Asanten sana wana JF kwa ushauri wenu,nimefanikiwa kumaliza tatizo na x bf wangu.

Nilileta uzi hapa usemao;'Nisaidien nifanye nn ili aniache na maisha yangu'.Nashukuru nilipata mawazo mengi sana kutoka kwenu,na jtano iliyopita nikayatumia kwa kuwafuta maraki zake 2 wanaommudu nikawaeleza situation nzima,kesho yake wakaonana nae wakataka kujua kwanza 7bu za yeye kunifanya vile akawaambia ananihitaji kwa garama yoyote kwana ndoa yake haina aman na mkewe karudi kwao alimpiga mpaka mimba aliyokuwa nayo ikatoka na wazazi wa mke wamemwambia akachue mahari yake so akaona mtu pekee wa kuweza kumwelewa na kuishi nae ni mimi ndio maana yuko radhi kwa lolote ili mradi turudiane,wakamwambia poa asinisumbue tena kwa vitisho wao wataongea na mimi.

Ijumaa tukakutana tena na wale marafiki zake na kujadili tutumie njia gani, basi nikawapa wazo niliipata humu ya kuwa tutafute cheki cha kuonesha nimeathirika ajue hatuwezi kurudiana,kweli wale marafiki zake wakakubali mmojawao ana rafiki yake ni daktari akaongea nae jana akapata cheti tena chenye tarehe ya mwezi wa nne na kinachoonyesha nimeathirika na ninahudhuria cklinic.

Basi jana jioni tukenda nyumbani kwa mmojawapo wa wale marafiki zake na yeye akaja wakamwambia wameongea na mimi nami nimeomba nimjibu maombi yake mbele ya rafiki zake, nikaanza kwa kumpa pole na matatizo ya ndoa yake then nikamhadithia kuwa nilipoachana nae nilipata bwana akaniambukiza ukimwi na sasa naumwa nikamwonyesha na vyeti vyenye maelezo ya kuugua kwangu,pale ilibidi nivute hisia mpaka machozi yakawa yanatoka ili aamini,basi kusikia vile alistuka yani akawa kama amechanganyikiwa flan akawa ananitizama kwa woga, alisikitika sana na akajiona yeye ndio alisababisha kwan tusingeachana nisingepata hayo matatatizo.


Kwa kweli alijutia sana na akaniomba nimsamehe na akanishukuru kwa kutolipiza kisasi kwan ningeweza kukubali turudiane ili nimwambukize,kwakweli tangu mda ule alikosa amani alikuwa mwoga,hata maneno yakawa yanakatika katika akiongea,akaniahidi pale pale kuwa hatarudia tena kunisumbua kwa namna yoyote ile na kuanzia cku ile ataniheshimu sana kwan nimeyajali sana maisha yake kwa kuwa mkweli kwake,akanitaka niwe na amani kabisa,hata kama nikipata mwanaume atakaeridhika kuwa nami ktk kuugua kwangu yeye ameridhika kabisa na wala hatanifatilia tena,tukamaliza kikao yeye akasema kuna mahali anawahi so akaondoka akatuacha, kwakweli atulicheka sana alipoondoka kwani jamaa aliogopa hata kunipa mkono tuagane,wakuu nashukuruni sana sana kwani sasa nina aman tele moyoni,mungu awabariki sana.

una uhakika huyo jamaa haingii humu jf/mmu? maana.......
 
Amani ya moyo haitafutwi hivi dada yangu,lakini kama una enjoy haina tatizo endelea na maisha yako

Niliamua kutumia njia hii kutokana na mtu mwenyewe,hope mungu atanisamehe kwa hili kwan nia yangu ilikuwa kutafuta amani ya moyo wangu kwa namna ambayo isingenipa madhara wala kumdhuru mwingine.
 
siri ni ya mtu mmoja, umeuhusisha hao rafiki zake, tegemea siri kuvuja.
 
Duh! umwemweza..lakini Je? ingekuwaje kama naye angekudanganya kuwa alishathirika miaka mingi iliyopita ila aliogopa kukwambia?
 
Duh! kumbe watu wengine mpaka watishwe na H.I.V ndio wanaogopa, haya shosti relax ule happy ......
 
siri ni ya mtu mmoja, umeuhusisha hao rafiki zake, tegemea siri kuvuja.
Mbele ya ngoma hata aambiwe ilikuwa uongo anavyoiogopa wala hatanitafuta, hana hamu hata ya kuniona tena mkuu!
 
Duh! umwemweza..lakini Je? ingekuwaje kama naye angekudanganya kuwa alishathirika miaka mingi iliyopita ila aliogopa kukwambia?
Kwa matatizo aliyonayo, nikamwongezea na ya kwangu akili ilishasizi akabaki amechanganyikiwa tu na wala hakuweza kuwaza hilo!
 
Back
Top Bottom