Arumeru: Wanaohujumu Kampeni kufukuzwa

Itakuwa njema manake tutegemee kampeni za sera na sio sura
 
Wakiwaondoa hao CCM watamtuma nani tena? chama kile kimechafuka hakuna msafi! hao waliotumwa huko ndio hawana kashfa zinazoweza kuoneka kwa haraka!

Mimi ni mmojawapo wa wanajamii wachache wasio na itikadi ya kisiasa humu jamvini,hivyo maneno yangu hayana itikadi yoyote ya chama chochote kile cha kisiasa

Ninachoweza kusaidia CCM, CDM kama ingekuwa ni bidhaa wataalamu wa masoko [Marketers] wanasema ilifanya chaguo la walengwa wake [yani Marketing segment] wakati wa ujio wake iliingia kwenye mashule na vyuo na kuhakikisha kada ya wasomi wanailewa,.Nakumbuka miaka ya 1995 kuna watu ndani ya chadema waliokuwa wanatembelea mashule yenye A'Level na kuconvince wanafunzi kujiunga na chadema,pata picha toka mwaka 1995 leo hiii watu kama Zitto ni viongozi unategemea aina gani ya bidhaa CDM itakuwa imebeba.

Mchezo kama huu ulichezwa na kampuni ya TIGO [MOBITEL NA BUZZ by then] wakaingia mashuleni na kugawa namba na kutoa muda wanafunzi wakawa hewani,walilenga wanafunzi wakijua miaka mitano ijayo wanafunzi husika watakuwa ni watumiaji na wenye maaamuzi ya bidhaa yani kwa jina jingine watakuwa ndio wazalishaji na walaji kwenye upande wa jamii.

Hivyo Viongozi wa CCM kama Job na Wasira ni aina ya makada ambao hawajui propaganda za dunia ya sasa zikoje na zinapokewaje na umma hasa wa kada ya kizazi kipya.Sijui picha ya Job na Mwenzie wakati wanatamka hayo walikuwa wamepima kuwa kama jamii ikiyapokea itayatafasiri vipi?Lakini hadithi yote inayo likumba CCM ni makosa ya kimfumo ya CCM ya kubeba timu za wazee na kupeleka vitani na wenye Elimu ndogo ya kizazi kipya kinachotegemea kudanganywa kwenye uongo ulio karibu na ukweli na sio Propaganda za kizamani.

CCM walipaswa miaka iliyopita kuwa wamekusanya vijana wapya wenye damu zinazochemka wanaopanga maneno yenye kuleta sura halisi na pindi yakitiliwa nguvu yanauwezo wa kuleta tija na sio lundo la ndio mzee !!!,ndio mkuu !!! matokeo yake ndio hayo vijana wao wote ni ndio mzee,kijana ambae sie Mzee wameogopa kumpeleka kwa kuwa wanajua msimamo wake ulio wazi aushabihiani na mpigiwa kampeni.Inasikitisha sana na inauma kuwa CCM yenye umri mkubwa ninayoizidi miaka miwili hapa duniani kweli imekosa vijana aina ya Nape na wenye damu inayochemka Tanzania nzima, leo hii kusima mbele ya majukwaa na kujibizana na vijana wa CDM aina ya Vicent juu ya SERA na MAENDELEO WATAKAYOWALETEA WANA ARUMERU.

Sipendi na uwa nachukia sana mfumo wa CCM ambao umeundwa wa kuchagua na kuunda Viongozi wa chama chao ambao hatimae wanakuja kuwa ni Viongozi wa Taifa.Mara nyingi walio wakubwa kwa maana ya umri na madaraka ndani ya CCM,uwa awapendi kuwainua na kukuza vipaji vya vijana walio WAZI NA WENYE FIKRA BINAFSI KWA MAANA YA VIJANA WENYE KUJISIMAMIA KATIKA KUJIELEWA NA KUWA NA UFAHAMU WA NINI MAANA YA KUJIAANDA KUWA KIINGOZI.[FREEMAN-INDEPENDENT MIND].Aina hiyo ya kijana uwa hana nafasi ndani ya uongozi wa CCM,walio wengi ni wale wa NDIO MZEE !!!! ambao mwisho wa yote vichwa vyenye kuunda mambo yani hao watu wazima wakishachoka kuwatuma na kuwabunia mambo hawana jipya ndio utata unapoanza kwa kuwa vijana wao wenge waliundwa kuwa tegemezi [Spoon feeding] na kibaya zaidi wanakuwa watumwa wa michezo michafu.

Hakika sote tunajua isingekuwa BUSARA YA MWENYEKITI WAO Jakaya Kikwete leo hii NAPE ingekuwa HISTORIA ya KISIASA.Matokeo leo hii ni Nape pekee anaweza akakaa meza moja na TINDU LISSU wakabishana habari za mbinu zipi zi sawa za kupambana na ufisadi na sio aonyeshewe kidole kuwa nae ni fisadi.

CDM walipima na kujua kizazi kijacho ndani ya Tanzania miaka ya tisini,kuja elfu mbili watakuwa ni aina gani ya Watanzania hivyo wakawatayarishia viongozi vijana wa kukinadi chama.Hivyo CDM kwa kujua hilo kama la TIGO matokeo yake leo wasomi wengi wanaijua CDM na kuwa CCM kwa kukumbatia UZAMANI NA WAZEE WENYE ITIKADI YA UMWINYI/SUPERIORITY NA KUWA SISI NDIO WENYE NCHI.Matokeo yake CDM wakabeba new generation na graduate wakawa supportive mpaka hata walipoingia vyuoni wakawa tayari ni CREAM ya CDM.Ukileta na UFISADI wale kama sisi tusio na vyama inakuwa ni mizani ya kuona japo kidogo anapatikana mchokonozi wa kisheria ambae akichokonoa kwa wenye Nchi waliojivisha wao sisi Watanzania tuliopewa nasi haki na Mungu ya kuzaliwa Tanzania tukiwa tunacheleweshewa haki ya kuchangia ujenzi wa TAIFA hili kwenye maswala muhimu tunatizama yetu macho tukisubiria MUNGU ashushe nyakati zake ambazo huwa hazina longo longo wala mizengwe.

Manke nakumbuka nyakati uwa hazina longolongo wala mbwembwe kwa kuwa Mzee mmoja maarufu CCM Zanzibar marehemu Mzee Thabit inasemekana wakati JK alipokosa Urais mwaka 1995,Mzee yule kwa kujua ukweli alimwambia JK kijana usiwe na hofu wewe tulia Mungu akipanga amepanga hivyo wakati ukifika HAKUNA HATAKAE ZUIA UJIO WAKO,NA KWELI ULIPOFIKA WAKAJARIBU LAKINI WALICHOKIONA NA KUJALIBU WALIPATA WAKAJUA HAKUNA JINGINE BALI NIKUTOA SIFA KUMI NA TATU ZA MGOMBEA ANAETAKIWA NA CCM AMBAZO DHAHILI ZILIKUWA NI JK.

Hivyo Proganda haiwezi kucheza kwenye professional manake sikuizi dunia ilishasahau haya maswala ya Propaganda bali inaangalia kitu kinaitwa mahusiano ya jamii [Public Relation].Propaganda haina nafasi kama PR"Binadamu siku hizi atungiwi uongo bali anashirikishwa kujitungia uongo wake mwenyewe" Hivyo kwa kuwa CCM imejitoa katika kukusanya BRAIN mpya zisizo na majina ya UKOO kwenye siasa za Tanzania, yani BRAIN kama TINDU LISSU au ZITTO ni vijana wapya kabisa toka kwenye familia ya kawaida kabisa ya kitanzania wala sio watoto wa mwanasiasa yoyote mwenye jina kubwa hata mjomba au shangazi mwenye jina ngazi ya kisiasa kitaifa.

Matoeko yake Viongozi wa CCM na makada wkubwa wanatamka hadharani kuwa Mgombea achaguliwe ili afutwe machozi ya kufiwa na Baba yake mwanasiasa mwenzao hakika ukipima hayo utaona ni kejeri lakini ndani ya watamkaji sio kejeri wao hayo ni maisha, hawana Changamoto zenye kujua fikra mpya za kizazi cha sasa kinawaza nini vichwani mwao

Hivyo mpaka sasa CCM aina vijana wapya wasomi waliojitolea kwa moyo wao wote kuhakikisha wanasimamia kwa nguvu zao zote kuwa CCM isimame kama chama chenye sifa na jina la kuaminika daima kwenye umma popote pale ndani na nje ya miji mikuu na vijiji.Kila siku sasa CCM imekuwa ikitegemea kutetewa na wananchi wa vijijini ambao nao siku hizi TV na Radio zinaonyesha jinsi ndugu zao walio mijini wanavyoipinga, kupitia chaguzi ndogo ndogo sasa wananchi walioko vijijini wanaona ni jinsi gani CCM inaendelea kuumizwa na kunyanganywa keki ambayo daima walifiklia kuwa ni yao pekee.

Hakika ningekuwa ni Analyst wa CCM daima nisinge ruhusu watoto wa familia za wazazi walio kwenye siasangazi za kitaifa kugombea viti vya ubunge,ningeshauri waaanze na ngazi za chini kabisa.Leo tazama SIOI [Mfutwa Machozi] katoka uko alikotoka kama vile HAKUNA vijana ndani ya CCM ambao hawana majina ya kifamilia kwenye siasa na pia ni wasomi wanaokubalika kwenye jamii hata kama ni kwa Washiiri tu na sio lazima awe na jina Dar es Salaam ndio aweze kukubalika kuwa Mbunge.Matokeo ya mfumo huo vijana wanaendelea kutengeneza chuki,bali watu wazima wao hakuna shida kwa kuwa wao wameshapoteza wanawoga waliokwisha mezeshwa kuwa CCM ndio mwamuzi wao lakini kizazi hiki kilichofuatwa na CDM mashuleni na vyuoni ndio kinaongezewa kaa la moto na ndio maana atuishi kuona CDM wakitamba kuwa wao ni PEOPLE'S POWER AND VOICE.

Aiitaji kuwa na degree kujua kati ya mtu mzima na kijana nani ana nafasi ya kuishi duniani kwa mapenzi ya Mungu. CCM kwa kuendelea kutegemea watu wazima ambayo yenyewe dhahiri inajua ilishawalibu na Propaganda za kizamani na zisizo na mashiko ambayo wao kwa ukweli wanajua kuwa Propaganda hizo huko tunakokwenda zimekosa manufaa kwao wao na chama chao.

Binafsi naamini kabisa kuwa Mzee Mkapa alichokuwa anafanya kuhusu VICENT na FAMILIA ya MWALIMU NYERERE ilikuwa ni PROPAGANDA lakini kwa kutokujua kuwa kizazi cha sasa ambao wengi wao wana umri wa kuanzia miaka 16+ mpaka -45 kushuka chini wameshakuwa si kizazi cha Propoganda za soviet ya zamani, bali ni kizazi cha kushirikishwa kudanganywa.Hivyo Mzee wa watu alivyowashushia CDM propaganda wao wakamshushia shirikisho la udanganyifu matokeo yake ndio hayo Mzee wa watu chali inatafutwa namna ya kunusuru na zigo alilotwishwa ambalo tayari madhara yake ni makubwa sana.

Hivyo ushauri wangu kwa CCM wajipange kwa yafuatayo
1: Kwanza kurecruit vijana wapya kabisa kwenye Safu ya utetezi,kuleta sura mpya kabisa yani majina yasiokuwepo kwenye sura ya kisiasa ngazi ya kitaifa Nchini,wasaidiane na NAPE wao ambae ndiye naona anaemsaidia JK kidogo kufuta aibu ya kusema wazi lolote lile mbele ya umma ukizingatia gumzo letu kuu watanzania ni UFISADI.

2: Kuunda kikosi kazi kipya kwa ajili ya kuludisha Heshima kwenye jamii,maanalyst hawa wasiwe na itikadi ya UCCM damuni yani wawe ni wale wanaosukumwa kushauri ukweli kuhusu jamii dhidi ya CCM.Hawa watatoa mchango wa nini kifanyike kuhusu CCM.Ukweli CCM haikubaliki mijini na pole pole inaanza kusambaa kuingia vijijini ambako ndio ngome ya mwisho ya CCM na picha hiyo kwa vijana kitendo cha wanaccm kendelea kuona CCM kuwa mambo yako shwari basi ndio kusema CCM inakubali KIFO CHAKE yenyewe.

3: Kutafuta njia na majibu ya nini kifanyike ikubalike TIBA ikiwemo kukubali kuwa UFISADI ni donda hivyo kuendelea kukumbatia kuwa eti hakuna msafi hivyo hakuna wa kumnyooshe kidole mwenzie basi ni kujisogeza karibu na kifo.

4: kuakikisha wale wote wenye kampeni za waziwazi kuhusu urais wa 2015 wanakumbana na lungu la chama iwe ni kwa kuhujumiwa au kuonywa kwa dhahiri mbele ya umma kuwafichua wazi kuwa fulani asisikilizwe kwenye kampeni alizokwisha anza .Vinginevyo,ccm wataisikia 2015 kwenye BOMBA ndio kusema hata mfumo kwa miaka mitano hii itakuwa imeshajiaanda kufanya kazi na CDM kwa kuwa uchaguzi ujao kama CCM watendeleza Propaganda basi MFUMO wajiaandae kuwapokea CDM, vinginevyo patachimbika na lawama zitakazoibuka baada ya jamaa kutaka KIELEWEKE basi itakuwa imebaki ni kazi ya MFUMO kujipanga ni jinsi gani watafanya kazi na chama cha kipya cha madaraka nje na CCM.

Manake binafs daima nimekuwa nikisema SIPENDI CCM IFE kwa kuwa KIFO CHA CCM , CDM HATAKUWA NA MPINZANI. NA WALE WOTE WENYE KUIOMBEA CCM IFE WAJUE KUWA ITATUCHUKUA MIAKA ISHIRINI TENA KUPATA MPINZANIA WA CHADEMA HIVYO CHADEMA AKIINGIA MADARAKANI UJENZI WA CHAMA PINZANI KUISIMAMIA CHADEMA UTATUCHUKUA MIAKA NA MIAKA NA HIVYO TUTALUDI KULE KULE ILIVYOTUCHUKUA MIAKA KUIONA CDM INASIMAMA KAMA CHAMA RASMI CHA UPINZANIA TANZANIA.

Je wakati tunaangaikia ujenzi wa chama cha upinzani baada ya CCM kufa Mlinzi wetu [Watch Dog] wa mali na mfumo na mienendo ya shughuri za Serikali na Maendeleo atakuwa Nani ?

Hivyo tuombe CCM isimame kama chama ambacho kikishindwa kujinadi mbele ya Umma na kukosa mandate ya kutawala basi,nao wawe chama cha UPINZANI kama KANU,ZANU na vinginevyo barani Africa lakini wenye nguvu ya kuwatingisha CDM,kama CDM anavyowatisha wao sasa.

CCM pelekeni watu wa kuuza sera,sio wauza sura na majungu ya Kisiasa.
 
Wana JF baada ya Mkuu wao(Leiguanan)kutinga Arumeru vikao vya ndani Mfululizo vimekaa na kuanza kushutumiana na kufikiria kupanga Safu Upya Jana katika Kata ya Akheri katika kikao cha Ndani na akina Mama wamemshauri Lowasa kuwatimua Sendeka,Kibajaj,Wasira na Maji marefu
KIBAJAJ:yeye ni muhujumu number moja kwa kauli yake ya kusema Siyoi apewe ubunge ili Kufutwa machozi ambayo imepingwa vibaya sana wakazi wa Arumeru huku akipita chini chini na kuthibisha mgombea wa CCM ni spoonfeeding hawezi kujieleza Mwenyewe..pia Kibajaj alikatazwa na Lowasa kwenda Igunga kwenye kampeni akaenda kwa Kiburi na Lowasa akamfuta kwenye kundi Lake na walihoji nani kamleta?
OLE Sendeka:ametajwa kuwa Double Agent baada ya kutofautiana Mara kwa Mara na Vijana watiifu wa Lowasa na kutoa kauli za dharau na Ubaguzi ili Siyoi asichaguliwe na Mbaya zaidi ni Pale alipoutafuta Msafara wa Mgombea wa CHADEMA kule Mikungani ili kumkaribisha Mjengeni na kumpa Pongezi kuwa tayari ame shinda(alikutana na Msafara na akausimamisha)alipoambiwa na DR Acha Unafiki alisema ni kweli vijana wako wametushinda nampa Pongezi and I mean It,kauli ambayo kambi ya pili imechukizwa nayo. Na kusema ni Msaliti afukuzwe..
WASSIRA: yeye japo ni Mlezi wa CCM mkoa wa Arusha amesahtumiwa kwa Wote na Lowassa Wanataka kiti cha Urais basi wasira anahujumu Siyio Aanguke ili kudhoofisha nguvu Ya Lowassa ili pia katika mbio Za Urais asiwe na pa kujititumua baada ya Mkwe wake kuanguka vibaya,maana kauli zake kurudia alizotangulia kusema Mkapa ambazo zimelitikisa Taifa amekuwa akizirudia ili kuchochea Ugomvi na yeye anatakiwa atoke..
MAJI MAREFU: yeye pia ametajwa kama muhujumu number nne kwa kuwa Mzazi mwenzake Marry Chatanda hakuwa anamtaka Siyoi Tangu Mwanzo na Maji marefu anatuhumiwa kuvujisha Siri na Mipango ya CCM hasa pale alipopangiwa kutoa Hongo shuleni na Vyuo na CHADEMA wakatangaza jukwaani,Mbaya Zaidi ni pale alipoaenda Elephant Lodge anapokaa mgombea wa Chadema na timu yake Kuwapa Pongezi na kumkum batia Mgombea wa CHADEMA huku akimkaribisha Mjengoni,baada ya Kustukiwa na waandishi wa CCM na makachero wa Lowassa ika bidi atimue mbio na Gari dogo la Kukodi na kukimbilia kambi ya CCM huku akisingizia anataka kuuwawa na CHADEMA,jambo ambalo CCM wamelikataa na kusema yeye ni Msaliti.
FAMILIA YA KAWAWA KUTINGA ARUMERU:katika kikao hicho wameamua kuwaita watoto wa Kawawa ili waje kujaribu kuokoa JAHAZI baada ya VINCENT NYERERE kuipeleka puta sana CCM uamuzi huo uimechukuliwa na kikao cha pili cha ndani ili kujaribu kupunguza ukali na mbinu za Vincent huku wakiamua kuyatumia zaidi Magazeti kumchafua Vincent kwa kumkata Nguvu kwani amekuwa Mwiba mkali kuliko ilivyotegemewa..
Kutoka ARUMERU ni Mimi Mgeni wenu wa JF
 
Mgeni Wetu kutoka Arumeru Mashariki unapata wapi hizi data?

Nikiona hao uliowataja wamepotezewa then nitakuamini na pia nikisikia Vita Kawawa na dada yake wamekuja huko Arumeru then nitakupa full credit.

Je Maria (Mary) Chatanda hayuko kwenye Timu ya Kampeni?
 
Asante sana; sasa hivi kutoka na vyanzo mbalimbali kuna jambo moja ambalo liko wazi sana - kuruhusiwa kwa Siyoi kugombea Arumeru Mashariki ilikuwa ni mbinu maridadi ya kumpa Lowassa kamba ya kujinyongea.

a. Lowassa akishinda na Siyoi wake itamthibitisha kuwa anaweza kuishinda serikali na chama chake na atakuwa officially ni King Maker. Nasikia hakuna kiwango cha fedha ambacho hakitatumika kuhakikisha Siyoi ashinde. Vyanzo vyote vinathibitisha kuwa CCM (EL camp) wako tayari kutumia fedha kushinda na kwa fedha CDM wala haitaweza kuwakaribia.

b. Lowassa akishindwa itaacha uchungu mdomoni kwa sababu kwanza anajua kuwa harakati nzima zimekuwa sabotage na wana CCM wenzake na ninaamini hatoona aibu kusema hilo aidha hadharani au kwenye vikao vya chama. Hili hata hivyo litategemea sana kama ataamua kupanda jukwaani. Akipanda jukwaani manake ni kuwa kampeni nzima ya Siyoi itakuwa ni kupitia mgongo wa Lowassa.

Lakini wakianza kuumana wenyewe ni CDM ndio itatakiwa ioneshe inatumia vipi nafasi hiyo kupata kura za wana CCM...
 
siku chache tu zimebaki za campaign, upepo u safi kwa chadema hadi sasa, kipindi wao wanaendelea na kusuguana ni muda mzuri wa chadema kuwamaliza kabisa.
 
Duh, najaribu kutafakari Mary Chatanda na Maji Marefu.... kumbe ndio maana yule mama yuko vile
 
Mkuu usiwe na haraka mtoto hukua taratibu, matawi yatapatikana tu! CCM walijijenga wakati ya chama kimoja, hawakuwa na mshindani, hilo lisikupe tabu.

Na pia kwa kumuongezea huyo "Cuf Ngangari" ni kwamba, wapiga kura sio wanachama tu wa vyama vya siasa. Kura unapigiwa na watu wote waliokukubali, yaani wanachama wa vyama vyote na wasio wanachama. Hivyo takwimu za wanachama zina mislead sana kama anataka kuzitumia kuhesabu kura.
 
Hatari ya hujuma dhidi ya Siyoi na CCM kwa ujumla alitakiwa aione Mwenyekiti wa Chama kwanza wala sio Lowassa anayepaswa kushughulikia hili yeye kama yeye. kama Lowassa atafanikiwa kurekebisha hili akiwa yeye mwenyewe basi kutakuwa na haja kutenganisha kofia ya URAIS na Uwenyekiti wa Chama.
 
Huyo amekuwa akitajwa kuwa ni mnafiki! hivyo haaminiki.

huyu sio mnafki bali ni miongoni mwa wagombea ulaji 2015 na ndio maana kuna kundi lingine hawamtaki na wameamua kumchafua, waache wachafuane wenyewe sisi cdm waleeeeeeeeee!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom