Arusha sasa ni Salama - Kikwete

Ni hatari sana kwa kiongozi mkuu wa nchi kwa majungu amani ipi iloyo potea arusha na ameirudisha nani mbona anakuja na kuondoka kama mwizi hapa . Mi naona yeye mwenyewe na ccm yake ndio hawana amani apa arusha.

Kakulia uswahilini we huoni hata akiwa anazungumza jukwaani huwa anaweka vidole viwili juu sababu ameshazoea mipasho!!!!!
 
hakika ujinga wa lema uliondoa amani ya arusha! sasa arusha pako swari na kila mtu anafanya kazi zake kwa amani!

pole sana kwa kuwa mtumwa wa ccm, kama wewe ni mkazi wa arusha ndio utajua kuwa lema ni kiongozi wa aina gani, mlishakula hela za barabara lema kawashikia chini mda huu barabara zinatengenezwa, machinga walikuwa wananyanyaswa lema kuja wanafanya biashara zao,unafurahi wamama wanavyochukuliwa mboga zao na manispaa yenu ya ccm? Mgambo walikuwa wanafunga watu mashati je baada ya lema kuchaguliwa umeshaona hio kitu?kiwanja cha pale kilombero nyie ccm mmeuza kinyemela na mkataka kujenga kama lema asingekuwa mzalendo asingezuia ujenzi,kama wewe si mkazi wa hapa kaa kimya,
hayo ni machache tu
 
Nadhani katika wapumbavu Tanzania hii na wewe umo, huwezi ukatukana tusi baya kiasi hicho Rais wa nchi.
Nyie CHADEMA mtabaki hivyo hivyo mpaka mwisho maana Ubaya hautoruhusiwa kukanyaga patakatifu- Matusi yako ipo siku yatalipizwa, Take care.

hivi arusha kuna chadema na ccm tu? Mbona unamwambia jamaa yeye ni chadema unauhakika? Au chadema imekubana kwenye dili zako za njia ya panya?nijuze
 
Nina wasiwasi na IQ ya baadhi ya viongozi wetu! Ilikuwa ni laazima atanabaishe kuwa kahusika kwenye kesi ya Lema? Mimi naona huyu bwana kakosa washauri, au kama wako ni vilaza au kama siyo vilaza yeye ni haambiliki! Sasa ameudhihilishia umma kuwa ni kweli walihusika na khukumu ya kesi ya Lema kwa lengo la kutuliza amani ya Arusha, sasa ni kweli Arusha kulikosa amani? Au mashushushu wanampelekea majungu ya uongo? Manaake mimi siyo mkaazi wa Arusha (Japo ni mzaliwa) lakini mala nyingi niko Arusha, alilioliongea halipo huko!

Arusha haijawahi kukosa amani kwa jinsi anavyo ongea, ni mambo tuu iku ile ya mauaji arusha, kweli Africa kuna viongozi! Wanasikitisha lakini!
 
Rais Jakaya Kikwete amewapongeza wakazi wote wa Arusha kwa kurudisha amani iliyokuwa imepotea.Rais amesema kamwe serikali yake isingeruhusu mkutano wa kimataifa kufanyika Arusha katika hali ya sintofahamu iliyokuwepo kabla.Rais ameyasema hayo katika hotuba yake iliyosambazwa kwa vyombo vya habari muda mchache uliopita.
Rais amesema mkutano wa kimataifa uliofanyika Arusha ni kutokana na juhudi za wakazi wa Arusha kurejesha amani iliyokuwa imepotea.Amewasihi wakazi wote wa Arusha kuendeleza amani iliyopo ili jiji hilo liendelee kutambulika kama Geneva ya Afrika.Rais amemalizia kwa kusema Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.

Kwa tafsiri ya alichokisema hasa anagusia uongozi(ubunge) wa Lema na ktk hili nnayaunganisha maneno ya mkuu Wa mkoa wa Arusha(alieteuliwa na Raisi Jakaya Kikwete)nae aliipongeza mahakama kwa uamuzi iliyoutoa kwa kumvua Lema mbunge Wa Arusha mjini kupitia Chadema kuwa hali sasa itakuwa shwari.

Huyu mkuu Wa mkoa ambae anatakiwa kufanya shughuli za kiserikali hakufafanua ni jinsi gani Lema Kama mbunge alikuwa akipoteza amani ktk jiji la Arusha.Hoja yake (mufilisi)huyu mkuu wa mkoa hakupaswa kuitoa,japo kumbukumbu inanikumbusha hawa wakuu wa mikoa/wilaya huwa ni makada wa ccm na wanafanya kazi za ccm kwa maagizo ya mkubwa wao raisi wa sasa Jakaya.Tujiulize haya matamko Yao yanayofanana ni ajenda gani imejificha nyuma ya matamko yao?

Dunia hii ukisimama ktk haki utanyanyaswa kwa kila hila na wakubwa Wa nchi hii.Wengi Wa wakazi Wa Arusha hatuitaki ccm imetutesa vya kutosha.Ushuru Wa magari tunalipa mara tatu kwa kampuni mbili tofauti ndani ya manispaa moja je hii ni haki?Lema amelikemea hili na manispaa walikiri kukosea na wakaahidi mwisho Wa mikataba ya kampuni hizo hawatalirudia kosa hilo.Hilo ni dogo lakin ni wizi unaofanywa mchana kweupe sasa je vipi kuhusu wizi tusiojua ndani ya manispaa yetu?Lema akikemea anaambiwa mgomvi,taratibu za kumpata meya Wa jiji la Arusha ulikiukwa Lema akilipinga anaambiwa mgomvi

Kiwanja kilichopo Kilombero(iliyokuwa stand ya mabasi makubwa zamani)kimeuzwa kinyemela Lema akilikemea na kuuanika wizi huu Wa Mali za Watanzania mbele ya Watanzania anaambiwa mgomvi.Yapo mengi sana lakini nnaomba nimwambie Jakaya na Serikali yake kuwa sio Kama tumetulia wakazi Wa Arusha,tuna asira mioyoni mwetu sababu ya mambo maovu mnayoyafanya dhidi yetu na dhidi ya viongozi wetu mlituua kwa mitutu ya bunduki January 5 hatujasahau na polisi waliofanya kitendo kile ninyi viongozi mliwatetea na hawajawajibishwa mpaka leo,mmetunyang'anya mbunge wetu kwa hila zenu hatujasahau na hakika ipo siku mambo yote haya mnayoyafanya yatakuja na majibu yake na hapo ndipo mtakumbuka Kama mlipanda upendo au mlipanda chuki ndani ya miyoyo yetu wananchi.

2015 hata jiwe litapigiwa kura lituongoze kuliko ccm.
 
Nnaomba nimwambie Jakaya na Serikali yake kuwa sio Kama tumetulia wakazi Wa Arusha,tuna asira mioyoni mwetu sababu ya mambo maovu mnayoyafanya dhidi yetu na dhidi ya viongozi wetu mlituua kwa mitutu ya bunduki January 5 hatujasahau na polisi waliofanya kitendo kile ninyi viongozi mliwatetea na hawajawajibishwa mpaka leo,mmetunyang'anya mbunge wetu kwa hila zenu hatujasahau na hakika ipo siku mambo yote haya mnayoyafanya yatakuja na majibu yake na hapo ndipo mtakumbuka Kama mlipanda upendo au mlipanda chuki ndani ya miyoyo yetu wananchi.

2015 hata jiwe litapigiwa kura lituongoze kuliko ccm.

KAKA CHUKUA 5
 
arusha amani ya kutosha tu!
Njoo mchana uje kuhutubia wananchi pale stadium basi@jk
 
Mkuu nadhani anakumbushia polisi walivyovamia maandamano ya amani ya CDM na kufanikiwa kuua wanachama watatu.Pia vurugu walizokuwa wanamfanyia mbunge aliyeporwa ubunge Godbless Lema

usiwe kama pinda aliyedanganya bunge waliouwawa ni wanachama wawili wa CDM na raia mmoja wa Kenya! mungu awapumzishe kwa amani maana walikufa wakipigania haki!!
 
hivi arusha ilikua haina amani?

Hilo ni swali la msingi sana la kujiuliza ambalo jibu lake lipo.Arusha amani ipo ila haki ndio tumenyang'anywa,tumpuuze raisi Jakaya ni muongo na amesema uongo na ni kawaida ya viongozi hasa wa ccm na Serikali yake Kama ilivyokuwa kwa Pinda bungeni dhidi ya Lema na sakata la mauaji ya Arusha
 
Hilo ni swali la msingi sana la kujiuliza ambalo jibu lake lipo.Arusha amani ipo ila haki ndio tumenyang'anywa,tumpuuze raisi Jakaya ni muongo na amesema uongo na ni kawaida ya viongozi hasa wa ccm na Serikali yake Kama ilivyokuwa kwa Pinda bungeni dhidi ya Lema na sakata la mauaji ya Arusha

Binafsi nadhani amepoteza sifa ya kuitwa Raisi
 
Akiwa kama amiri jeshi mkuu ni lini alitutangazia kama Arusha si salama? Huyu jamaa ana matatizo ya kufiri au hukurupuka tuu na kuropoka?
 
Huyu Rais amekosa la kusema ndio maana wakati akihutubia alionekana hajiamini. Akashindwa kusema anavyotaka kuuza ardhi sh 200 kwa ekari, akadai wawekezaji wanakuja hawatapora ardhi wanalima na kuiacha, muda hataji miaka watakayomilikishwa. Sasa la utulivu Arusha kachemsha, amesahau alivyoshiriki kuandika hukumu feki na kumpa Jaji wake asome. Wasije wakaamua uchaguzi wa jimbo kutokuwepo kwa kukwamisha rufaa ya CHADEMA. Yeye anajua alivyochakachua kuwepo ikulu, kama anabisha aitishe uchaguzi sasa hivi aone.
 
Maneno haya ya Mh. Rais nimaneno ambayo yamelenga kuvunja mioyo ya wengi na kuwafurahisha wachache, wenye kufaidika na mfumo huwo wa dhuluma. Najua Rafiki yangu Godbless Lema amesikia kauli hiyo, huenda akaijibu mapema sana leo ama kesho ama sasa ama akaipuuza kauli hizo za kejeli.

Mimi kama mimi HENRY J KILEWO Mwananchi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Naifananisha kauli hii kama kauli ya mtu 'aliyeshindwa kuwatumikia Wananchi wake na kuanza kutafuta mchawi wake' Wananchi wa ARUSHA wanampenda mbunge wao na huenda wakampata mapema sana leo ama kesho ama saa watakayoamua, Cheo hakiwezi kupora haki ya mtu ama utu bali huchelewesha tu. Tazama viganja vyako vya mikono. Je, Vinamistari ? Na kama ipo, je! kuna mtu anayeweza kuifuta? Kama hakuna, Basi hakuna mtu anayeweza kuzuia, haki,utu na usawa wa mwanadamu.

Tuendeleeni kumuomba mungu tutayaona mengi zaidi ya haya naamini mungu anakusudio lake na atatenda Makubwa mapema leo ama kesho... Watashindana na sisi lakini hawatashinda. WATATUUA KWA RISASI ZA MOTO, WATAKUFA KWA PRESHA YA DHAMBI, MSIOGOPE MUNGU YUPO UPANDE WETU.
 
napata shida sana nikiwa kwenye mikutano yangu ya kikazi nje ya tanzania kujitambulisha kuwa mimi ni mtanzanai na kikwete ni rais wangu...sababu yake ni rahisi kweli....nina rais mwenye very mediocre thinking...very low thinking ability....i mean very low...sijui nisemeje..lakini mungu yupo ...nakukumbuka sana Dr.Salim
 
Another idiot Zengo, JK haijui Arusha wala hatakaa aijue yeye abakie na starehe zake kwenda ulaya.

Ukitaka kujua kwamba haelewi hata kilichokuwa kinaendelea Arusha kwenye huo mkutano, alikuja alhamisi this week kufungua mkutano ulioanza jumatatu na kuisha jumamosi, kwahiyo haelewi hata mkutano ulikuwa unahusu nini. Sasa anapokuja na kusema sasa Ar kuna amani anamaanisha amefanikiwa kumtoa Lema ili aje kulala mahotelini Arusha na vimada.

Sasa aelewe kwamba moto aliouanzisha ndiyo amezidi kuuchochea yeye na CCM yake ndiyo kwaheri.

Ar hakuna vurugu yoyote, watu wanafanya mkutano wao ulete vurugu for what reason? CDM wakifanya mkutano wao JK ndiyo anatuma vibaraka wake(polisi/usalama wa taifa) kuja kupiga watu, kwahiyo JK ndiyo mleta vurugu Arusha then anarudi kinafiki kudai Lema ndiyo anavunja hali ya Amani Ar.

JK acha UNAFIKI kwa watu Arusha na TZ kwa ujumla
 
Back
Top Bottom