Real Masai
Senior Member
- Oct 12, 2011
- 123
- 24
hivi ni kweli JF kuna vichwa? yaani mbona hamtoi hoja? yaani wote mnadai nina chuki sasa hata kama nina chuki jibuni basi hoja ili ijulikane nina chuki! nina wasiwasi hata hamjui mbunge wenu kawafanyia nini! kama wa CCM hakufanya niambieni wa CDM amefanya nini?halafu swali jingine hivi tulimchagua Lema au CDM?
Nionavyo hapo, una chuki binafsi.Nikuulize, unajua Felix Mrema alikuwa Mbunge muda gani?Ukiwa na majibu ujiulize yafuatayo
1: Alichokifanya,
2: Wabunge wa CCM wengi wanatekeleza yapi kama si Serikali tuliyoipa dhamana ya kutatua matatizo ya Watanzania.
3: Lema amekuwa mbunge kwa muda gani. Ukipata jibu, jiulize ni mangapi anayoweza kuyafanya yy kama yeye zaidi ya kufwatilia Mipango mikakati ya Serikali.
4: Kazi (majukumu) hasa za mbunge zaidi ya kuisimamia na kuiambia serikali matatizo ya wananchi wake.
Kama nikipata majibu hapo juu, moja bada ya moja niseme yafuatayo.Uongozi ni dhamana kwa kulinda na kutetea raslimali za wanyonge.Unapokuwa na uongozi madhubuti lazima gurudumu la maendeleo lisonge mbele.Hasa nini maana ya UTAWALA BORA.Je ni kuweka siasa mbele,ama kuwa na mikakati ambayo ni endelevu?.Ni bora kuwa na fikra za kimaendeleo zaidi kwa kuwa rasilimali tunayo isipokuwa "Poor ACCOUNTABILITY". "If the Goverment is 100% accountable we will see efficiency and effectively performance".Siasa ni siasa, ila tunaitaji mabadiliko ya dhati kupata maendeleo na kumwangalia mtu ama chama iwe CDM,CCM ama chochote kile si hoja ila Uwezo, Fikra endelevu na uwezo wa kuishauri na kutekeleza majukumu yake ndani ya Mikango mikakati ya Serikali.Tunaitaji kuwa na uongozi thabiti ili kusimamia raslimali tulizonazo na si kelele za kumwangalia LEMA kafanya nini ndani mwaka na nusu ss toka awe Mbunge.
Tunaitaji Fikra Endelevu na Mabadiliko ya kweli.