Asaalam aleikum wakuu,

Kyatsvapi

JF-Expert Member
May 15, 2009
317
196
Natafuta cable ambayo naweza kutumia kuunganisha PC (Laptop) na LCD. Laptop yangu ina support VGA (Female) na nataka kutumia HDMI port katika LCD.

Nisaidieni kwa kuipata hapa bongo Daslam....

Natanguliza shukrani za dhati.
 
Jaribu kuulizia kwenye maduka ya vifaa vya kompyuta kama KVD na mengineyo. Unaweza usipate cable halisi lakini nina hakika ukiuliza CONVERTER inayoweza kuunganisha ports ambazo hazishabiliani utafanikiwa
 
Natafuta cable ambayo naweza kutumia kuunganisha PC (Laptop) na LCD. Laptop yangu ina support VGA (Female) na nataka kutumia HDMI port katika LCD.

Nisaidieni kwa kuipata hapa bongo Daslam....

Natanguliza shukrani za dhati.

yaani hata kwa mtu wa kawaida tu akinisalimia kwa salam hiyo huwa ananikinai palepale na huwa simsemeshi tena. kuna kipindi yule dogo mnyakyusa wa tbc 1 anayetangaza michezo, yule mapepe aliyeoa juzijuzi tu, alikuwa anaanza kwa salam alekum ivyoivyo, na watangazaji wengine, WANAFIKIRI WATU WOTE WANAOWASIKILIZA NI WA SALAM ALEKUMU yao...inakera kupindukia, hasa unapoona limbukeni anayefanya kazi kwenye chombo cha uma (watu wa dini zote) anaposalima kwa dini moja...huwa nabadilisha channel harakaharaka!
 
Loh kazi kweli kweli,Asalaam aleykum haina udini, labda mkuu unahitaji kujua maana yake ni sawa na mtu akakuamkia Shikamoo, Shikamoo sio kiswahili fasihi, ni maneno ya lugha moja ya kienyeji lakini inakubalika sawa na mtu akikusalimia "Good morning" au "Good day" utamkasirikia au utasikia kichefuchefu?. Maana kamili ya Asalaam alaykum ni hii kwa kiingereza "PEACE BE UPON YOU" Jee mtu akikutakia heri/amani kuna ubaya gani?
** Unanikumbusha mdada aliealikwa dinner akasema yeye hapendi, lakini alikubali just kusindikiza watu, ilipofika wakati wa kutoa oda akauliza mbona yeye hawajamuodeshea? alipoambiwa si ulisema hutaki dinner? akajibu ndio mimi sikujua kama dinner ndio hii.

u said it all, well said!
 
mbona sijawahi kusikia hata siku moja hao watangazaji wakiamkia "shalom! shalom!", unataka sisi wengine tusio waislam tuamkiwe kwa kiislam? mimi pia huwa sipendi hata kusikia na huwa sijibu.
 
Sorry Ubungo ubungo,

Naona nimebadilisha mada kabsaaaaa! Nipeni mawazo basi wapi naweza pata zaidi ya KVD cos hao jamaa hawana hiyo kitu.

Tks
 
Mm nimestuka, huyo anayechukia salam ya kiarabu...! mimi si muislamu lakn, ila ninasisitiza ANACHUKI binafsi, hajui hata neno salaam ni la kiarabu (si kiislam tafadhali). Nashindawa kuelewa aliwezaje kufungua topic hii kama anachukia neno hilo kihivyo!!...sory off topic.
 
hiyo maana yake amani ya mungu iwe juu yako, na si vinginevyo sasa uwezo wako mdogo wa kuelewa na chuki uliyozaliwanayo kwa mama yako inakusumbua,

Kaka nenda KVD muulizie jamaa anaitwa Teacher, amehamia mitaa ya mnazi mmoja atakusaidia
 
Kwa kweli hizi chuki tuzipunguze, chuku inakwenda mpaka inafika mahali hata salamu ya mungu inakuwa huitaki, pole
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom