Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema Serikali kutoa huduma ya Elimu na Afya bure inawezekana ikiwa tu mianya ya rushwa na ufisadi itadhibitiwa ipasavyo na wananchi wataweza kunufaika na rasilimali zilizopo nchini....
Yalisemwa na Chadema mwaka 2010 lakini wakabana, sasa joto la M4C linaanza kuwachoma...taratibu watajivua nguo moja baada ya mwingine. Kama vipofu walidai haiwezekani, M4C imewaondolea wingu lililowaziba macho...
Aliongeza, Hatuwezi kuwa na nchi ina kila kitu, tunayo makaa ya mawe, maziwa, mito, bahari, madini, gesi, mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro na tuna hekta za kilimo zaidi ya milioni 88, tunataka Watanzania muamke na muache kushabikia rushwa ndogo ndogo tuingie katika utamaduni unaotuwezesha kujenga heshima ya nchi yetu kwa kujali uongozi ulionyooka na wenye uhadilifu.
Lahaula! masikini Sitta, alikuwa anakataa nini na sasa anakubali nini!...once he was blind but now he can see, thanx to makamanda! Mwanga wa Chadema utawatoa mkukumkuku pangoni. Kwa habari zaidi bonyeza hapa;