Armed robbers raid Mwadui diamond

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
KUna wakati mgodi wa Mwadui ulielezwa kwamba haukua ukiilipa serikali mgawo kutokana na hisa zake.. Sasa sina hakika kama wameanza kulipa na kinachofanyika sasa ni HUJUMA ili mgodi uonekana unapata hasara na wasiendelee kulipa huo mgawo. WAKATI WOWOTE (KUANZIA SASA) tutasikia matukio ya kutisha huko MWADUI
 
TUJIKUMBUSJHE Pia kuhusu Tansort ya London ambayo ni 100% ya Serikali ya Tanzania lakini fedha zake zinashikiliwa na kampuni ya Afrika Kusini inayomiliki Mgodi wa Mwadui
 
Jamani nchi yangu Tanzania kuna nini? Nyuma tu kidogo ya fensi ya mgodi wananchi wako ktk ulimwengu miaka ya 1000 B.C.

Mungu tuhurumie kosa tulilotenda tusaidie

Watanzania lililobakia ni kumwomba Mungu pekee

Tumezidiwa nguvu na shetani(mafisadi, wanyonyaji, walarushwa, wazinzi, waongo n.k)
 
Kwa walio Tanzania mhusika tutakutana nae usiku huu baada ya mimi kutoka kazini, yaani baada ya saa 3 usiku saa za Tanzania
 
Anasema hawezi kuzungumza kwa simu.... anatweta analilia Tanzania yake, anasema "Tanzania haipaswi kuwa masikini milele"
 
Halisi, nadhani hakuna kitu kitakachowauma sana wa Bongo kama Mwadui. Miaka ile kuna mtu aliandika hadithi kuhusu Mwadui na watu wengi tulipenda wazo zima la mgodi huo. Lakini hayo unayoyasema Buzwagi itaonekana mtoto..
 
Nchi yetu bila uhuni wa wachache nadhani ingekuwa tayari na ingeweza kumudu system ya income support, job seekers allowance na hata child benefit... mapato ya taifa yanayopotea kwa wizi ni mengi mno kwa kweli, na hizi habari zinazojitokeza kila leo sidhani kama za uongo..

SteveD.
 
Katika yote haya, blunder baada blunder, plunder baada ya plunder, haya sisi wananchi tuchukue hatua gani? It is easy to create a problem, can we also create solutions? samahani hii hoja yangu inajirudia mara kwa mara kwa sababu nami nahangaika kutafuta majibu. Kila nikitaka ku-create solution najikuta nime-create problem!

Je, tuandamane tukawafukuze hawa jamaa kwenye migodi yetu, yaani tufanye beyond these complains-all parts of my body are trembling!
 
Kitila, kwa kweli saa nyingine mtu unashikwa na hasira mpaka unashindwa hata kuongea, kila ukisikia tetesi fulani hivi ukizichambua kidogo tu unapata mwangaza na kuona jinsi nchi yetu ilivyo na inavyo haribiwa na wachache... tusifikie kupigana vita wenyewe kwa wenyewe, namwomba Mola. Lakini kwa haya yanayozidi kufichuka bila masuluhisho, wasitahamaki hawa wachache kujikuta wanaandamwa kizazi kimoja baada ya kingine. Wanafyonza kila kitu mali yetu sote na kujisahau kuwa dunia hubadilika, warithi wao nao tutawasakama hivyo hivyo... wanajisahu kuwa faragha kwao leo, kesho kwetu. Serikali zijazo Tanzania yetu hazitatabirika...na kama hali ndiyo hii basi utaifishaji tuuruhusu urudi!!

SteveD.
 
Katika yote haya, blunder baada blunder, plunder baada ya plunder, haya sisi wananchi tuchukue hatua gani? It is easy to create a problem, can we also create solutions? samahani hii hoja yangu inajirudia mara kwa mara kwa sababu nami nahangaika kutafuta majibu. Kila nikitaka ku-create solution najikuta nime-create problem!

Je, tuandamane tukawafukuze hawa jamaa kwenye migodi yetu, yaani tufanye beyond these complains-all parts of my body are trembling!

Mzee Kitila mambo ya kufanya wala siyo makubwa kama watu wanavyofikiria.

Binafsi naamini kuna njia kubwa mbili. Ya kwanza ni ngumu inayowezekana na ya pili ni ngumu zaidi iliyo nje ya vitu vinavyowezekana kwa sasa.

Ngumu inayowezekana:
- Kuhakikisha kuwa Bunge la Tanzania linaondolowa wingi wa wabunge wa CCM na hivyo kulifanya liwe na nguvu kidogo ambapo mijadala yote itahitaji compromise na accomodation. Na bunge bilo ambalo litakuwa la chama tofauti na kile anachotoka Rais litalazimisha kutungwa sheria za usimamizi na ulinzi; litatengeneza checks and balances na kumtumia Rais miswada hiyo ili aikubali.

- Mojawapo ya sheria ambazo Bunge hilo litatunga ni zile zinazokataza viongozi, zinazosimamia viongozi, na zinazolazimisha viongozi. Kwa mfano, sheria inayohusu Mgongano wa kimaslahi. n.k n.k

Ngumu zaidi:
- Ni kuweza kuwashawishi wabunge wa chama tawala kufanya hilo hapo juu na kwenda kinyume na Rais au kinyume na chama chao.

-
 
Ngumu zaidi:
- Ni kuweza kuwashawishi wabunge wa chama tawala kufanya hilo hapo juu na kwenda kinyume na Rais au kinyume na chama chao.

Mzee hii ni ngumu kweli. Inamaana hata shati la kijani alichukie mmmm. noma.
Lakini siku zinahesabika kwa wale waonao mbali.

Ngoma ikilia sana mwisho?.......Ameingia kwa kishindo lakini tawi la kutoka kwa kuzomewa amelikalia...

Tutegemee makuu hapo mbele kidogo tu ya safari yetu. Ni huzuni lakini hayana budi kutokea...
 
Mzee Kitila mambo ya kufanya wala siyo makubwa kama watu wanavyofikiria.

Binafsi naamini kuna njia kubwa mbili. Ya kwanza ni ngumu inayowezekana na ya pili ni ngumu zaidi iliyo nje ya vitu vinavyowezekana kwa sasa.

Ngumu inayowezekana:
- Kuhakikisha kuwa Bunge la Tanzania linaondolowa wingi wa wabunge wa CCM na hivyo kulifanya liwe na nguvu kidogo ambapo mijadala yote itahitaji compromise na accomodation. Na bunge bilo ambalo litakuwa la chama tofauti na kile anachotoka Rais litalazimisha kutungwa sheria za usimamizi na ulinzi; litatengeneza checks and balances na kumtumia Rais miswada hiyo ili aikubali.

-

Great, sasa maanake ni kwamba kuanzia sasa hivi, pamoja na mambo mengine tuelekeze juhudi zetu katika kuhakikisha kwamba upinzani unapata viti vingi bungeni katika uchaguzi ujao. Tunaweza kufanya mambo matatu: i) ku-identify miongoni mwetu na kwingineko wenye sifa na tunafikiri wanafaa kuwa wabunge na kuwashawishi wagombee kupitia upinzani ii) kuwasaidia financially kwa kuanzisha kuamfuko kwa ajili hiyo maana najua kugombea ubunge ni money eating business na inawezekana kuna watu watakuwa na sifa tele lakini wakakwama financially, lakini hawa tunawachangia kwa sharti moja kwamba hela zetu hawatazitumia kwa ajili takrima-sisi hatutaki kuwa sehemu ya kubariki uchafu! iii) kuwashawishi na kuwaelimisha wapiga kura juu ya umuhimu wa kuchagua wabunge wengi wa upinzani-kwa njia ya maandishi (makala, posters, etc), mikutano, vijeweni, kampeni za mtu kwa mtu (lakini sio kitanda kwa kitanda), n.k.

Hiyo vipi?
 
mzee, kama watu wako serious tuzungumze tuwaanzishie kampeni fulani fulani... wengine mambo haya ya kampeni ndiyo kazi zetu...
 
Nashangaa wabunge wako Dodoma lakini wanachokifanya hakijulikani, yaani wapo pale kwa ajili ya allowance tu na hawajishughulishi na matatizo ya wananchi. Hii ni hatari kubwa wataamka siku moja na kujikuta wako Keko.
 
Nashangaa wabunge wako Dodoma lakini wanachokifanya hakijulikani, yaani wapo pale kwa ajili ya allowance tu na hawajishughulishi na matatizo ya wananchi. Hii ni hatari kubwa wataamka siku moja na kujikuta wako Keko.

Ndio sasa tunasema, ok, inawezekana hao wana matatizo kweli je, sisi tutashirikije kuhakikisha kwamba tunakuwa na bunge zuri? Je, inawezekana kuna wenzetu watanzania tunaowajua na tunafikiri wana uwezo na tunaweza kuwashawishi na kuwawezesha wagombee? Hii sasa ndio issue. In other words, what we are saying is that,yes, we may not be part of the problem, but can we be part of the solution?
 
mzee, kama watu wako serious tuzungumze tuwaanzishie kampeni fulani fulani... wengine mambo haya ya kampeni ndiyo kazi zetu...


Mzee: Hili jambo lazima tulichukulie serious if we are serious na matatizo tunayoyajadili hapa katika forum. Lazima tuamue kwa dhati kabisa kwamba na sisi tunataka ku-solve problem fulani na tuone mwisho wake, mpaka kieleweke. Inawezekana tukiamua!
 
"WATU WASIOJULIKANA" wamevamia almasi wa Mwadui unaomilikiwa kwa ubia kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya Williamson Diamond Limited, na kufanikiwa kupora almasi na silaha moja waliyoipora kwa mlinzi wa mgodi huo.

Thamani halisi ya almasi iliyoporwa haijafahamika pamoja na taarifa ambazo zimepingwa na wafanyakazi na wanaoufahgamu mgodi huo kwamba almasi zilizoporwa ni karati sizizozidi hamisini tu (50 carate).

Tukio hilo limetokea saa nane usiku (0200hrs)saa za Afrika Mashariki usiku wa kuamkia leo (Alhamisi).

Watu hao walipovamia mgodi huo walikwenda moja kwa moja eneo ambalo upo mkanda unaosafirisha mchanga wa almasi kutoka katika mgodi kwenda katika chumba cha kuchambulia (sorting) na kuchukua mchanga huo kisha kuchukua greda la kijiko na kubomoa eneo la kuchambulia almasi na kuchukua zote zilizokuwapo hapo.

Habari zinasema kwamba silaha aliyoporwa mlinzi wa mgodi imepatikana katika mabonde ya vijiji vinavyozunguka mgodi huo. Hakuna taarifa zozote za kukamatwa kwa wahusika wa uporaji huo.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Shaibu Ibrahim, na wenzake walikuwapo eneo la tukio leo asubuhi lakini taarifa zinasema hakuna mwandishi wa habari aliyeruhusiwa kwenda eneo hilo na hakutolewa taarifa zozote za polisi wala uongozi wa mgodi, labda kesho Ijumaa.

Aliyenisimulia tukio hili alikuwapo eneo hilo leo asubuhi na anashangaa sana inakuaje tukio kama hilo litokee.

Hoja yake ni kwamba upo uwezekano mkubwa wa HUJUMA ZA NDANI YA MGODI ZINAZOFANYWA ili kupunguza faisa inayotokana na mgodi husika.

Serikali inamiliki asilimia 25 ya hisa katika mgodi huo. Nakumbuka Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) chini ya Hamad Rashid wa CUF iliwahi kufanya uchunguzi na kubaini kwamba serikali haijawahi kupata mgawo wa faida tokea kukabidhiwa kwa mgodi huo kwa kampuni ya De Beers na wabunge walisema kama hawapati faida mbona hawaondoki? Ndipo sasa ikaanza kuelezwa kwamba kuanzia miaka miwili ama mitatu iliyopita ndio wameanza kupata faida sasa kama utatokea wizi ama uharibifu ama hasara, itabidi serikali ya Tanzania nayo iingie hasara.

PAC pia ilibaini kuwapo kwa uzembe ama ujinga mkubwa na serikali kukiri kwamba fedha zote zinazolipwa na De Beers kwa serikali kwa kazi ya kuchambua almasi zake katika kampuni ya Tansort iliyoko London zilikua zinahifadhiwa katika kampuni ya De Beers. Tansort ni kampuni ya serikali kwa asilimia 100. Kampuni hiyo ilikua haijawahi kukaguliwa kwa miaka yote tokea ianzishwe na mwakilishi wa CAG aliyekwenda London kukagua alizuiwa, hata PAC walikosa ushirikiano wa kutosha kabla ya kurudi na kupiga kelele.

Makusanyo ya Tansort yalikua hayaingizwi Hazina na haijulikani yalitumika vipi. Tansort sasa inasemekana imeanza kukaguliwa na kuingizwa katika hesabu za serikali.

Nitaomba kusahihishwa kwa baadhi ya Kumbukumbu kwa kuwa hapa naandika kutoka kichwani sina mahali pa kurejea maana aliyenisimulia angeshituka kama ningechukua notebook na kalamu. Kwa mwenye source nzuri zaidi atusaidie.
 
Back
Top Bottom