Arumeru Mashariki, CHADEMA kunyakua jimbo?

Itakwa vema kama jimbo hili litabaki chini ya ccm, kwa sababu mtoto wa sumari ataweza kuendeleza na kuzifanyia kazi ahadi alizoweka babake. Goodluck kwa sioi
 
Mkuu hao vijana wapo wangapi? Wewe ndio wamekutuma uje uwasemee humu JF? kwa nini usipeleke malalamiko yao pale Lumumba.

Mkuu Ritz,
Nakumbuka wakati wa uchaguzi mdogo wa Uzini uliahidi kwamba CDM ikishinda utatembea uchi kuanzia Ubungo hadi Kimara - Bonyokwa. Vipi kuhusu uchaguzi wa Arumeru? Hatujasikia ahadi yako Mkuu! Au ndiyo unaogopa kutembea uchi??
 
Hawana ubavu huo wa kumkataa, sera za chama chao ni kulindana, wangemkataa SIOI ambaye kachaguliwa kwa vishawishi vya rushwa. Ila Mkapa atakumbuka machungu yaliyompata sehemu fulani Machame mwaka 1995, uchaguzi wa vyama vingi wa kwanza alipopambana na Mrema, walizomewa pamoja na Dr. Omary Juma wakaishia kusema acheni kutuchagua kwanza huyo Mrema wenu hapati urais.

ilitokea Masama huko Hai
 
Acha umbea mtoto wa kiume . Utafuatwa na matarumbeta . Shauri yako .
 
Je chadema itayaweza maarifa na "nguvu" anazodaiwa kuwa nazo kada mmoja tu maarufu wa ccm ambae is nothing than mbunge wa monduli bwana Lowassa?

Ikumbukwe kuwa katika kinyang'anyiro hicho mgombea wa ccm ni mkwe wake bwana lowassa ambae inaelezwa amepigana kufa na kupona na kuzishinda "fitna" za uchaguzi za ndani ya ccm na kufanikiwa kumuwezesha mkwe wake huyo kuwa mteule wa ugombea wa kiti cha ubunge wa arumeru kilichoachwa wazi kufuatia kifo cha babake.

Je chadema itaviweza vishindo vya Lowassa kama ilivyofanya Arusha mjini wakati wa uchaguzi mkuu ambapo ilielezwa mgombea wa ccm(yule mama nimemsahau jina lake)nyuma yake kulikua nguvu kubwa za lowassa ambazo hata hivyo zilishindwa kuonekana mbele ya mgombea wa chadema bwana Lema;leo mpambano wa lowassa na chadema unarejewa tena ndani ya viunga vilevile vya arusha ambako pande zote mbili,lowassa an chadema zinaelezwa kuwa nguvu...dalili zinaonyesha nani ataibuka mbabe???

Nawasilisha.....!
 
Itakwa vema kama jimbo hili litabaki chini ya ccm, kwa sababu mtoto wa sumari ataweza kuendeleza na kuzifanyia kazi ahadi alizoweka babake. Goodluck kwa sioi
Huo ni uongozi wa kifalme ambao unapingwa katika dunia ya leo, sasa inatia shaka kama Tz inayofikiriwa kuwa ni nchi yenye demokrasia watu wanarithishana uongozi eti atekeleze ahadi za baba yake. Labda kama Wameru bado wako katika zama za ujima watamchagua. Hakuna familia ambayo ina lease ya kuongoza na kufaidi keki ya uhuru. Tunachotaka ni mtu mwenye uwezo wa kusimamia maendeleo katika Jimbo la Arumeru Mashariki.
 
Kwa kuanzia mteule wa CDM, Joshua Nassari, siku NEC itakapotangaza Siyoi Sumari ni Mgombea kupitia CCM, Joshua apinge uhalali wa uteuzi huo, kutokana na uteuzi kugubikwa na RUSHWA.

Nape Nnauye alipotangaza kwa waandishi wa habari kuwa Siyoi Sumari ndiye mteule wa CCM, alikiri kuwa uteuzi huo uligubikwa na rushwa. Hapa Arusha tunajua kuwa TAKUKURU imewatia mbaroni vijana wawili, wasaidizi wa Edward Lowassa kutokana na tuhuma za kutoa rushwa kwa wajumbe waliomchagua Siyoi Sumari. Imeelezwa kwamba simu za mkononi za hao vijana zilikutwa na sms nyingi zikiahidi wajumbe wa mkutano fedha.

Huu ni ushahidi tosha kwamba rushwa imetumika. CHADEMA lazima wakumbuke Uchaguzi Mkuu wa 2010 Mbeya Vijijini, ambapo Shitambala mgombea wetu alienguliwa kutokana na CCM kudai hakuapa kiapo mbele ya Magistrate.

National Electoral Commission wakiwa na Mheshimiwa Jaji Lubuva kama Chairman mpya, lazima wakubali kuwa allegations za rushwa ni sababu tosha kumwengua Mgombea Ubunge. NEC iwashirikishe TAKUKURU iwaletee huo ushahidi.
 
Mkuu hao vijana wapo wangapi? Wewe ndio wamekutuma uje uwasemee humu JF? kwa nini usipeleke malalamiko yao pale Lumumba.

Wewe nawe ni fisadi aliyekubuhu.Pole,maskini mliowadhulumu watawalilia mpaka makaburini mwao.
 
Chadema kueni makini sana na ayo maneno ya sita,nimnafiki.alishindwa kuliokoa taifa leo ata 2ambia nini!!hana jipya.
 
Halafu magamba wanamteua Benjamin Mkapa kufungua na kufunga mikutano ya kampeni.


Anahusika sana katika uovu, hasa katika kuruhusu ufisadi wa EPA, Deep Green, Radar, kuuza nyumba za serikali na mengineyo, na i bila shaka alifaidika na fisidi hizo dhidi ya wananchi wa Tanzania

Aidha Mkapa alijimilikisha mgodi wa makaa ya awe wa Kiwira. Kumteua fisadi huyo kufungua na kufunga kampeni ni tusi kwa wakazi wa Arumeru.

Ushauri kwa CDM ni kwamba siku ya kufungua kampeni yao iwe baada ya ufunguzi wa CCm, ili waweze kumchanachana live Mkapa na ufisadi wake.

 
i think you have a point brother. Hapa ni kweli yabidi kuwepo umakini wa hali ya juu kwa kuwa hapa sio ccm ya kawaida inapambana na cdm, ni ccm-l yenye nguvu kuliko ccm-k

naunga mkono hoja asilimia mia kwa 100 hapa ni luwasa
ila waswahili wanasema asiye sikia la mkuu?????? Tumesha sikia ya wakuu mengi kuhusu maisha mabaya yanayoletwa na ccm kama tusipobadilika ....tutavunjika guu!!! Tusisahau louasa alingatuka kwa kashfa!!1 mwisho wa kunukuu
 
Back
Top Bottom