiri

Anakutisha ili aendelee kukunyanyasa, ujue wanaume wengi wanatumiaga udhaifu wetu wa kuwapenda watoto kututesea, USIKUBALI, mateso yako ni makubwa mno.. Nenda kwenye vyombo vya sheria na utapata haki yako. Kwanza hakuna mwanaume mwenye ruhusa ya kuishi na watoto wenye umri chini ya miaka 7, haijalishi ni wakwake..

Nenda ustawi wa jamii, nenda hata police kamshtakie hayo mateso anayokupa, utapata msaada wa dhati.. Nshakuambia tena huyo mumeo ni muuaji, na asipokuua kwa vipigo, atakuua kwa ukimwi.. Mshirikishe mamako na ndugu zako.. Watakusaidia.. Pole sana..
 
mama weeee! Sweetlady kapandisha mzuka.
Hahaha... Utasutwa wewe, shauri yako... Nasikitika bana mdada anateswa na mumewe wa ndoa.. Wanaume wengne utafikiri hawajazaliwa na wanawake.. Inatia hasira bana. ..
 
Habari zenu wapendwa mie mwenzenu nimepatwa na kasheshe nyingine sasa, mume alinisusia wiki tatu alikuwa haongei na mimi. Alikuja kuongea juzi, mnajua kani miss eti he he wanaume wakiwa na haja yao ndo wanakufata kwa uongo. Sasa baada ya mwezi ndo kaja kukutana kimwili dakika 5 na kadischarge ndani kinguvu bila permission yangu.

Sasa naomba kuuliza nitakuwa nimeshika mimba au la nilipata period tarehe 10 nilimaliza 16 tumeonana tarehe 24 je naweza kushika mimba niliomba msaada kwenye JF doctor lakini naona wengine wananitosa wanafikiri nataka kuua,je mngekuwa nyinyi dada zangu na jitu kama hili la kutesa mngekubali kupata tena mtoto na hapa na mtoto bado miezi 4 nisaidieni.
 
ndiyo unataka kuua, unadhani kutoa mimba ni kutumbua jipu?

na utaua watoto wangapi maishani mwako kwa kisingizio cha kutoa mimba, kama unabakwa na huchukui hatua, unakimbilia JF kulalamika, unashauriwa hufuati ushauri, unabakwa tena unarudi JF.... hivi mwisho wa hii circle ya kubakwa-JF-abortion-kubakwa-JF-abortion itakoma lini?

hebu zinduka wewe, kuna wanawake walikuwa na shida kubwa kushinda zako na wameshinda. tatizo lako muoga wa kusema haya manyanyaso sasa basi na usimame kidete kama mwanamke wa shoka kuitetea heshima yako na maisha ya watoto wako dhidi ya huyo mumeo fedhuli

hebu simama sasa!

acha kulialia na kujiita unlucky, chukua hatua mara moja, sema moyoni mwako kuwa enough is enough na uondoke kurekebisha hatima yako na ya watoto wako.

na sisi tutakuombea upate kushinda na zaidi ya kushinda maana vita yako ni takatiffu. usiogope Mungu atakuwa pamoja nawe!
 
asante miss judith

mpendwa,

futa wazo la kutoa mimba kichwani mwako kisha acha kulialia, hebu chukua hatua bana unatuangusha wanawake wenzio! utalialia hadi mwaka gani?

hebu simama mpendwa, kama unahitaji msaada wangu wowote, niPM

ubarikiwe
 
Habari zenu wapendwa mie mwenzenu nimepatwa na kasheshe nyingine sasa, mume alinisusia wiki tatu alikuwa haongei na mimi. Alikuja kuongea juzi, mnajua kani miss eti he he wanaume wakiwa na haja yao ndo wanakufata kwa uongo. Sasa baada ya mwezi ndo kaja kukutana kimwili dakika 5 na kadischarge ndani kinguvu bila permission yangu. <br /> <br /> Sasa naomba kuuliza nitakuwa nimeshika mimba au la nilipata period tarehe 10 nilimaliza 16 tumeonana tarehe 24 je naweza kushika mimba niliomba msaada kwenye JF doctor lakini naona wengine wananitosa wanafikiri nataka kuua,je mngekuwa nyinyi dada zangu na jitu kama hili la kutesa mngekubali kupata tena mtoto na hapa na mtoto bado miezi 4 nisaidieni.
<br /> <br / tatizo lk ni kutokujiamini unahofu kw ukitetea haki yk mume atakuacha, unampenda sn mumeo lkn mume hakupendi tn anakudharau. ndgu simamia haki yk utadhalilishwa hd lini? mumeo atakutesa na atakuzalisha sn ukichakaa anakufukuza anaoa mke mwngn
 
nampenda sana mume wangu hata mwanaume mwingine simwangalii nakuwa sina time nao hata mtu akinitongoza namwambia mume wangu niko honest but still ndo hivyo
<br /> <br / aisee ht mm nampenda saaana mume wng na nimelala naye kwnye maboksi mpaka ss tnamiliki mali kadhaa lakini siwez vumilia aninyanyase ht kidogo, yn aisee haiwezekani km ni pesa ntatafuta yn nachapa wendo, MUNGU YUPO ATAMLIPA mi cjui ww unang'ang'nia nn? Hy mumeo ni mwarabu?mana ndo tabia zao hz.
 
Pia maisha si kukomoana, bali nyendo zake hizo zitamfikisha mahali atakutafuta na kukupigia magoti!
Je njia za kusuluhisha ndoa hii zote zimeshindikana?
Huoni kuwa labda wewe binafsi una tabia moja ya kishenzi inayom'boa sana bwanako, maana si rahisi ukajiona!
Kweili kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni, lakini maoni haya ya kuwa "mmoja kutoka nje ya ndoa kunasababishwa na kukosa kitu fulani toka kwa mwezake" ni hoja ambayo haikubaliki. Ikiwa tu mdau katika ndoa atakumbuka ahadi ya ndoa kamwe hatofikiria kwenda nje ya ndoa ili kujaza pengo.

Nafikiri kuna kitu ambacho kimemfanya mume wako awe na hizo tabia
Angalia mienendo yako na ujichunguze mahali ambapo ulikosea na ujirekebishe mapema
Kwenda nje ni kumkomoa mumeo na hapo hujafanya lolote la maana
Je ushawashirikisha wazazi au mshenga wa ndoa yako kabla ya kufikia maamuzi haya
Hivi mume kuwa na tabia mbaya (kama ya ulevi, uzinzi, dharau, maneno machafu, kumpiga mkewe) kunasababishwa na tabia mbaya za mke? Nahisi kama kuwaza hivi ni kuishi katika himaya ya "mfumo dume".

Badala ya kufikiria mawazo ya kwenda nje ili kulipiza yale anayofanya mme wako, ni vema ukautumia huo muda kufanya utafiti wa kina kufahamu ni nini anachokikosa kwako mme wako ili ukifanye kiwepo na asiwe na mawazo ya kwenda kukitafuta nje.
[Maelezo ya juu yanahusu hoja hii pia]
kila mwaka nazalishwa mtoto mmoja ili niwe busy na watoto ye afanye mambo yake hivi kweli jamani wanaume wanaroho ngumu namna hiyo now nimepatwa na matatizo fulani ya magoti kulia nikichuchuma au nikibend zinalia sielewi ni nini au yale maji ya uchungu yanaifect naomba ushauri
Na wewe dada yangu umezidi! Eti "kila mwaka nazalishwa mtoto mmoja". Karibi siamini ninachokisikia! Utakubalije mtu mzima na akili zakoi uzalishwe? Hivi huelewi njia yoyote ya kukufanya usizae kama kutaki?
Anyway, pole sana kwa yote.
 
sweetlady kuondoka rahisi dear lakini sharti lake unajua huyu bwana anasema watoto atawachukua na watoto wangu wote wa kike maskini nimewazaa kwa tabu na mama angu na ndugu zangu wote wamenisamehe mama angu ananiambia niachane nae ni mnyama huyu mara nyingi tu nimetolewa humu ndani nafukuzwa bila viatu kisa ukimtell kama y unarudi alfajiri
Kwanza naungana na hasira za SweetLady! Unlucky, umejilegeza sana. Kila mara "Bwana anasema", "Ninamwachia Mungu"... hakuna cha bwana kasema wala cha kumwachia Mungu. Mungu anasaidia wale tu wanaojisaidia na wala sio wale wanaolialia tu na kusubiri kudra ya Mungu. Ukiwa hivi nakuhakikishia hutopata chengine zaidi ya majeraha ya kipigo cha mumeo, makovu ya unyanyasaji wake na hatimae kifo.
Kwenye red, suala la watoto ninavyoelewa watoto ama ni wako au wenu lakini sio wake peke yake. Kwa hivyo, chukua watoto wako, rudi kwenu, akija kutaka watoto mwambie aende akawadai mahakamani. Tafuta ushauri toka chama cha wanasheria wanawake. Wasiliana na Miss Judith kwa ushauri zaidi. Wewe mwanamke wewe, wacha kulialia, kaza buti, jikomboe.
 
asanteni sana wapendwa kuzaa sio mimi bwana mwenyewe anataka watoto watano but mimi sitaki ndo sasa nimefunguka macho nitaenda kuwekesha vijiti na nilirudi mara nyingi nyumbani kwetu lakini huko ndugu zangu wifi yangu anaroho mbaya hapendi sie tukae pale anafanya visa mpaka utaona karaha na kaka ndo huyo katutupa hatujali baba ndo kafariki mama hawezi kufanya kitu na sio mimi na dada angu pia hali yake kama yangu nae anavumilia hatuna pakwenda wapendwa dah ndo hivyo mwishwe tutolewe roho
 
Mimi nina ushauri mmoja tu kwako, kusali umesali sana, na unamfanyia yote mema ambayo hata sie hatufanyi na bado unadharauliwa ,

Kama hajaweza kukuendeleza kielimu ama kikipato kwa miaka yote 6 mliyoishi pamoja, wewe uko naye unasubiri nini? Au ni unaishi 'a Tanzanian dream' ile dream ya kuwa married ndio kipimo cha mwanamke?

Funguka dada, achana na huyo mwanaume na urudi kwa mama yako ukae utafute cha kufanya, kama ni kisomo ama kazi, je elimu yako ni ya kiwango gani?

Kuhusu watoto , hii ni excuse ninaisikia kila kukicha kuwa nataka niondoke lakini watoto!! Watoto hawatakufa njaa, mwachie hapo nenda ondoka hata leo usitake mpaka akupatie Ukimwi ama ulemavu, sikubaliani na yeyote anayesema umuombee ili abadilike! Christ! Hata Mungu hapendi tukae kwenye abusive relationship in the name of love...

Naomba ukija kucomment uelezee mpango wako wa maisha ya baadae huku ukiwa kwa mama...mwanaume hajakugusa miezi anakugusa only once na ndio siku anayocheka na wewe ?!

Bidada pls fuata ushauri wa sweetlady

Kuna dada mmoja amesema tabia zako za kishetani, sielewi kwanini watu mko mbio kuhukumu, kwanini usiseme tabia za mwanaume za kishetani ilhali zimeonyeshwa, unapomsema mwenzio ana upeo mdogo wa uchambuzi wa mambo, haisaidii, ile kuleta mada yake humu ni hatua, ujue safari ya hatua elfumoja huanza na hatua moja...

Dada usikonde na mawazo hebu toka kwa bazazi huyo, hujazaliwa kwa ajili yake, na hata ukitoka sio umekashfu Mungu wako, endelea kumtumikia kwa uhuru nje ya huyo mpigaji, mnyanyasaji,mlevi,mzinzi na mbakaji yes! Majina yote yanamfaa yeye
 
Pia maisha si kukomoana, bali nyendo zake hizo zitamfikisha mahali atakutafuta na kukupigia magoti!
Je njia za kusuluhisha ndoa hii zote zimeshindikana?
Huoni kuwa labda wewe binafsi una tabia moja ya kishenzi inayom'boa sana bwanako, maana si rahisi ukajiona!

paka huyu dada anahitaji ushauri najua no one can write ubaya wake ila ni vyema tukamweleza maneno ya kumfariji
ni vip umuhukumu.
huyo mwanaume ndio anatabia ya kishenzi na ndio maana mwanamke amelalama humu jf.
 
Mens. cycle yako ni ya siku ngapi (26, 28 au 30)?, kwa details ulizotoa uwezekano wa mimba kutunga kwa tarehe hiyo ni 100%+-0.5 na hasa kama mzunguko wako ni wa siku 28, yaani hiyo tarehe ndo ilikuwa kwenye redi hasa (ovulation) day. Unless kama homorne zako zilikuwa zimebadilika. Pole sana.
 
mie nimesoma mpaka form four na computer corse pia na nilikuwa nafanya kazi kabla ya kuolewa kwenye bank ndo huyu bwana nilimpata hukohuko mpaka kaniachisha kazi na mie menstruation cycle yangu ni 34 mie namvumilia huyu bwana coz nampenda kufa sana sana sijui kaniroga dah
 
Mimi nina ushauri mmoja tu kwako, kusali umesali sana, na unamfanyia yote mema ambayo hata sie hatufanyi na bado unadharauliwa ,

Kama hajaweza kukuendeleza kielimu ama kikipato kwa miaka yote 6 mliyoishi pamoja, wewe uko naye unasubiri nini? Au ni unaishi 'a Tanzanian dream' ile dream ya kuwa married ndio kipimo cha mwanamke?

Funguka dada, achana na huyo mwanaume na urudi kwa mama yako ukae utafute cha kufanya, kama ni kisomo ama kazi, je elimu yako ni ya kiwango gani?

Kuhusu watoto , hii ni excuse ninaisikia kila kukicha kuwa nataka niondoke lakini watoto!! Watoto hawatakufa njaa, mwachie hapo nenda ondoka hata leo usitake mpaka akupatie Ukimwi ama ulemavu, sikubaliani na yeyote anayesema umuombee ili abadilike! Christ! Hata Mungu hapendi tukae kwenye abusive relationship in the name of love...

Naomba ukija kucomment uelezee mpango wako wa maisha ya baadae huku ukiwa kwa mama...mwanaume hajakugusa miezi anakugusa only once na ndio siku anayocheka na wewe ?!

Bidada pls fuata ushauri wa sweetlady

Kuna dada mmoja amesema tabia zako za kishetani, sielewi kwanini watu mko mbio kuhukumu, kwanini usiseme tabia za mwanaume za kishetani ilhali zimeonyeshwa, unapomsema mwenzio ana upeo mdogo wa uchambuzi wa mambo, haisaidii, ile kuleta mada yake humu ni hatua, ujue safari ya hatua elfumoja huanza na hatua moja...

Dada usikonde na mawazo hebu toka kwa bazazi huyo, hujazaliwa kwa ajili yake, na hata ukitoka sio umekashfu Mungu wako, endelea kumtumikia kwa uhuru nje ya huyo mpigaji, mnyanyasaji,mlevi,mzinzi na mbakaji yes! Majina yote yanamfaa yeye

dada Nsiande naona umecharuka!

nami naungana na wewe hapo kwenye bold (pamoja na yote niliyomuasa) "afunguke" na Mungu atamsaidia.

ubarikiwe sana dada
 
mie nimesoma mpaka form four na computer corse pia na nilikuwa nafanya kazi kabla ya kuolewa kwenye bank ndo huyu bwana nilimpata hukohuko mpaka kaniachisha kazi na mie menstruation cycle yangu ni 34 mie namvumilia huyu bwana coz nampenda kufa sana sana sijui kaniroga dah
<br /> <br / kama ni ushauri umeshapewa wakila aina na wachangiaji tofauti tofauti bado unasema huyu MUME UNAMPENDA SANA SANA inamaana pamoja na mateso unayopata kamwe huwezi kumwacha mumeo sasa ndugu yngu ungeweka wazi ni msaada gani unapenda upewe na wana jf? 1. Wa maombi 2.wa kazi (ajira) 3. Kiafya au 4. Iundwe tume tk jf ije iongee (imrekebishe) mumeo? Mana sielewi hatima ya ushaur wa wana jf.
 
hapo penye kuunda tume nimepapenda, nadhani ndilo lililobaki sasa, manake kishashauriwa sana na hataki kuchukua hatua yoyote, yeye kila kukicha anakuja kulialia hapa JF! kama ni huruma tumeishamhurumia na kama ni ushauri, tumeishamshauri mengi sana, imebaki kwake kuchukua hatua!

ubarikiwe mpendwa
 
Back
Top Bottom