Arusha kwa sasa KWISHNEY!

Maisha ni magumu, watu hawana fedha. Ni tatizo la uchumi wa nchi. Nahisi wewe unataka kuunganisha Arusha na siasa za CDM. Mtwara kuna maisha mazuri? Kuna biashara nzuri toka asubuhi hadi usiku?

unaongelea Mtwara ya nchi gani yenye maisha mazuri ndugu?
 
Mbona juzi juzi tuu jiji la Arusha na Manispaa ya Moshi imetajwa kama miji misafi hapa nchini? Huwezi kupima uchumi wa Arusha kwa kuangalia uchangamfu wa biashara katika maduka ya stendi ndogo hasa msimu huu ambao siyo wa sikukuu.

Mkuu hakuna uhusiano wowote kati ya mji kuwa msafi na mzunguko wa pesa.
 
hali ni mbaya kila kona ya nchi hii..nafikiri ipo siku majiji yetu yataanza kushushwa hadhi na kuwa MANISPAA
 
Hali ya uchumi sio nzuri, na kipato cha mtu mmoja mmoja nacho kinadidimia siku hadi siku. Sio kwamba wananchi hawajitumi au wengi wao ni vipi, la! ni sera na ilani za ccm tu.

Kwa sasa ktk vipaumbele vya serikali, kikubwa kuliko vyote (Mgimwa hakukitaja) na chenye kuchukua zaidi ya 70% ya muda na rasilimali zote ni namna gani ccm itabaki madarkani baada ya uchaguzi ujao wa 2015. So hivi vipaumbele vingine ni kama viini macho tu lakini kila kitu kimeeelekezwa huko, je kwa uhalisia huo maisha ya mtanzania wa kawaida yataacha kuwa mabaya?
 
Nashukuru na nimeliona limeandikwa pia kwenye blog ya michuzi. Tuacheni utani na masihara mji wa Arusha kwa sasa una hali mbaya sana. Hali ya mji wa Arusha kiuchumi kwa sasa sio maridhawa kabisa. Nilijaribu kutembelea maeneo mengi ya kibiashara km sokoni ambapo kuna maduka mbali mbali . Ikifika saa 10 tu jioni wanaanza kufunga hakuna wateja, hata zile siku za kawaida za kazi. Biashara za taxi , ma-bus ndio usiseme, karibia 90% ni mbovu mbovu sana. Hali ya usafi wa mji ni mbaya sana. Kwa kweli , wana JF tuna haja yakuutizama upya mji huu, GENEVA OF AFRICA INAPOTEA KWENYE RAMANI

Uchumi utakuaje wakati muda mwingi watu wanapoteza kwenye mikutano ya kisiasa na maandamano?
 
Mbona juzi juzi tuu jiji la Arusha na Manispaa ya Moshi imetajwa kama miji misafi hapa nchini? Huwezi kupima uchumi wa Arusha kwa kuangalia uchangamfu wa biashara katika maduka ya stendi ndogo hasa msimu huu ambao siyo wa sikukuu.

Soma thread yangu vizuri utanielewa, maeneo niliyotembelea ni mengi. Na jua kwenye mikusanyiko mingi ndipo kwenye biashara
 
Maeneo ya Unga Limited, Sakina, Stand ya vifodi, ukipita maeneo hayo kwa kweli kiuchumi kunasikitisha sana maduka ya nguo hakuna wateja wakati kipindi cha nyuma biashara ilikuwa nzuri sana Arusha, hata wale vijana wajasiriamali walikuwa wanakwenda Nairobi kuchukuwa biashara saizi wapo tu mitaani hakuna kazi.
 
Mi nadhani labda mtoa mada atakua amedondoka toka huko mbele mda si mrefu ndio maana anaona kama vile mji umezorota sana..hali hii ni kawaida kama ulikua nje ya nchi kwa muda flani halafu ukarudi hm.lzima utaona kama vile hali ya maisha imeshuka sana kulinganisha na zamani!!! Zamani imeshapita..sikatai hali imekua mbaya Arusha..lakini mabadiliko ya kiuchumi ya mji wa arusha yametokea kutokana na mambo mawili makubwa....kwanza ..baada ya machimbo ya tanzanite kumilikiswa makaburu na pili...baada ya september 11, na mtikisiko wa uchumi wa dunia...watalii walipungu kwakasi ya ajabu...hivyo kwa kiasi flani uchumi wa arusa umeshuka lakini sio sana ingawa bado kuna masalia ya tanzanite na watalii..lakini ikumbukwe kua idadi ya makampuni pia imeongezeka hivyo ushindani umekua mkubwa pia katika sekta zote..mji pia umetanuka sio kama zamani town ndio ilikua kila kitu..
 
Majebere unataka kusema Lema ndio kaondoka na uchumi wa Arusha? Wewe ndio kichaa maana hujui hatma ya nchi hii haiko mikononi mwa CCM.
 
Rekebisha kidogo hapo, ni Lema sio mheshimiwa mbunge. Halafu hivi wewe umeenda Mwanza hivi karibuni? Nakushauri uende ukaone biashara inavyo kwenda.

Angalia hicho ulichokalia,ndo kinachokufanya upate kichefuchefu na kutapika pumba hizo!
 
Back
Top Bottom