Argentina Yataifisha Visima vya Mafuta

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
BUENOS AIRES— Rais Cristina Kirchner wa Argentina hatimaye amekamilisha dhamiri yake ya kuitafisha kampuni kubwa za mafuta nchini humo, YPE ambayo mbia wake mkubwa ni Repsol ya Madrid nchini Uhispania.

Madai ya Bibi Kircner ni kwa kampuni hiyo ya Uhispania imekuwa ikijishughilisha na faida za uwekezaji kwenye soko la hisa bila ya kuwekeza katika uchimbaji mafuta, kiasi kwamba, licha ya utajiri wake wa mafuta, mwaka jana Argentina ililazimika kuagiza mafuta kutoka nje ili kukidhi mahitaji ya ndani.

Tayari kumekuwepo na maoni kadhaa ya kuunga mkono na kupinga uamuzi huo, lakini pia uamuzi huo umeshaanzisha vita vya kibiashara na pengine ugomvi wa kidiplomasia baina ya serikali za Buenos Aires na Madrid. Viongozi wa Madrid tayari wameahidi kuchukua hatua za kufaa huku wakiungwa mkono na Jumuiya ya Ulaya.

Wakati huo huo, Rais wa Mexico Felipe Calderon ameilaumu Argentina kwa uamuzi wake huo na kuuita si wa kiuwajibikaji ikizingatiwa madhara yake katika mikataba ya biashara kimataifa. Hata hivyo, kauli ya mwanzo ya Calderon ilikuwa "ukiona mwenzako ananyolewa wewe tia maji" akimaanisha kuwa Mexico ni mmoja wa wawekezaji katika visima vya mafuta vya Argentina.
Maelezo zaid hapa
 
Maamuzi magumu kuyachukua ktk ulimwengu wa Kibepari
Big up mama for the national interests
 
Legelege si yuko huko brazil, hajifunzi tu kutoka kwa wenzake?
 
Maamuzi magumu kuyachukua ktk ulimwengu wa Kibepari
Big up mama for the national interests
Na hiyo ndio sababu yake kubwa - MASLAHI YA TAIFA wakati sisi viongozi wetu wanajali maslahi ya MATUMBO [yao].
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom