Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,895
- 31,106
eep: Wakuu baada ya kufanya tathimini nzito na yakina si kama zile Synovate na REDET nimebaini bila shaka yoyote wala ushabiki nafasi ya ubunge Arusha bado iko wazi kwa wagombea watatu Bwana G Lema CHADEMA,Bwana M Lyimo wa TLP na Mama Batilda Buriani wa CCM wote wana nafasi kubwa kuibuka na ushindi jimbo la Arusha mjini.
{1} Mama Batilda Buriani kwa wiki mbili sasa amekuwa akifanya kampeni za nguvu kubwa sana,ameweza kuwafikia wapiga kura wengi kwa mtindo wa nyumba kwa nyumba.CCM kiasi fulani wameweza kuwarejesha kundini baadhi ya wanachama wake ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakimsumbua Batilda.Batilda anategemea kupata kura nyingi kata ya Kati,kata za pembezoni zamani zilikuwa kata za wilaya ya Arumeru.Wapiga kura wazee ,wasiopenda fujo na wanaCCM wanategemewa kumpa kura Dr Batilda Buriani.Idadi ya wapiga siku ya uchaguzi ikiwa ndogo Dr Batilda atashinda kwakuwa atapata kura za wazee ambao si wengi kama wapiga kura vijana wenye mwamko mkubwa wa mageuzi.
{2] Bwana Macmillan Lyimo amejitahidi sana kuwafikia wapiga kura wengi hasa kata za Ungalimited,Sokoni 1,Sinoni,Lemara,Sombetini,Elerai,Matevesi na Terati [chuo cha VETA].Wananchi wengi hata wanachama wa vyama vya CCM na CHADEMA wanakubali bila ubishi Lyimo ni kichwa hana ubisho wala hatukani mtu kwenye mikutano yake.Bwana Lyimo anategemea kupata kura nyingi kwa watu wenye kupima uwezo wa mgombea kujenga hoja na kuitetea.Kampeni zake za nyumba kwa nyumba kwenye kata nilizozitaja zinaweza kumsaidia kupata kura nyingi.Wakongwe wa siasa za upinzani Arusha Mzee Kivuyo [diwani kata ya Sokoni 1 tangu 1995]na Meagie wamemsaidia Lyimo kuvuka viunzi vingi.TLP na CHADEMA wanaweza kugawana kura nyingi na kutoa mwanya mgombea wa CCM kushinda kwa ulaini.
{3} Bwana Godbless Lema amejitahidi sana kuwafikia wapiga kura wengi hasa kata za Kimandolu,Themi,Kaloleni,Levolosi,Ngarenaro.Lema anategemea kupata kura nyingi kutoka kwa vijana na watu wazima wanaotaka mabadiliko kwa namna yoyote[wapo watu wako tayari kupigia kura jiwe kuliko CCM].Hawajui kama yuko mpinzani mwingine wa kumpa kura zaidi ya Lema.Lema angekuwa na nusu ya uwezo wa Lyimo hakika Mama Batilda angefungasha virago siku nyingi.Mikutano mingi ya Lema imejaa balah blah na pumba nyingi kiasi nashindwa kuamini wapo watu wenye akili nzuri watakao mpigia kura.Elimu ya Bwana Lema imeendelea kumwangusha sana hasa siasa za majukwaani ameshindwa kujenga hoja za msingi badala yake amejikita zaidi kumshambulia Dr Batilda maisha yake binafsi na Lyimo ametumwa kumvurugia ? ?.Vipo vipeperushu ambavyo Lema amevitoa kwaajili ya kumsaidia kwenye kampeni zake taarifa za ndani [kanzi] zinachakachuliwa kuelezea ukihiyo wa Lema vinatarajiwa kutawanywa leo muda wowote kuanzia sasa.Wapiga kura wengi wakijitokeza Lema atashinda.TLP na CHADEMA wangekaa meza moja kazi ya kuiondoa CCM ingekuwa rahisi sana.
Kamanda PakaJimmy huo ndio utafiti wangu usishangae sana Mama akiibuka ushindi hatujawatendea haki waTanzania wapinzani lazima wajue watabeba zigo la lawama Arusha ikiangukia tena CCM.