Arumeru: Tunasubiri uthibitisho kuwa hamdanganyiki

Noboka

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
1,246
626
"Kwakuwa kule bungeni kuna kula, tumpe kura Zitto Kabwe, ili na yeye akale kama alivyokula mwenzake wa CCM".
Nimeanza na nukuu hiyo ambayo ilitumika sana mwaka 2005 kuhamasisha wazee ili wamchague Zitto Kabwe kuwa mbunge. Kinachotokea leo kule Kigoma Kaskazini, Zitto pamoja na mapungufu yake kama binadamu, lakini wapiga kura wake hawajuti kabisa kumchagua. Nimefuatilia sana kampeni zinavyoendelea hadi nasema kama wananchi wetu wangekuwa na ufahamu mkubwa nadhani CCM wasingekuwa na ubavu hata wa kupanda jukwaani kudanganya watu, wangestahili kutemewa matema kama ishara ya laana.
Hivi miaka karibuni 50 mko madarakani na leo unaenda kwa wapiga kura kuwadanganya,ardhi, maji ooh sijui viwanda anyway labda ndiyo maana kina Mwigullu wanaishia kutueleza historia za mapenzi tu kwani hakuna la maana wanaloweza kuzungumza.
Sasa aidha Nasari atafanya kitu au hatafanya, mpeni nayeye akale kama wanavyokula wengine kwani na yeye si mtoto na kijana wenu? Halafu 2015 mtaamua mnavyotaka tena, lakini nina imani hamtajuta!
Kiukweli kama toka miaka ya hamsini wameru mlienda kudai uhuru kuhusu masuala ya ardhi na leo bado hilo ni tatizo, Mungu awape neema msiwape ushindi CCM labda waamue kujitangaza, vinginevyo mtakuwa mnajipa laana wenyewe.
 
Ni kweli mkuu naungana na wewe asilimia 100. Nilisikiliza clip ya lusinde nikafikiri nasikiliza mateja ni hatari sana kwa taifa Hili kuanzia sasa namtangaza lusinde Kama janga la kitaifa
 
Back
Top Bottom