DALLAI LAMA
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 8,651
- 2,627
Democratic, kama unadhani huo ndio ukweli, umenoa!. Ila pia nimegundua ni wanabodi wachache sana huwa wanaukubali ukweli halisi!, wengi zaidi huogopa ukweli halisi na badala yake kung'ang'ania ukweli wa kujifariji nafsi zao kwa kujipa matumaini ya uwongo na mwisho wa siku huishia kulia lia tuu!.
Baada ya kupitishwa Sioi, uchaguzi Arumeru ndio umemalizika!. Kinachoendelea sasa ni kwa NEC kukamilisha tuu taratibu kukidhi matakwa ya kidemokrasia kusubiria kumtangaza rasmi!.
Wenye akili wataisoma hii post na kujinyamazia kusubiria April 2!. Ving'ang'anizi wa maubishi mtaanza kubisha na kuendelea kujifariji kuwa mtu yule yule toka chama kile kile aliyeshindwa na mahututi kitandani, sasa anaweza kushindana na mwana mfalme wa mtu yule yule aliyewashinda mwanzo na akashinda!.
Wengi wanategemea zaidi kura za chuki za wana CCM dhidi ya siasa za uchifu, usultani na ufalme za CCM kwa mtoto kumrithi baba yake bila kutambua asili ya Wameru ni ufalme wa koo fulani fulani!. Jerry alikuwa ni mfalme wao na Sioi ndiye mwana mfalume!.
Kwa wapenzi wa demokrasia ya kweli mtanisamehe sana kwa kuwadondolea ukweli mchungu!. Ili kuupata ukombozi wa kweli, lazima tukubali kukimeza "the bitter pill"- Sioi ndiye Mbunge Mteule wa Arumeru akisubiri kuapishwa!.
Pasco (wa jf).
pasco nlikuwa nakuheshim ila sasa nakufananisha na lyatonga,huna lolote.huitendei haki democracy