Arobaini/matanga ya kamanda regia yawa funzo kwa wanasiasa wa leo...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
WANASIASA na viongozi wa kuchaguliwa wameshauriwa kuwa na mahusiano mazuri na Mungu ili awape mvuto wa kukubalika mbele za watu na kutimiza malengo ya waliowachagua.

Mwito huo umetolewa na baba mzazi wa aliyekuwa Mbunge Viti Maalumu, Regia Mtema (Chadema), Estelaus Mtema alipokuwa akizungumza na gazeti hili jana mara baada ya misa ya shukrani kufuatia kifo cha Mbunge huyo.

Misa hiyo ilifanyika nyumbani kwao Ifakara. Regia alifariki papo hapo kwa ajali ya gari Januari 14, mwaka huu eneo la Ruvu, Pwani, baada ya gari lake kupinduka mara kadhaa akikwepa lori.

Alisema wanasiasa wengi na viongozi wa kijamii wanakosa kukubalika na watu na kubaki kuwa wabinafsi kwa kuwa wanakosa kumtegemea Mungu katika utendaji wao badala yake wanatumia nguvu nyingi za kimwili ikiwamo ushirikina.

Akitolea mfano wa binti yake Regia, Estelaus alisema: "Sizungumzi hili kwa kuwa alikuwa mwanangu, lakini sisi wenyewe tulishangaa alivyokuwa na mvuto wa pekee kwa watu, alimtegemea Mungu tangu mdogo alikuwa akitembea kwa miguu umbali mrefu bila kujali ulemavu wake kwenda kufundisha vijana wenzake neno la Mungu kabla ya kuingia katika siasa."

Aliongeza, "alipenda kutumikia watu, amesaidia wengi kwa mfano kuna albino hapa amempangia chumba hapa Ifakara baada ya kukutana naye na kumweleza kuwa yuko katika hatari ya kuuawa, kuna wanawake zaidi ya watatu ambao tumewashuhudia walitekelezwa wao na watoto wao na wanaume zao, Regia amewapangia nyumba.

Estelaus alisema kati ya fedha ambazo Regia alikuwa akizipata kutokana na ubunge aliweza kuzigawa na kubakia na robo ya fedha, hali ambayo ilifanya watofautiane na pacha wake Remegia kutokana na namna alivyopitiliza kusaidia watu hasa wahitaji.

Remejia alithibitisha kutofautiana kwao. Awali katika misa, iliyoongozwa na Padri, Ludwick Mdengeri katika mahubiri yake aliitaka familia isivunjike moyo wala kukata tamaa kutokana na tukio hilo, kama walivyoamua kufanya shukrani hiyo waendelee kushukuru Mungu daima.
 
R.i.p Reggy,tunaendeleza fikra na mapambano yako ktk mkoa wetu wa Morogoro na Tanzania yetu kwa ujumla,tutakukumbuka daima Regia
 
She was born a leader and a true woman of the people! REST IN PEACE GENDER SENSITIVE.
 
R.I.P the late hon. Regia, a popular leader of her generation.
 
Dah! nimemkumbuka Regia baada ya kusoma hii post.
R.I.P kamanda Regia Mtema, tunakupenda kiongozi wetu.
Hakuna kulala mpaka kinaeleweka.
 
Back
Top Bottom