Arusha: Operation zika CCM, jenga CHADEMA

Kampeni hiyo isiishie Arusha tu ifike mpaka Songea Lindi na mtwara
Yah hili ndilo suala la msingi maana kama chama kinaishia kuelimisha watu waliokwisha kuelimika kwa nguvu kubwa kiasi hicho itakuwa ni upotezaji wa muda na other resources.Arusha wameipokea chadema vzr, hapo inahitaji sensitization tu. Nguvu kubwa ielekezwe sehemu ambazo ujumbe wa CHADEMA haujafika kabisa ili kuelimisha watu na kuondoa dhana ya CHADEMA kuwa ni chama cha watu wa kaskazini.
 
Nimeamua kuanzisha thread inayohusu kampeni ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Arusha mjini inayo julikana kama "Oparesheni zika CCM jenga Chadema" ambayo mpaka sasa wameshafanya mikutano kwenye kata tatu kati ya kumi na tisa na siku ya leo watakuwa kata ya Daraja mbili. Pamoja na kukusanya kero mbalimbali zilizoko kwa wananchi pia Oparesheni hii nikujenga chama...Mikutano hii imekuwa na mahudhurio makubwa sana hii inaonyesha wananchi wa Arusha wanaimani kubwa sana na CHADEMA.

Tuendelee kujuzana kitakachokuwa kinatokea kwenye mzunguko wa kata zote 19.

View attachment 45110View attachment 45111View attachment 45112
Picha wakazi wa kata ya Kimandolu wakifatilia mkutano chadema

View attachment 45102View attachment 45103View attachment 45104View attachment 45105
Picha za mkutano wa kata ya Kaloleni wakisikiliza kwa umakini kabisa kamanda Godbless Lema.

Kero kubwa ni barabara za lami katika manispaa hiyo. Kwani manispaa haina hata barabara moja ya Lami. zote zenye lami ni mali ya TanRoad.

Sasa chadema wanawasaidiaje wakaazi wa huko Levolosi, Kaloleni, Sakina, Majengo n.k ambako ni vumbi tupu!!!.

​kama wamefika mpaka kwenye kata basi wamefanya vyema lakini wanatakiwa operation hizi waanze kufika mpaka kwenye vijiji ndio hapo watu watasema CCM bye bye
 
Barubaru, hii ngoma kwenye red umeshaipiga mpaka imepasuka.

Arusha ina lami nyingi kuliko miji yote isipokuwa Dar tu. Haka ka-complication ulichojilazimishia ya kuwa ni za Tanroad ni wewe peke yako. Wana Arusha wanazienjoy tu hizo lami bila kujichanganya eti ni lami ya nani.

Kwa taarifa yako, hata Dar wananyang'aywa barabara zao na kupelekwa Tanroads baada ya kushindwa kuziweka lami.
 
Kwa kuwa wakazi wa Levolosi, kaloleni, Majengo ni walipa kodi, wenye jukum u la kujenga barabara ni serikali ya CCM kazi ya chadema ni kuwa amsha wananchi wadai haki zako kama kujengewa barabara, maji safi n.k
 
Mkuu mbona zipo sana tu wasiliana na Nanyaro Ephata zinapatika kwenye ofisi ya Chadema wilaya (Ngarenaro).

Vp kapello pia zinapatikana? last time nimenunua kwa Tendwa Dar tsh 3000 juzi kati namuuliza tena anasema hawana zimeisha. kama kwako zipo niambie nipitie, pia bendera vp ntapata?bei/utaratibu ukoje? tafadhali
 
MP Nanyaro Ephata......
 
​kama wamefika mpaka kwenye kata basi wamefanya vyema lakini wanatakiwa operation hizi waanze kufika mpaka kwenye vijiji ndio hapo watu watasema CCM bye bye
umesema vema mkuu...
 
Barubaru, hii ngoma kwenye red umeshaipiga mpaka imepasuka.

Arusha ina lami nyingi kuliko miji yote isipokuwa Dar tu. Haka ka-complication ulichojilazimishia ya kuwa ni za Tanroad ni wewe peke yako. Wana Arusha wanazienjoy tu hizo lami bila kujichanganya eti ni lami ya nani.

Kwa taarifa yako, hata Dar wananyang'aywa barabara zao na kupelekwa Tanroads baada ya kushindwa kuziweka lami.

Vile vile kutoka stand ya daladala kupitia afisi za Dar Expr mpaka hospitali ya Seriani mpaka kufika maghorofa ya NHC nako vipi kumeshawekwa lami mwezi huu.

Kumbuka wananchi hawataki stori bali wanataka maendeleo na sio malumbano.

Kazi kwako. You can't fool all the people all the time.

jamani operesheni kama hizi ziende pia vijijini, ili mabadiliko ya kweli yaweze kupatikana, people tired with this ruling party, hawajafahamu tu kuwa they can change and life goes on well, kuliko ilivyo sasa.
 
Vile vile kutoka stand ya daladala kupitia afisi za Dar Expr mpaka hospitali ya Seriani mpaka kufika maghorofa ya NHC nako vipi kumeshawekwa lami mwezi huu.Kumbuka wananchi hawataki stori bali wanataka maendeleo na sio malumbano.Kazi kwako. You can't fool all the people all the time.
Katikati ya mji kuna km 30 zitajengwa na pesa ilishatolewa na World bank na mchakato umeshaanza, Njiro mpaka Nelson Mandela University napo kuna pesa ilsha tolewa tangu 2006 cha ajabu mpka leo haija jengwa, barabara ya East Africa ina panuliwa hii pesa imetolewa na World Bank kwa ushirikiana na EAC…..hivyo yote haya yakifanyika itakuwa ahueni ingawa bado kero ya barabara Arusha ni kubwa sana yaani miundombinu hovyo na sasa tunasikia Kaloleni wantaka kujenga mji wa kisasa sijui msongamano itakuwaje ukiangalia ofisi zote za kiserikali na EAC ziko maeneo hay ohayo……………wangekuwa na lengo zuri wange enda hata burka wakaanzisha mji mpya kuliko Kaloleni
 
Hii sasa ndio mikakati ya kichama sio kulala na kujivuna mwisho tukajikuta nje ya ulingo.. well-done Crashwise
 
Back
Top Bottom