Arumeru Mashariki hawaitaji sera wanaitaji porojo - Mwigulu

Katika hali isiyo ya kawaida na wala haikutegemea kusikia kauli kama hii kutolewa na kada na meneja wa kampeni kwa mgombea wa ccm kwenye uchaguzi wa jimbo la arumeru mashariki mwigulu kuwa sababu inayowafanya ccm kampeni zao zitawaliwe na matusi na siyo sera zenye kujibu matatizo ya wanaarumeru ni kuwa kama wakitoa sera ambazo zitakuwa na uchambuzi wa kiuchumi basi mkutano utakaofuata watakosa watu ndiyo maana wanapiga porojo zilizojaa matusi,dhiaka na kejeli.
Mytake.
Kama ccm inajengwa na vijana mithili ya mwigulu basi kwishenie
 
Ukweli ni kwamba hawawezi kutangaza sera za chama maana wanaogopa kuulizwa maswali ambayo hawana majibu yake, kwani sera huandamana na ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa lakini hazitekelezeki.
 
Dah hawa watu wamefikia pabaya jamani.

Kinyungu hilo lipo wazi haliitaji tochi kuliona ukifuatia uzi wa jana walipo fanya kampeni tindigani mwigulu katoa live katika utetezi wake sababu ya wao kutukana kwenye kampeni
 
Ukweli ni kwamba hawawezi kutangaza sera za chama maana wanaogopa kuulizwa maswali ambayo hawana majibu yake, kwani sera huandamana na ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa lakini hazitekelezeki.

Saudi hizi kampeni zimeshapoteza mvuto yaan badala ya mgombea ndiyo amwage sera zake kwa wapiga kura wapambe ndiyo wanafanya hiyo kazi.
 
...wamesoma mazingira labda na kugundua wanaArumeru wanapenda matusi, kashfa,majungu na wanajaa kuyasikiliza.
 
Katika hali isiyo ya kawaida na wala haikutegemea kusikia kauli kama hii kutolewa na kada na meneja wa kampeni kwa mgombea wa ccm kwenye uchaguzi wa jimbo la arumeru mashariki mwigulu kuwa sababu inayowafanya ccm kampeni zao zitawaliwe na matusi na siyo sera zenye kujibu matatizo ya wanaarumeru ni kuwa kama wakitoa sera ambazo zitakuwa na uchambuzi wa kiuchumi basi mkutano utakaofuata watakosa watu ndiyo maana wanapiga porojo zilizojaa matusi,dhiaka na kejeli.
Mytake.
Kama ccm inajengwa na vijana mithili ya mwigulu basi kwishenie

Nchemba+Lusinde=0
 
Subirin tar 1 April tutajua aliyeishiwa sera. Mimi sina shaka na kama nimeishiwa na cdm wanataka kushinda ndio kweli wananishauri niondoke. Kilio cha nini kama CCM IMECHOKA? AM CONFIDENT CCM ITASHINDA

Kijana kama wewe kuongea mambo yasiyo na tija kwa maendeleo ya jamii ni dhambi.
 
Walianza na umri mdogo wa Nassari, wakaja na madai hajaoa, sasa hana NGO, analisha mbwa wa kizungu. Mwigulu mtu asiye na NGO ana kasoro gani? Na mtu anayelisha mbwa wa kuzungu ni kichaa?

Kama kweli Mwigulu na wenzako ni wanaume wa kweli itisheni mdahalo. Acha wananchi waulize maswali ndio tutajua nani fundi na nani kibarua.

Mdahalo unahitajika sana pale Arumeru. Sijui kama kuna mtu/taasisi/chombo cha habari ambacho kina mpango wa kuweka mdahalo kati ya wagombea?!
 
Kuhusu kutokuruhusu maswali ndugu yangu kwanza muda ni kikwazo pili huyu ndio kwanza anaomba ubunge angekuwa anaomba mara ya pili kuna la kujibu tatu mikutano ya hadhara kuna matatizo sisi huwa hatufanyi vurugu mikutano ya wenzetu ila kwetu ukiruhusu hayatakwepo maswali ya maendeleo bali namna gani mgombea abomolewe. Kuhusu porojo ndg yangu ndicho watu wanachotaka kusikia. Mimi first class economist nikishusha mambo ya growth models na inflation targeting siku inayofuata sipati watu mkutanoni. Samahani kama jibu halijatosheleza mengine ni utaratibu wetu kwamba tujibu kwanza kashfa alizozushiwa mgombea badala ya yeye ili mgombea aseme sera tu

Hapo kwenye RED panadhihirisha kuwa CCM imebaki na wapiga kura wajinga tu.
Kwa upande mwingine umeamua kuwatukana Wameru.
Hakika kuitetea CCM inahitaji uwe na akili ya maiti.
 
Wakuu salaam,

Leo CCM walikuwa katika viwanja vya Nkoanrua Primary, kwanza wameambulia takribani robo tu ya watu waliokuwepo siku chache zilizopita ktk mkutano wa CDM ambapo Dr. Slaa aliunguruma hapo! Pamoja na uchache huo nimeshangaa kuona watu wote uwanjani hapo wakinyoosha vidole viwili (alama ya chadema) baada ya kuona Helikopta ya chadema ikipita kuelekea maeneo ya jirani ktk kampeni!

Watu hao (ingawa ni wachache) inaonekana wamepatikana pia kwa shida kwani walikua wakisombwa na malori, Coaster na Hiace kadhaa ambazo zilikodishwa! Sijui aliyezilipa ni nani hasa! Ila jana pia nimeshangaa kuona Ole Sendeka na Lowasa maeneo ya Arumeru wameongozana japo kila mtu alikuwa kwenye gari lake!

Viwanja vimetawaliwa na matusi na kejeli yaliyotolewa na Mwigulu kuelekezwa kwa wananchi kwa kosa la kuzomea msafara wa CCM, maeneo mengi ambapo inaaminika ni kambi za CDM, CCM imeambulia kuzomewa huku wengine wakipiga ukunga wakisema wezi haoooooo! kila walipopita!

Nawasilisha!
 
katika hali isiyo ya kawaida na wala haikutegemea kusikia kauli kama hii kutolewa na kada na meneja wa kampeni kwa mgombea wa ccm kwenye uchaguzi wa jimbo la arumeru mashariki mwigulu kuwa sababu inayowafanya ccm kampeni zao zitawaliwe na matusi na siyo sera zenye kujibu matatizo ya wanaarumeru ni kuwa kama wakitoa sera ambazo zitakuwa na uchambuzi wa kiuchumi basi mkutano utakaofuata watakosa watu ndiyo maana wanapiga porojo zilizojaa matusi,dhiaka na kejeli.
Mytake.
Kama ccm inajengwa na vijana mithili ya mwigulu basi kwishenie
wakuu sera ya ccm wanaifahamu walioiandaa asilimia 99.99.ya viongozi wa ccm akiwemo katibu mkuu mukama,nape,pinda na jk mwenyewe hakuna anaeifahamu kwa sababu hailingani na matamko yao hata jk aliwahi kukili kua haifahamu sera ya ccm.mungu ibariki tanzania.
 
Ole Sendeka ameishajisalimisha kwa Lowassa, tunamsubiri Nape tu naye aende huko. Wazungu wanasema if u can't beat them join them...

Hivi Laigwanan anaweza kupanda jukwaani na kutoa siasa za maji taka. Ni kama kila atakachosema jibu litakuwa "NA WEWE" mfano akisema Siyoi atapambana na mchwa katika halmashauri ya Meru, wananchi watajibu "MCHWA NA WEWE" tena malkia wao... Sidhani kama Laigwanan nywele nyeupe atapanda jukwaani
 
komba alikiri kwa kinywa chake kuwa ccm imezidiwa,yupo arumeru kutimiza wajibu tu!
 
Back
Top Bottom