- Thread starter
- #21
Ingekuwa vizuri hawa viongozi wakuu wa taifa Kichama wanapoongea tusiishie tu kusifia umati wa watu waliojitokeza. Hebu tujuze Mbowe kazungumza nini juu ya uchumi wa nchi yetu,mikakati ya kujikwamua kiuchumi,..na sera nyingine kama kilimo,elimu,ajira na kadhalika. Haya ndio mambo muhimu tunayohitaji kupima uzito wa hotuba za hawa viongozi na sera za vyama siasa. Ni kwa njia hii ndio tutaweza kupima kati ya viongozi shupavu,wenye mipango,wenye sera makini,wakweli..vinginevyo tutaingiza madarakani vilaza,waongo,walafi,wapenda sifa na wabinafsi.
Mleta uzi,Mbowe kwa nafasi yake amesema nini juu ya hayo?
Nenda pale Lumumba watakupa hotuba yake.