ARUMERU: Kutokana na mambo kuwa magumu Green Guard waanza mazoezi

Tunashukuru kwa taarifa , tutashirikiana panapobidi mpaka kieleweke! Sisi tuna Mungu kamanda!

Nilibahatika kuwaona hao green guard kwenye msiba wa yule diwani wa sijui ungaltd, Msangi(RIP) yaani wamejichokea, wamevaa viatu vimepinda, havina hata kiwi, afya zao zinatia huruma! Hawana jipya kiukweli ni vijana waliochoshwa na maisha wakajipeleka CCM wakatumiwe na wala nchi, mie mwanzoni niliposikia green guard nikajua ni watu haswa kumbe vijitu havina mbele wala nyuma... Hawana jipya!

Kwa hali ilivyo kwa sasa unadhani ni mtu gani mwenye akili timamu atakubali kuitumikia ccm? Wamebakia wajinga wachache wanaoikumbatia ccm ndn maana elimu hawaiwekei kipao mbele kwani wanajua kuamka kwa wananchi ndiko kutaing'oa madarakani
 
Ni kweli unachosema mkuu! Wanajisumbua bure tu hawa magamba! Afu sijui wanafanyishwa mazoezi ya nini manake wako choka mbaya kabisa, wanatumika zaidi kipindi cha kampeni na kwenye misiba ya viongozi wa chama chao, huwa wanafanyishwa kazi za kudhalilisha sana kwa mwanaume mwenye akili timamu hawezi kukubali kuzifanya! Yaani wana maisha duni sana, sijui wanalishwaga nini mpaka hawazinduki! Kampeni ikimalizika wanabaki kwenye ofisi za kata kuganga njaa!

Ha ha haa vifo na kampeni ndo pona yao, basi wapole kwa hilo
 
Yote ya hayo tuwaachie kazi wana Arumeru kazi ya kuikataa ccm na magamba yake kwa nguvu zote
 
Huyu Crashwise alikuwa akiandika ***** kama huu wakati wa uchaguzi wa Igunga. Anaonekana ni mtaalam wa kutunga story za kijinga ili asifiwe na magwanda. Hana ushahidi wa ****** alioweka hapa. Tumezoea usanii wako.

Maumivu ya kichwa huanza pole pole, mwisho mtu uropoka kama wewe.

Kama hana ushaidi wowote aliouweka, basi tunaomba utuwekee wewe
 
Ccm wameweka kambi ya kuwafundisha green guard eneo la Leganga barabara ya kwenda Dik dik kama unaenda dik dik mtaa wa pili kushoto huku Nchemba Mwigulu amekuwa akipita na kugawa hela lakini pia anawapa wananchi contact namba za simu za viongozi wa chadema wa kitaifa ili kuwahadaa wananchi kuwa yeye na Mbowe, Dr Slaa na n.k ni marafiki sana hivyo hakuna haja ya wananchi kuwakataa kuongea nao..

pia ametoa mil 10 atakae fanikiwa kumdhamini mgombea wa CHADEMA huku akiwa amemdhamini wa chama kigine kitu ambacho kitapelekea kukatiwa rufaa na kuondolewa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea jimbo la Arumeru Mashariki....

Ninavyowajua watu wa ARUSHA CCM wanajisumbua tu na Green Guard yao, hakuna wa kupigwa na hao watoto wa shule. Na waombe Mungu watu wa mererani wasipandishe monkari, huyo Mwingulu atakimbia kama baba yake alivyokimbia jeshini na kupasua mbuga na kibegi chake. Vijana kuleni pesa yao kwa sana lakini hukumu wataiona kwenye sanduku la kura.
 
Ha ha haa vifo na kampeni ndo pona yao, basi wapole kwa hilo
Yes mkuu, akifa kiongozi wanapelekwa kupasua kuni, kupanga na kufuta viti, kuonya masufuria, kushusha hema na vyakula, kugawa maji na kuokota chupa za maji wakauze, n.k then mwisho wa siku wanalipwa elfu 5!... Kama hakuna kampeni wala kifo hawana kazi ya kufanya!
 
Kwa hali ilivyo kwa sasa unadhani ni mtu gani mwenye akili timamu atakubali kuitumikia ccm? Wamebakia wajinga wachache wanaoikumbatia ccm ndn maana elimu hawaiwekei kipao mbele kwani wanajua kuamka kwa wananchi ndiko kutaing'oa madarakani
Naamini hakuna! Unachosema ni kweli wamewakamata wale wajinga wajinga wote, hakuna mwenye akili timamu kati yao!... Mimi kuna wamama nawafahamu wao na CCM ni damu damu nadhani walikunywa maji ya bendera, cha kushangaza na kusikitisha ni kwamba wana maisha magumu, wanashindwa hata kusomesha watoto, ukijaribu kuwaelimisha kuhusu mabadiliko nakuapia utalia, wana ufahamu duni ! Sasa CCM watu kama hao ndio wanawapenda manake wajinga ndio waliwao!
 
Katika sehemu zote kuelekea uchaguzi,sehemu muhimu mno ni ujazaji wa fomu za kugombea ipasavyo.Fomu zijazwe na wahusika kisheria na wasiwe mamluki.Kinyume na hapo,Nassari ataenguliwa kwa pingamizi la awali.CHADEMA kaeni chonjo huko...
 
Kwa taarifa hii...nikuwa ma.ga.mba katika kutathimini kwao wamegundua hawatoki Arumeru Mashariki....ukiacha suala la rushwa.....kufikiria mbinu ya kumuwekea mtego mgombea wa CHADEMA ili waje wamuondoe kupitia pingamizi ni ishara kuu ya anguko la CCM jimboni humo....Kwanini waogope kuchuana na CDM wao ni chama makini kama wanavyojinadi siku zote?
 
Kwa taarifa hii...nikuwa ma.ga.mba katika kutathimini kwao wamegundua hawatoki Arumeru Mashariki....ukiacha suala la rushwa.....kufikiria mbinu ya kumuwekea mtego mgombea wa CHADEMA ili waje wamuondoe kupitia pingamizi ni ishara kuu ya anguko la CCM jimboni humo....Kwanini waogope kuchuana na CDM wao ni chama makini kama wanavyojinadi siku zote?

Nafikiri umakini unahitajika katika kukamilisha mtiririko wa fomu na kanuni zote ili kujiepusha na mitego kama hii.
 
arusha atutakaa kimya hira zao wazifanye kwa ungalifu sana maana tukimuweka kwenye 18 mmoja wao atakuawa mfano ama akutwe akitumia mali za serikali kwenye kampeni ama aikitoa rushwa maana tuna jua takukuru hawana msaada kwetu....

hakuna kama arusha, lete ujinga watu wakugeuze rangi nyekundu,
 
Back
Top Bottom