GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 306
Nashukuru na nimeliona limeandikwa pia kwenye blog ya michuzi. Tuacheni utani na masihara mji wa Arusha kwa sasa una hali mbaya sana. Hali ya mji wa Arusha kiuchumi kwa sasa sio maridhawa kabisa. Nilijaribu kutembelea maeneo mengi ya kibiashara km sokoni ambapo kuna maduka mbali mbali . Ikifika saa 10 tu jioni wanaanza kufunga hakuna wateja, hata zile siku za kawaida za kazi. Biashara za taxi , ma-bus ndio usiseme, karibia 90% ni mbovu mbovu sana. Hali ya usafi wa mji ni mbaya sana. Kwa kweli , wana JF tuna haja yakuutizama upya mji huu, GENEVA OF AFRICA INAPOTEA KWENYE RAMANI