As far as opportunity cost is concerned, CHADEMA kateni rufaa

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,848
2,669
Opportunity cost ni the next best alternatiive. Cdm wana mawili; kutaka rufaa ama kukubali matokeo na kurudia uchaguzi. Kwa mtazamo wangu, kurudia uchaguzi ni gharama sana kwa upande wa muda na fedha, pengine hata maisha pia. Cdm mfanye tathmini ni gharama kiasi gani zilitumika Igunga, Arumeru, na sasa Arusha mjini. Kadhalika watazame na gharama za kurudia kesi.

Awali, kesi ya Lema haikupewa sana maana na wananchi kote Tanzania. Hukumu ya kesi imefungua masikio ya watanzania kote nchini na nje ya nchi. Kwa maana hii hata serikali imeshaona mwitikio wa watanzania katika kesi hii.

Kwa mujibu wa mawakili waliokuwa wakiendesha kesi hii upande wa Lema, wanasema kuwa kesi ilikuwa na dosari nyingi (sina sababu ya kuzirudia hapa). Sasa kwa mwendo huu ni wazi kuwa marudio ya kesi yatavuta hisia za watanzania kwa kiasi kikubwa zaidi na kupelekea serikali na mahakama kufikiria mara ya pili. Kwa hiyo wito wangu, kateni rufaa na mwisho wa siku jimbo litarudi cdm
 
Thanks for your post kamanda!Mimi pia kama kijana wa Kitanzania mpenda haki na demokrasia ya kweli my best alternative kwa CDM ni kukata rufaa ili kuwathibitishia Watanzania kuwa Jaji Rwakibarila hakutenda haki katika uamuzi wake!Maamuzi yake hayana Ushahidi kamili kuwa Lema alimkashifu Mama yetu Dk Burian.Vigezo alivyotumia Jaji sijui amebase kwenye evidence ipi!!!!Kesi yote ni vituko vitupu naifananisha na Hekaya za Abunuwasi au Tamthiliya ya Kusadikika.CDM kutokata rufaa eti kwa kigezo Uchaguzi ukirudiwa Watashinda sikubaliani na uamuzi huo!Kukubali Uamuzi wa Kesi maana yake ni kuwaambia Watanzania kuwa Lema hajaonewa ila ni kweli Alikiuka Sheria za Uchaguzi kama Jaji alivyodai!Pia siungi mkono Maoni ya Lema kuwa hapendi kuwa Mbunge wa Mahakama!Hili neno Mbunge wa Mahakama ni propaganda tu zilizoanzishwa na baadhi ya Watu hasa baada ya Hamad R na David K kuvuliwa uanachama na vyama vyao na kufungua kesi mahakamani!Ukweli utabaki palepale kuwa Lema alichaguliwa na WanaArusha lakini Mahakama na Serikali ya Magamba inafanya hili kumoundoa kwa Fitina!Naunga mkono CDM kukata Rufaa
 
na je vip kuhusu nafasi ya ubumge wa lema,wakati rufaa ya ikiwa insikilizwa? Je atendelea kuwa mbunge?
 
kwa upande wa Lema, ninavyoelewa ni kuwa jimbo lipo wazi hadi aidha uchaguzi utakaporudiwa na ashinde tena ama ashinde rufaa. Ndio maana ukichunguza maandishi na kauli nyingi utaona neno 'mheshimiwa' halipo tena bali utauna 'bwana' ama 'ndugu'. Cha msingi kina ndugu Lema wajipange na rufaa tu na tutashinda kwa kuwa kama alivyosema dogo janja, sisi (cdm) tuna Mungu na wao wana vyungu (majungu).
 
Yaani maamuzi haya, nadhani Mheshimiwa Jaji alipitiwa, haiwezekani atukanwe mwingine, kisha machungu asikie mtu baki! hii ni sawa nakuoga wewe na akatakata mwingine! Rufaa ni muhimu sana, maana huyo jaji amejichanganya ama amechanganywa! japo Arusha bado ni ya kwetu, hata uchaguzi ukirudiwa bora CCM wakapima maji na kutokushiriki, bora lawama kuliko fedhea watakayo ipata!
 
ni kweli kabisa. Ni hukumu ya kipumbavu kuwahi kutokea hapa nchini. Nachoona ni kuwa ccm hawataki tena futi sita bali kina kirefu cha NUNGWI
 
cdm wamefanya jambo la busara kuamua kukata rufaa. Hii itaharakisha na kurahisisha mchakato wa kulirudisha jimbo mikononi mwetu. Viva cdm
 
Nawashukuru kwa mawazo mazuri na mimi sasa ni elelewa umuhimu wa kukata rufaa ,Tuendelee kuwaombea makamanda wetu
 
Back
Top Bottom