Arusha bado ngoma nzito kwa JK!

hivi akipita arusha kutatokea nini?acheni siasa za uhasama nina hakika jk akija huko sioni kitakachotokea sanasana ninawaomba siku akitua ar mjipange barabarani kumpokea kwa shangwe na nderemo kama enzi hizo lengo ni kuepusha uhasamausiokwisha
haiwezekani!!!!!!!! Hizo nderemo labda kwao uko bagamoyo, ar big no!! Nae analijua ilo ndo akapita juu kwa juu, uoni serikali yake inawazuia watu ata kujumuika pamoja?? Uoni inavyowabambikia kesi watu wa arusha, uoni matamasha ya dini yakikesha ila wananchi wakithubutu wanabambikiwa kesi, jk hawezi onekana uko
 
Watu wanapenda kujidagnya bana hivi kweli rais Kikwete hawezi kupita Arusha kisa anawaogopa wana Chadema!

Hawezi jamani,ninyi wote mnaobisha najua wengine ni wausalama tell him to try nitakuwa shahidi kwani nitahakikisha nipo mjini that day.nawapenda na kuwakubali ndugu zangu wa Arusha.
 
Chadema kwa porojo bana, wameshindwa kuwafanya chochote RPC, RC, Rais ndio wataweza
 
Sijui wewe unaishi wapi hadi uwe mgumu kuelewa, lakini kwa ufupi mji wa Arusha uko katika Next Level!
Wana Arusha wana uwezo wa kufanya japo kitendo chochote ili kuonyesha wanachoamini na kusimamia mioyoni mwao.

Nimeshudia leo dereva mmoja wa magari yanayoenda kwa jina la MILANO(wanaoishi Arusha wanayajua sana), akigomea maelekezo ya traffic waliokuwa wanaopanga magari eneo la gereza kuu Kisongo, ili kuupisha msafara wa JK.

Dereva huyo amebebwa juu juu na wanausalama wa msafara huo kwa Tanganyika -jeki na kuingizwa katika gereza kuu la hapohapo Kisongo, na majaliwa yake ni Jumatatu ambapo huenda akapata mzamana!...mbaya zaidi kijana huyo haonyeshi kujutia kitendo chake!Usipime na Wana-Arusha jomba!
Kwa kujipa matumaini tu hamjambo!!! am sure, for 100% hata akifika Arusha hakuna mtakachofanya!!!Mnaweza kujaribu kufanya myatakayo lakini hamwezi kufanikiwa!

Tatizo lenu mnazani Arusha ni very special kwamba lazima JK apite...!!! Hivi ni nini kilichofanyika Arusha ambacho hakijawahi kufanyika sehemu yoyote TZ hii hata Rais wa nchi aogope kwenda huko?!

Kwa Arusha gani? Hii hii inayofanya machalii wasambaratike kwa kuogopa maji ya kuwasha na mabomu ya machozi?! Ikiwa mlishindwa kuwa wabiishi kwa issue ya kukesha pale NMC siku saba mfululizo, mtaweza kushindana na nguvu za dora ikiwa Rais wa nchi ataamua kutia mguu Arusha?

Wana-Arusha, msijidanganye, yaani mko bado saana kwavile hata maji ya kuwasha tu mnayaogopa!!!
 
ndugu yangu screenmaster nakubaliana na hoja yako labda niongeze kidogo kwa taarifa ya wana jamvi wengine ni kwamba jk hajawahi kukanyaga Arusha kwa mwaka mzima kufanya shughuli za kiserikali sasa kwa mara ya mwisho alifanya shughuli za kiserikali Desemba 17 mwaka 2010 alipofungua mount meru hotel na tangu wakati hajawahi kufika tena.

Novemba 12 mwaka huu alikuwa aje azindue mpango wa chanjo ya Taifa kwa watoto lakini katika hatua ya kushangaza alikuja makamu wa Rais Dk.

Bilal kuzindua badala yake na wakati huo watendaji wa serikali mkoani arusha walitangaza sana kuwa rais angezindua chanjo hiyo.Ifahamike kuwa Arusha ilikuwa kati ya mikoa michache ambayo katika awamu ya kwanza ya utawala wake aliitembelea sana na wakati mwingine hata mra mbili kwa mwezi kwa shughuli za kiserikali na hata zile binafsi

Swali ni kwamba je jk anahofu gani kuja ar? je ni mgogoro wa kisiasa wa Chadema ?je ni mgogoro wa ndani wa ccm baina yake na kundi la EL?
 
Hawezi jamani,ninyi wote mnaobisha najua wengine ni wausalama tell him to try nitakuwa shahidi kwani nitahakikisha nipo mjini that day.nawapenda na kuwakubali ndugu zangu wa Arusha.
Thats why we also like you! Only because unasema ukweli. Sala la Arusa ni zaidi ya wengi wanavyodhani. Maana hata lile swala la kukamatwa watu waliokuwa kwenye mkesha pale nmc ni mvua iliwasaidia polisi. Otherwise pangekuwa kosovo!
 
Ndugu yangu screenmaster nakubaliana na hoja yako labda niongeze kidogo kwa taarifa ya wana jamvi wengine ni kwamba jk hajawahi kukanyaga Arusha kwa mwaka mzima kufanya shughuli za kiserikali sasa kwa mara ya mwisho alifanya shughuli za kiserikali Desemba 17 mwaka 2010 alipofungua mount meru hotel na tangu wakati hajawahi kufika tena.

Novemba 12 mwaka huu alikuwa aje azindue mpango wa chanjo ya Taifa kwa watoto lakini katika hatua ya kushangaza alikuja makamu wa Rais Dk.Bilal kuzindua badala yake na wakati huo watendaji wa serikali mkoani arusha walitangaza sana kuwa rais angezindua chanjo hiyo.

Ifahamike kuwa Arusha ilikuwa kati ya mikoa michache ambayo katika awamu ya kwanza ya utawala wake aliitembelea sana na wakati mwingine hata mra mbili kwa mwezi kwa shughuli za kiserikali na hata zile binafsi

Swali ni kwamba je jk anahofu gani kuja ar? je ni mgogoro wa kisiasa wa Chadema ?je ni mgogoro wa ndani wa ccm baina yake na kundi la EL?

Labda ungeanza kushangaa kwanini tuna makamu wa rais, lakini kushangaa rais kuwakilishwa na makamu wake?! Sehemu yoyote ukisikia Mr. X anamwakilisha Mr.Y, basi juwa walitangaza kwamba ni Mr. Y ndie angefika hapo na sio Mr.X!

Wait, wait!! JK atakuja kuigopa Arusha endapo tu Wana-Arusha wataacha kuogopa maji ya kuwasha na mabomu ya machozi ambavyo imethibitika mnashindwa kuvihimili (refer Lema issue at NMC).

Huwezi kujisingizia kufa wakati hata kujisingizia kuzimia huwezi!!
 
Kajitengenezea maadui wengi acha ahangaike anaogopa kivuli chake mwenyewe.:lol:
 
Thats why we also like you! Only because unasema ukweli. Sala la Arusa ni zaidi ya wengi wanavyodhani. Maana hata lile swala la kukamatwa watu waliokuwa kwenye mkesha pale nmc ni mvua iliwasaidia polisi. Otherwise pangekuwa kosovo!

Haya sasa, ,kumbe hata mvua mnaiogopa!!! Mie nilizani maji ya kuwasha na mambomu ya machozi pekee!!!
 
Haya sasa, ,kumbe hata mvua mnaiogopa!!! Mie nilizani maji ya kuwasha na mambomu ya machozi pekee!!!

Ha! Ha! Ha! Mkuu, nimecheka sana, kwa hiyo mvua ndio iliofanya mpaka wakaacha yebo yebo zao uwanjani
 
JK alikuwa hana raha, mnyonge, mpole hana uchangamfu ... Stressed by Magamba in Dodoma?? Did Magamba proved him worthless? ... JK Should take care..... AND... Realy be careful with this. Because if he will let the magamba stress internalise ... Honestly and shurely his immunite wil be Compromised! ... And it will give his opponents the power he wouldnt wish!!

Definitely, he introduced this issue without an exit plan. Kazi yake ni kukaanga mbuyu na kuwaachia wenye meno (kina Nape) watafune, this time imekula kwake.
 
Makosa ya kiutendaji yaliyofanywa na yanayofanywa na jk kwa watanzania ni mengi lakini watz tunatofautiana namna ya kuelezea kutoridhishwa na uongozi wake na chama chake kwa ujumla. Nitatoa mifano michache 1. Wafanyakazi hawafanyi kazi ipasavyo ili kuonesha kutoridhika kwao mfano ipo wazi mwaka jana 82% ya wahitimu wa kidato cha nne walifeli, ajali za treni zinasababishwa ili kuonesha kutoridhika na sasa uchumi mzima unayumba thamani ya shiling, inflation nk kwahyo wanaArusha wana namna yao ya kuonesha kutoridhika.
 
Watu wanapenda kujidagnya bana hivi kweli rais Kikwete hawezi kupita Arusha kisa anawaogopa wana Chadema!


Mkuu wewe akili yako naona haina akili kabisa.Mtoa mad hakuna alikosema kwamba ni Chadema but kasema wana wa Arusha
 
Mbona mbeya hawakumfanya chochote RPC na RC lakini wakampiga mawe kikwete?

Wakampiga mawe Kikwete au wakaurushia mawe msafara wa Rais?! Wewe; acha masihara yako bana, kweli JK alipigwa mawe? alipigwa kichwani, mguuni, mkononi, mgongoni au sehemu gani ya mwili wake?!
 
Ha! Ha! Ha! Mkuu, nimecheka sana, kwa hiyo mvua ndio iliofanya mpaka wakaacha yebo yebo zao uwanjani

Umeona enhee, wengine tulikuwa hatujui ndipo mkuu Filipo katuhabarisha leo hii!!! Au inawezekana ilipokuja mvua, machalii ikabidi waanze kula kona kwa kuzani maji ya kuwasha yanamwagwa kwa helikopta kwa kutokea juu!!
 
Back
Top Bottom