Arusha kumekucha

du kweli nch ishauzwa arusha hakuna umeme mji mzima daladala hakuna maji hakuna na mbunge wetu hayupo du kweli magamba kiboko
 
Wana JF huku Arusha hali ni tete baada ya madereva wa vifodi kugoma wakishinikiza mbunge wao aachiliwe huru na OCD Ars ahamishwe. Askari mmoja wa FFU kapigwa kajeruhiwa vibaya mno kwenye purukushani. Kituo cha vifodi kiko kitupu na barabarani hakuna kifodi hata kimoja, peoles are matching to and fro different areas.
NAWASILISHA

Tunaomba updates please! Ikiwezekana na picture tuwekee
 
nimewasiliana na mdogo wangu yupo huko kasema hali ni mbaya mjini, vurugu zimetawala, viford vimegoma kufanya kazi.
 
Waacheni watu wadai haki zao!ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa demokrasia umezidi hapa Arusha
 
Wakuu mgomo wa daladala hapa Arusha ni mkubwa sana, nilitoka katikati ya mji kuelekea, njiro hakuna daaladala. nimetumia taxi na nilipotoka sakina kuingia mjini the situation is worse.
Nikasimama sehemu kuwasikiliza machalii wa jiji wanasema wameshazoea mabomu hivyo Zuberi aendelee kumdharau Mungu.
 
Itafaa zaidi mlioko huko mkituwekea picha hapa tuone kinachojiri
 
Wakuu mgomo wa daladala hapa Arusha ni mkubwa sana, nilitoka katikati ya mji kuelekea, njiro hakuna daaladala. nimetumia taxi na nilipotoka sakina kuingia mjini the situation is worse.<BR>Nikasimama sehemu kuwasikiliza machalii wa jiji wanasema wameshazoea mabomu hivyo Zuberi aendelee kumdharau Mungu.
 
Hali ni shwari alakini si shwari kwakuwa wtu wamekosa mahitaji yao ya msingi,ukikosa usafiri hakuna kitakachokua kinaendelea.watu wapo wamesimama vituoni hakuna hata gari moja inayobeba abiria na jua linawaka sana.

Tatizo la arusha ni huyu ocd anaitwa zuberi alishaapa kupambana na lema mpaka mwisho tangu kipindi kile cha uchaguzi,hakuna asiejua bifu lake na lema.kwa ujmla hali ni mbaya kwani watu wapo wameshikwa na taharuki kwani mapolisi wapo wanapitapita na mbwembwe zao za kutishia raia.
 
Mnatuchanganya tuu...mara wamegoma, mara hawajagoma! Halafu kituko sasa watu wanaobishana wote washabiki wa CCM na Chadema....kwani huu mgomo unahusu chama? Watu wamedhani mbunge na wanaArusha hawatendewi haki na polisi....waendesha vifodi wakaamua kugoma kudemonstrate kwa polisi, Chadema na CCM wanaingia vipi? Au Chadema wanamiliki vifodi na CCM wanamiliki polisi? Upuuzi mtupu...
 
Wana jamvi heshima kwenu.

Ule mgomo wa daldala,taxi na bodaboda umeshindwa kufanyika kama ilivyotarajiwa.
Madereve wa daladala na bodabado wamekataa kuitikia mwito wa wanaharakati wa CDM wa kugoma kwa siku ya leo ili kushinikiza Mbunge wa Arusha mjini Mheshimiwa Godbless Lema aachiwe huru.

Mheshimiwa Godbless Lema aliigoma kuchukua dhamani na kukubali kwenda gerezani kwa hiyari yake mwenyewe ikiwa ni sehemu ya kupinga kuonewa na kunyanyaswa na jeshi la polisi mkoani Arusha.

Nimezungumza na madereva wa daladala na bodaboda wengi wamekataa kuunga mkono mgomo kwa kigezo kikubwa kwamba Lema hakunyimwa mdhamana bali alitakaa mwenyewe kwenda magereza pengine ni sehemu ya mkakati wake wa kufungua matawi mengi ya CDM au kujitafutia umaarufu zaidi ambao tayari anao.Wengine walienda mbali zaidi kwa kuniambia ajira yao inategemea malipo ya siku hivyo kugoma ni kujinyima rizki na kuziumiza familia zao pasipo sababu za msingi.

Wapiga debe wanajaribu bila mafanikio kuwalazimisha madereva wa daladala wapaki magari.Jeshi la polisi FFU wamezidisha doria ili kukabiliana na wapiga debe wanaotishia usalama wa daladala na raia.

Nitarejea baadae nipo mtaani kuwapa kile wanajamvi wengi msichopenda kuelezwa.

mmmmhhh!!!!
 
Ccm wanafika mbali sna sasa itabidi tuwe tunajichukulia wanachama wao majirani zetu. Too much sufferings coz of them.
 
Wana JF huku Arusha hali ni tete baada ya madereva wa vifodi kugoma wakishinikiza mbunge wao aachiliwe huru na OCD Ars ahamishwe. Askari mmoja wa FFU kapigwa kajeruhiwa vibaya mno kwenye purukushani. Kituo cha vifodi kiko kitupu na barabarani hakuna kifodi hata kimoja, peoles are matching to and fro different areas.
NAWASILISHA

ACHA UONGO WEWE.MIMI NIKO ARUSHA,MAMBO YAKO MURUA,BUSINESS AS USUAL. AM CDM Dam dam,lakini acha uongo kudanganya watu.
 
Wana JF huku Arusha hali ni tete baada ya madereva wa vifodi kugoma wakishinikiza mbunge wao aachiliwe huru na OCD Ars ahamishwe. Askari mmoja wa FFU kapigwa kajeruhiwa vibaya mno kwenye purukushani. Kituo cha vifodi kiko kitupu na barabarani hakuna kifodi hata kimoja, peoles are matching to and fro different areas.
NAWASILISHA
Tukio hilo lietokea eneo gani?
 
Back
Top Bottom