Arumeru hali si shwari mabomu ya machozi yatumika kusambaratisha watu.

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,064
10,723
Wananchi wa Jimbo la Arumeru waishio pembezoni mwa eneo la Dolly (eneo ambalo wazungu wamemilikishwa)kuanzia jana jioni wameandamana kuelekea eneo hilo na kuanza kungoa fensi inayozunguka eneo hilo.Na hali ilizidi kuwa mbaya pale polisi wa kutuliza ghasia walipo fika eneo lile bila hata kuwauliza wananchi nini hoja yao wakaanza kuwarushia mabomu ya machozi wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo na hapo ndipo na wananchi wakaanza kuwajibu kwa mawe maaskari wale hali iliyopelekea idadi ya maaskari kuongezeka na wananchi nao kuongezeka.

Na hoja au madai ya wananchi wa eneo lile kwanza kabisa wanataka barabara iliyokuwa ikitumika kuunganisha kijiji cha MAJI YA CHAI na Maroroni iliyofungwa baada ya hao wazungu kuchukua eneo hilo ifunguliwe kwani imekuwa ikiwalazima kuzunguka mbali sana baada ya barabara hiyo kufungwa.

2.Kulikuwa na shule ya msingi ndani ya eneo hilo wazungu walio milikishwa ambapo baada ya wazungu kuchukua eneo hilo na kulifensi shule iliamishwa na kupelekwa eneo ambalo ni mbali na makazi hivyo kuwasababishia usumbufu watoto.

3.Wanadai baada ya muafaka wa barabara na shule kupatikana watataka sasa wajue nini muafaka hiyo ardhi iliyomilikishwa kwa mzungu mmoja huku wananchi wa eneo husika wakiteseka kwa kukosa ardhi.

4.Wanasema huu ndiyo wakati muafaka wa wao kudai haki yao ya msingi na kufanya hivyo ni kumkumbusha Mheshiwa Nassary kuanza kufanyia kazi ahadi alizozitoa kwenye kampeni kubwa likiwa ni hili swala la ardhi kubwa kumilikiwa na watu wachache.Na wanamatumaini huu sasa ndio wakati wao wa kukomboa ardhi zao umefika.

Nipo maeneo ya hapa nitajitahidi niane kama naweza nikawaletea na picha ili mueze kuona huu umati wa wananchi ulivyumkubwa hapa.
 
Si wamsubiri mbunge wao alifanyie kazi kidiplomasia!
 
CCM na Poli-CCM wasije wakaanza kusema kuwa na mbunge ndiye aliyewaambia wafanye hivyo. Nassari wewe bado ni kijina, nakushauri usije ukaingizwa kichwa kichwa katika mambo kama hayo. Najua haki ya wananchi kusikilizwa ipo lakini isitafsiriwe kuwa hawakufuata sheria. Jambo kama hilo linaweza kuchochewa na CCM kwa kutumia 'system' yake ili kuonesha kuwa CDM wanawaongoza watu kuleta vurugu.
 
Si wamsubiri mbunge wao alifanyie kazi kidiplomasia!

In this country of ours, you don't get what you deserve; you get what you fight for. Wamsubiri nasari waone kama hawajasubiri mpk Dec 31 2099. Toa macho tu hapo na diplomasia zako, UTAFRAI CHALII.
 
apa ailikuwa tayari amekwisha wahakikishia kubatilisha hati miliki za hao wazungu kwani yeye angetumia mbinu gani? Mi nausifia huu ubunifu wa wananchi wa Arumeru wa kudai haki yao bila kusubiri serikali iliyolala usingizi na isiyo sikivu kabisa. Ukiona serikali inajidai tu kujua matatizo ya wananchi wakati wa kampeni ujue ni ya kitapeli.
 
itafika mahali tutakubaliana tuu!
na tutakubaliana kutokukubaliana au kukubaliana
 
Mabadiliko yasipopatikana ndani ya ccm yatapatikana nje ya ccm

Kama hawaoni watalazimishwa kuona
 
kwa Wadau tu, hivi inakuwaje Mzungu toka ulaya, america au kwingineko apewe ardhi ktk maeneo ambayo tayari wazawa wana tatizo la ardhi. Hivi tuko tayari kuua raia wetu kwa ajili ya wakoloni kweli jamani. tufike mahali tuone aibu na kuwapendelea WATZ
 
Hatudanganyiki tutachukua mashamba kila mzungu plus mafisadi wana kwao na wana mama zao waende wakawafisadie.
 
Wenye shida ya kulima ni wananchi walio wengi hapo Arumeru, sasa kwa kuwa ardhi ya NCHI YAO WENYEWE ipo na wanaiona mchana kweupe, kwa miezi, kwa miaka ipo kwenye mikono wa WAKUJA mmoja au wengi walioamua kuweka uzio ili kujitofautisha na wazawa wanaonyanyasika kwenye nchi yao.
Nawaunga mkono Wananchi makini kwenda pale na kung'oa uzio, ikibidi leo waanze kilimo kwa ajili ya FAMILIA ZAO na kwa ajili ya kuuza kupata pato, polisi sina haja ya kuwalaumu maana si ajabu wapo watoto wa Arumeru wanawadhulu wazazi wao kwa kutii amri ya mkuu.
Hakuna muda mwingine zaidi ya hatua hii ya wananchi waliyochukua, miaka hamsini ya uhuru wameteseka sana na ardhi, wamelazimishwa wahamie Tanga na maeneo mengine kuwapisha WAKUJA, kwa nini WAKUJA wasipelekwe huko ili wazawa wabaki kwenye eneo la MABABU ZAO. Mkisubiri kuomba kuna miaka 99, chukua majembe, maksai, trekta na powertilla lima
 
Back
Top Bottom