Matumizi ya asali, tango na limao

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,499
11,231
Waungwana naombeni ufafanuzi wenu juu ya tetesi/hoja kuwa kuchanganya asali pamoja na limao kwa wakati mmoja inaweza kupelekea kifo kwa mtumiaji kwa kigezo kuwa Mchanganyiko huo hugeuka kuwa sumu, Hii habari niliisikia zamani nikiwa Bwana Mdogo na mpaka leo nimekuwa, sijaweza kuhakikisha hilo kwa kuhofia kufa kama ni kweli.

Wanajamii nitashukuru iwapo nitapatiwa ufafanuzi wa kitaalamu juu ya ukweli wa hoja hiyo, na kama siyo kweli, basi ni faida gani zinapatikana kwa kuchanganya asali na limao?
 
Pole ndugu kwa imani hiyo potofu. Kama nimelielewa vyema swali lako nalijibu hivi.

Asali iwapo imevunwa na kutunzwa vizuri ni chakula kitiacho nguvu mwilini. Limao ni mojawapo ya matunda yalosheheni vitamini. Vyote ni salama mwilini vikitumika vingali bado salama.

Aidha asali safi ikichanganywa na limao na haswa ukiongeza tangawizi ni dawa ya kikohozi. Kama kuna ambaye kuchanganya asali na limao vilimgeukia sumu basi zitakuwepo nyingine zikiwemo usafi na afya yake kabla. Mfano, mwenye vidonda tumoni limao litamuathiri kila atumiapo.
 
Pole ndugu kwa imani hiyo potofu. Kama nimelielewa vyema swali lako nalijibu hivi.
Asali iwapo imevunwa na kutunzwa vizuri ni chakula kitiacho nguvu mwilini. Limao ni mojawapo ya matunda yalosheheni vitamini. Vyote ni salama mwilini vikitumika vingali bado salama. Aidha asali safi ikichanganywa na limao na haswa ukiongeza tangawizi ni dawa ya kikohozi. Kama kuna ambaye kuchanganya asali na limao vilimgeukia sumu basi zitakuwepo nyingine zikiwemo usafi na afya yake kabla. Mfano, mwenye vidonda tumoni limao litamuathiri kila atumiapo.

Nashukuru kwa kunifumbua macho mkuu. Manake utotoni ilikuwa mtu ukishakula asali basi lazima ukae mbali sana na malimao au ndimu kiasi kuwa hata kachumbari kama imewekwa limao basi kwa siku hiyo unaikosa eti kwa kuhofia kufa.

Naona hizi dhana za vitisho juu ya mambo fulani mbali mbali zimetujaa sana watanzania ingawa mara nyingine hutumika ili kujenga jamii adilifu lakini matokeo yake hujenga jamii ya watu waoga. Ni vyema tukajenga utaratibu wa kueleza watoto wetu ukweli halisi bila kupindisha maneno.
 
Hakuna shida yoyote ile sema labda ukila kwa kiwango flani ila kama alivyosema ndugu ni kwamba huo mchanganyiko pia hutibu kikohozi pamoja na tangawizi. Nakumbukumbu wakati wa udogo vitu vingi tu tulikatazwa na kujengewa imani kuwa watoto wanavuliwa kwenye maji kama vile samaki.Fanya majaribio jibu utapata!
 
Naomba msaada Great thinkers, je ni kweli kuwa ukichanganya asali na ndimu/limao inakuwa sumu kwa binadamu?je kuna ukweli wowote wa kisayansi(chemistry)?
 
naomba msaada Great thinkers,je ni kweli kuwa ukichanganya asali na ndimu/limao inakuwa sumu kwa binadamu?je kuna ukweli wowote wa kisayansi(chemistry)?

Siyo kweli kabisa, mie binafsi nimekuwa nikitumia asali na limao/ndimu kwenye chai/maji ya moto kwa zaidi ya miaka sita sasa na sijawai kuwa na tatizo lolote.
 
Ni dawa nzuri ya kifua na kupendezesha ngozi sasa sijui inageuka sumu saa ngapi!
 
Hii imani imekuwepo sana.Sijui ilitokea wapi
Imani imetokea kwa watu wanaosema kuwa mzinga wa nyuki ukiulembea ndimu, nyuki wanakuwa na ghadhabu sana. Hivi kweli umlembee hata kijiwe kidogo tu watakuwachia?. Wanaosema hivi wanadai pia unapochanganya asali na ndimu "reaction yake" inatoa mapovu mengi kwa hiyo ukitia tumboni tumbo litavimba. UONGO. Ukweli ni kuwa asali na ndimu/limau, mbali ya kuwa ni tamu sana, vilevile ni dawa nzuri ya kukohozi, pumu na maradhi yanayohusiana na pumzi.
 
Thanks,walioniambia walizungumzia hasa hilo suala la reaction,na wakasema kuwa hiyo reaction inavuruga na kukatakata utumbo na kusababisha sudden death!
 
siyo kweli kabisa, mie binafsi nimekuwa nikitumia asali na limao/ndimu kwenye chai/maji ya moto kwa zaidi ya miaka sita sasa na sijawai kuwa na tatizo lolote.

Labda kwa kuwa unatumia chaini na majini,wanasema ukichanganya moja kwa moja,inaleta reaction ambayo inavuruga na kukata kata utumbo na kusababisha kifo cha ghafla
 
Labda kwa kuwa unatumia chaini na majini,wanasema ukichanganya moja kwa moja,inaleta reaction ambayo inavuruga na kukata kata utumbo na kusababisha kifo cha ghafla

Wazungu wanatumia sana asali na ndimu, jaribu kugoogle uone kama kuna kesi yoyote iliyoripotiwa
 
Waisraeli walikula vyakula vifuatavyo.
1.Asali
2.Nyama ya kuokwa
3.Mikate isiyotiwa chachu
4.Maziwa,Matunda yasiyopikwa,Mvinyo na Maji kutoka kwenye miamba
Hivi vikiwa vyakula vyetu Magonjwa yatokanavyo na vyakula (kula ovyo ovyo) yataondoka hapa duniani.
 
Tausi,
Nadhani ni kukosa uelewa zaidi.Ukiangalia dawa za nyumbani ( home remedies) kwa ajili ya kukohoa na magonjwa ya koo wanashauri uchanganye asali na ndimu na hakuna popote utasikia inaleta au imewahi kuleta madhara.

Duuh,jamani duniani kuna mambo,maana aliyeniambia kuwa ukichanganya hivyo vi2 vi2 inakuwa sumu,kwa kweli alisema kwa comfidence ya ajabu na msisitizo sana hata nikaogopa sana,anyway i'll try to mix an see
 
Nimewahi kusikia pia...lakini aliyesema akasisitiza kuwa inategemea ni asali ya nyuki wa aina gani (wadogo au wakubwa). Nimesahau ni ya nyuki wepi hasa ndio inasadikika kuwa sumu kwa binaadamu endapo itachanganywa na asali.

Mimi huwa nipo interested sana na hizi imani za zamani na kujaribu kuangalia busara/funzo/mantiki yake. Ukizifuatilia, nyingi ya imani hizi zina scientfic basis (au tuseme zinaelezeka kisanyansi) hata kama kwa nyakati hizi relevance yake imepungua au haipo kabisa kutokana na maendeleo.
 
Ni kweli mkuu,imani nyingi zina scientiffic base,mfano wanawake wajawazito kutokula mayai nk!
 
Hivi hamna anayejua contents/ingredients za asali na limao tuone vikichanganya vitatoa product gani na kwa kiasi gani.
 
Asali na limau ni dawa zuri sana na pia husaidia umeng'enya chakula tumboni kwa hiyo dhana ya sumu haipo kaisa ni imani sizizo naukweli wowote
 
Back
Top Bottom