Arusha: MADIWANI WALIOTIMULIWA CDM KUGOMBEA KUPITIA NCCR

Taasisi gani isiyohitaji nidhamu chini ya jua?
Umeathiriwa sana na siasa za Tanzania zisizo na nidhamu nini mkuu?...
Nidhamu gani hii ya kutaka usikilizwe wewe tu? Hii nidhamu ya kizezeta ndio imewafikisha CCM hapo walipo. Na ninyi CHADEMA igeni tu kuzitumia sheria hizi kandamizi na mbovu. Hamtaziacha hata mkikabidhiwa madaraka ya kuongoza nchi hii. Ni sawasawa na kula nyama ya mtu.
 
Mnataka kuwanyang'anya na haki zao za KIKATIBA na KIRAIA za NCHI hii? Acheni wagombee wanakotaka. Binafsi naichukia sana ile sheria iliyowavua UDIWANI kwani naamini kwa siasa za nchi hii anachaguliwa MTU sio CHAMA.

Sheria si mbaya.Chama ndicho kilichowadhamini kugombea udiwani sasa kama chama kimewakataa basi hawawezi kuendelea na udiwani.Zaidi ya hapo tuombe sheria ya mgombea binafsi iwe passed/enacted.
 
Nipo Arusha hivi sasa kikazi lakini kwakuwa Jiji hili ni ngome ya makamanda wa CHADEMA sikusita kufanya kautafiti kangu kadogo na huu ndio UWELI.

Kwa mujibu wa Bwana Bayo ambaye alikuwa Diwani wa kata ya Elerai anasema mbali na kukata rufaa juu ya maamuzi ya mahakama yaliyotolewa hivi karibuni dhidi yao lakini madiwani wote waliotimuliwa na CHADEMA wanategemea kugombea tena kupitia chama cha NCCR-MAGEUZI. Na kwa mujibu wake huyo Bayo, mkakati madhubuti unaandaliwa kuhakikisha wanashinda uchaguzi huo.

Nimejiuliza maswali mengi, mojawapo ni hili, wataamuaje kugombea kwa tiketi ya NCCR wakati wanakata rufaa? Je rufaa yao ikikubaliwa na mahakama ikawapa haki ya kuendelea kuwa madiwani wa Chadema mpango wao wa kuhamia NCCR utayeyuka au washajua mbali na kukata rufaa lakini watachemsha tena?

Hapo ndipo utakapojua kuwa watanganyika tumefikishwa mahali hata hatujielewi kwa vitendo na hata maneno yetu. We are totally confused. Hawa ni watu wamekwenda shule lakini angalia wanavyojichanganya utafikiri hawajawahi kupita darasa lolote. Mwisho wa yote ni aibu kwao. Mijitu mizima hovyo
 
Sheria si mbaya.Chama ndicho kilichowadhamini kugombea udiwani sasa kama chama kimewakataa basi hawawezi kuendelea na udiwani.Zaidi ya hapo tuombe sheria ya mgombea binafsi iwe passed/enacted.
Chama hakikuwadhamini. Katiba yetu ya JMT ndio inayolazimisha kila mgombea ateuliwe na chama fulani. Kwa kuwa na CHADEMA nao wameonyesha kuishabikia sheria hii, ni vigumu sana kupata mgombea binafsi nchi hii.
 
Nidhamu gani hii ya kutaka usikilizwe wewe tu? Hii nidhamu ya kizezeta ndio imewafikisha CCM hapo walipo. Na ninyi CHADEMA igeni tu kuzitumia sheria hizi kandamizi na mbovu.
Sielewi ni nani anayetaka asikilizwe yeye tu!...unaongelea kikundi gani hicho?
Katiba ndiyo kauli ya mwisho ya chama au taasisi yoyote, na kwa kesi ya hawa jamaa ndiyo iliyowafukuzisha uanachama!
Kama unadhani katiba ni sauti ya mtu mmoja, then hiyo ni ishu mpya!
 
Mnataka kuwanyang'anya na haki zao za KIKATIBA na KIRAIA za NCHI hii? Acheni wagombee wanakotaka. Binafsi naichukia sana ile sheria iliyowavua UDIWANI kwani naamini kwa siasa za nchi hii anachaguliwa MTU sio CHAMA.

Wewe nawe unaongea pumba gani hizi?? Tangu lini nchi hii anachaguliwa mtu badala ya chama. Hata kama ukiwa na mvuto kama bosi wetu anavyovutia wakinamama kwa tabasamu lake bado lazima uwe na chama. Wagombee wenyewe bila chama kama inawezekana. Peleka pumba zako huko. Waambie na hao wenzako kwamba huko nccr kwenyewe kuna watu pia wanataka hizo nafasi.
 
Sielewi ni nani anayetaka asikilizwe yeye tu!...unaongelea kikundi gani hicho?
Katiba ndiyo kauli ya mwisho ya chama au taasisi yoyote, na kwa kesi ya hawa jamaa ndiyo iliyowafukuzisha uanachama!
Kama unadhani katiba ni sauti ya mtu mmoja, then hiyo ni ishu mpya!
Kifungu gani cha katiba ya CHADEMA walichovunja hadi kufikia kuwanyang'anya uanachama? Wakuu wa CHADEMA wametumia udhaifu uliomo ndani ya katiba yetu ya JMT kuwamaliza hawa jamaa.
 
Wewe nawe unaongea pumba gani hizi?? Tangu lini nchi hii anachaguliwa mtu badala ya chama. Hata kama ukiwa na mvuto kama bosi wetu anavyovutia wakinamama kwa tabasamu lake bado lazima uwe na chama. Wagombee wenyewe bila chama kama inawezekana. Peleka pumba zako huko. Waambie na hao wenzako kwamba huko nccr kwenyewe kuna watu pia wanataka hizo nafasi.
Wagombea ni watu au chama? Wanaotangazwa kushinda au kushindwa ni watu au chama? Katiba yetu mbovu ya JMT ndiyo imeleta kadhia hii.
 
Hata wafanye vipi, hawawezi kupewa kura tena na wtanznia. Hizo ni speed za mende ndani ya kabati, amabazo haziwezi kudondosha kabati!!
 
Chama hakikuwadhamini. Katiba yetu ya JMT ndio inayolazimisha kila mgombea ateuliwe na chama fulani. Kwa kuwa na CHADEMA nao wameonyesha kuishabikia sheria hii, ni vigumu sana kupata mgombea binafsi nchi hii.
Sasa unawalaumu CDM kwa kufuata sheria?Kwa nini hao wagombea wasiende mahakamani kupigania haki yao ya kugombea kama wagombea binafsi?Hawajui haki zao au wamekubali ku-play by the rules?Hata wenzetu Kenya wameliona hili na hivyo kuliweka katika katiba mpya,ukihama chama chako kilichokudhamini basi unapoteza kiti chako...mdhamini lazima aheshimiwe.
 
Halafu weye jamaa unaingia jiji la watu bila hata kugonga mlango aisee!...acha hizo chalii yangu!...Ngarenaro vp wazima?

Mkuu PJ nimekuja kikazi tu mkuu, huyu jamaa nimekutana nae eneo moja wanaliita MAJENGO YA CHINI.
 
Good move, I suppor them 100%
attachment.php
 
Kifungu gani cha katiba ya CHADEMA walichovunja hadi kufikia kuwanyang'anya uanachama? Wakuu wa CHADEMA wametumia udhaifu uliomo ndani ya katiba yetu ya JMT kuwamaliza hawa jamaa.

Unaijua vizuri katiba ya Chadema au umeamua tu kuosha kinywa?
 
Kifungu gani cha katiba ya CHADEMA walichovunja hadi kufikia kuwanyang'anya uanachama? Wakuu wa CHADEMA wametumia udhaifu uliomo ndani ya katiba yetu ya JMT kuwamaliza hawa jamaa.
Wakati mwingine huw sikuelewi kabisa!!
anyway!!
 
Wapumzike kwa amani! Magamba yamewatumia, yamefanikisha lengo, yamewatapika. Kwisha kazi
 
Back
Top Bottom