Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,806
- 59,288
Nadhani baadhi yetu kama sio wengi tunajua nguvu ya neno asante na umuhimu wa kushukuru pale mtu/watu wengine wanapokua wamejituma, jitolea kwaajili yetu.Kwa kushukuru mtu anapokuwia mkarimu inafanya kesho awe tayari kuwa mkarimu tena mwako, kwakushukuru pale mtu anapokua amejituma/jitahidi kufanya kitu kwaajili yako kunafanya huyo mtu aongeze juhudi. Kinyume cha hapo ndio unakuta mtu anafanya na kulipua kitu kwasababu analazimika na ingekua uamuzi wake asingefanya kabisa.
Mimi nimewahi kukutana na watu ambao hata kusema asante kwa chakula hawajui au sijui niseme hawawezi.Mimi niliwashangaa kwa kutokushukuru na wao walinishangaa kwa kuuliza mbona hawashukuru, ila baada ya kuwaeleza kwanini nadhani ni muhimu kufanya hivyo wakanielewa na kuanza kulitumia neno "ASANTE" ipasavyo.
Je wewe kama wewe mara mwisho umemwambia dada wa kazi, mzazi wako, mwenzi wako asante baada ya kula ni lini?
Mara ya mwisho kumwambia mtu asante baada ya kutekeleza kitu chochote kile ulichomwomba/mwagiza afanye ni lini?
Mara ya mwisho umemshukuru hata mpishi/mhudumu wa hoteli au mgahawa ni lini?
Mara ya mwisho kumshukuru mwenzi wako kwa kuwa na wewe bega kwa bega ni lini?
Mara ya mwisho kumshukuru dada wa kazi kwa kukulelea mwana/wanao ilikua lini?
Mara ya mwisho kumshukuru mtu yeyote yule kwa sababu yoyote ile ni lini?
Kama hukumbuki au ilikua muda mrefu sana badilika.Hata mtu unaemlipa anastahili asante kwasababu angeweza kufanya anachofanya kwa kulipua pamoja na kwamba unamlipa.Jifunze kushukuru uwape watu morale ya kuendelea kukusaidia na kukutumikia kikamilifu, pia raha ya kuwa karibu nawe.
Jumatatu njema.