Belo
JF-Expert Member
- Jun 11, 2007
- 12,882
- 10,193
Papa Mapao,VoiceOfReason kwa kuongezea, asilimia kubwa ya wachezaji walioondoka Man U ukiondoa kiwango cha mpira, wengi waliondoka sababu ya Personal issues, nakubaliana na wewe khs hili,we kumbuka kile kitendo cha Sir Alex kumpiga kiatu usoni mwa David Beckam mpaka akamchana ngozi,hicho kitamfanya Beckam aendelee kubaki Man U under Sir Alex,mpaka aondoke SAF Beckam nina hakika atarudi Man U, Jaap Stam naye alikumbwa na upepo wa Ferguson bila kutarajia na ndo maana alimpaka huyo manager huku tayari alishaondoka pamoja na kwamba Stam ni beki mzuri sijui kama amestaafu, kwa Wenger sijaona bifu na wachezaji wake, ni kocha anayeweza kuishi na kila mchezaji, wachezaji wote walioondoka hakuna hata mmoja aliyempaka Wenger, nakubaliana na VoiceOfReason kwamba Wenger ni kocha mbunifu management ya soka kwa upande wa wachezaji! Wenger anapokuwa katika kipindi kigumu mara nyingi hutumia busara zake kuwatuliza wachezaji, lkn Ferguson wakati mwingine hasira zae utaziona waziwazi mpaka unaogopa! Cristiano nadhan alikimbia sababu hiyo!
SAF ni binadamu kama wewe so kugombana na watu ni kitu cha kawaida,Guardiola alisema kabisa hawataki Etoo na Ronaldinho hata Yaya Toure but kitu cha msingi ni jinsi ya kuziba pengo la huyo mchezaji,wote wameondoka bbut hamna pengo lao,Mancini amegombana na Belamy,Tevez,Adebayor.Mourinho aligombana na Baloteli,Roben but still timu inafanya vizuri
Issue ya Beckham alipigwa na kiatu bahati mbaya ,nakumbuka ilikuwa game against Liverpool timu ilionyesha kiwango kibovu SAF akawa anawafokea wachezaji na akapiga kiatu kikaenda kumpata Becks na baada ya kuondoka Becks SAF alimleta Ronaldo ambae alikuwa bora kuliko Becks mimi namchagua CR7 dhidi ya Becks.
Stam alitunga kitabu ambacho kilikuwa kinampiga madongo jinsi SAF alivyomsajili kutoka Holland sidhani kama kuna kocha angependela hicho kitu na kuondoka kwa Stam SAF alikuja kumleta RIO ambae ametengeza ukuta hapo ManU hadi sasa.Na baada ya kustaafu soka STAM anafanya kazi ya uskauti wa Manchester United katika bara la America ya Kusini
Hata suala la CR7 liko wazi kuwa yeye mwenyewe alitaka kuondoka na kupata changamoto nyingine na Madrid walikuja na offer ambayo huwezi kukataa na still unasema sababu ya kuondoka na SAF .Ukumbuke baada wa World Cup 2006 kule Ujerumani baada ya CR7 kusababisha Rooney apewe red card ,Waingereza walianza kumuandama CR7 na SAF alisimama kidedea kumtetea