Are you ready for HIV Test?

Na Maimuna Kubegeya(Mwananchi.co.tz)


UONGOZI wa shule ya msingi Philadephia iliyopo mkoani Pwani, umedaiwa kuwalazimisha wafanyakazi wake kupima ukimwi na kupeleka matokeo ya vipimo hivyo kwake.


Habari hizo, zimethibitishwa na baadhi ya wafanyakazi hao zimesema kuwa uamuzi huo umetokana na agizo maalum lililotolewa serikalini.


Wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti walisema mkuu wa shule hiyo, alitoa agizo kwa wafanyakazi wote kupima ukimwi huku akidai ni agizo serikali.


Walisema kuwa wao walikubali kutekeleza agizo hilo ili kulinda ajira zao.


?Si hivyo tu mkuu wa shule yetu alisema kuwa ni lazima tupime ukimwi kwani ni agizo ambalo limetoka serikalini,? alisema mmoja wao kwa masharti ya kutotajwa jina.


Walisema kinachowasikitisha, upimaji huo uliendeshwa kibaguzi na kwamba baadhi ya wafanyakazi raia wa Uganda hawakuhusishwa kabisa katika mpango huo.


Walisema licha ya kukubali kupima, wenzao

wamepinga kupimwa na wamesusia kwenda kupima.


Shule hiyo, ipo Mkuranga chini ya ?Tanzania Presbyterian Church? na inamilikiwa na raia wa Korea, chini ya uongozi wa mwalimu mkuu ambaye ni raia wa Uganda.


Mwananchi Jumapili ilishuhudia baadhi ya wafanyakazi hao wakiwa katika foleni ya kwenda kupima katika chumba cha Zahanati ya Zakheem Mbagala jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.


Mmoja wa wafanyakazi katika shule hiyo, alisema kupima ukimwi ni agizo la serikali.


?Unajua mama kwa Mtanzania wa kawaida suala la kupima ukimwi ni gumu sana lakini linapokuja suala la ajira, aaah ndio hivyo tena hakuna jinsi,? alisema mfanyakazi huyo.


Hata hivyo, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Chiza, alithibitisha kufanyika kwa mpango wa kupima ukimwi.


Mwalimu huyo alisema kupima ukimwi ni agizo la Wilaya ya Mkuranga na alikiri kuwepo ubaguzi katika kupima ukimwi.


?Tuliamua kuendesha zoezi hilo kwa Watanzania na kuwaacha Waganda kwa kuwa zoezi la kupima linawahusu Watanzania tu na sio watu wa mataifa mengine,? alisema mwalimu huyo.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Henry Orauya Clemens alisema sera za serikali zipo wazi kwamba hakuna mtu anayelazimishwa kupima ukimwi.


?Nikiwa kiongozi wa serikali nina hakika na haiwezekani serikali kuagiza wananchi wake kupima ukimwi kwa lazima,? alisisitiza Clemens.


Clemens alisema mikataba ya ajira ni nyenzo muhimu katika kulinda masilahi ya mwajiri na mwajiriwa hivyo wafanyakazi hao pia walitakiwa kuipitia mikataba hiyo ili kutokwenda kinyume na haki zao.


Pia Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Abdalah Kihato alikanusha kutoa agizo la kuwalazimisha wafanyakazi hao kupima ukimwi.


?Serikali inaendesha kampeni ya kuhamasisha na sio kulazimisha wananchi wake kupima ukimwi. Sifahamu kabisa na wala sijatoa agizo hilo,? alisema Kihato.


Hii ni kinyume na haki za binadamu......enhe wakishajua wanafukzua kazi au?
 
Hapa jamvini pia wanapima? mi niko tayari ila nipe majibu when I am ok; otherwise niruhusu nirudi nyumbani bila kuniambia chochote. Utatumia busara jinsi ya kunikwepa kwi kwi kwi kwi!
 
Mimi ilibidi tu nipime kwa lazima.
Hata sioni sababu ya kupima bila kushauriwa na daktari. Kama kuna ugonjwa ambao dokta anaona ni muhimu kupima HIV, then bora apime na aweze kuendela na tiba, ila mtaani tu, kwa kuhamasishwa na JK, hakukunishawishi kabisa.
Mume wangu aliumwa sana mguu, ukawa hausikii dawa hadi tukahisi labda ndio tayari. Basi akapima mimi nikagoma, ila aliniweza tu pale alipoweka stop mambo yote hadi na mimi nipime. Ilimchukua miezi kama mitatu hivi na yeye kupima mara tatu, akinishawishi, ndio na mimi nikakubali. Lakini baada ya kupima tumekuwa na raha sana na mguu umepona kabisa kwani tulikuwa negative.
binafsi mimi naona ni muhimu kupima kabla ya ndoa (kufanya mapenzi), kupata mtoto na ukishauriwa na dokta, au kama ni lazima kwa shule au ajira fulani.
otherwise ni kujitafutia presure ambazo hazina mpango.
Ukweli ni kuwa ukijijua unao kabla just hujaanza kuumwa ni vizuri kwani madawa nimeona yanawachosha sana watu walio dhaifu.
 
mahesabu unakumbuka wabunge an wao walikimbia zoezi la upimaji......

Mkuu Kana-ka Nsungu kuna cases nyingi kuwa mama ana ngoma baba hana au kinyume chake.....Kana vipi umepima?


Kabisa! The discordant couples..na hii mara nyingine imeleta matatizo sana kwenye nyumba za watu!
 
Aisee Kwa Mpangilio Huu Wa Kutumia Condom Siku Za Mwanzo Za Uboy Friend Girl Frendo, Kupima Lazima, Ikiwa Na Pamoja Na Mambo Ya 'huyu Wa Kuzugia Tu' 'namchuna Tu Huyu Mwenyewe Yupo', Aisee Bora Umekumbusha Suala Muhimu Sana.
 
kazi ipo hapo.
Je nahii kuhusu kupeleka hayo MARESULTs kwa wazungu!!!!!!!!!!!?????????????
Imbu nifahamishini imekaaje hapo?
 
Back
Top Bottom