Are you In? Oktoba 5, 2012.... SIKU YA KUWASOMEA WATOTO VITABU

Nsiande wanitesaaa lol

mimi nilipokuwa na miaka 9 nilikamatwa na kitabu kinaitwa 'kandanda kitandani' lol
we acha aisee

Vitabu vya warusi?
sio na kile cha 'Binti Chura'?

ULivisoma vya Ben R Mtobwa ?

Binti chura ni vile vya kichina vilivyotafsiriwa kiswahili

Hivi vya kirusi vililetwa nchini kwa wingi na wale ma'uncle' na ma 'aunt' zetu enzi hizo waliopata fursa ya kusoma urusi binafsi nilikuwa navyo kama viwili

Vitabu vya kiswahili vya hadithi pale mlimanicity vipo bei si mbaya sana,

Pia kama unaenda makongo kupitia ardhi ukianza ile vumbi tu after 'lami' utaona kibao cha library ya watoto kushoto

A novel idea (a bit pricey )wapo shoPpers,seacliff na steers ya mjini

Kuna hawa wauza magazeti wa posta wanauza bei maelewano ni used ila si vibaya sana
 
Last edited by a moderator:

Mtobwa nilisoma vya Joram Kiango
na Kalulu sungura anaeongea na kucheza mpira lol
 
Kongosho na Mwali

kuna kampuni ya printing ilikuwa inaitwa 'Mkuki na Nyota' i guess
walikuwa na vitabu vizuri vya kiswahili

so mkisomea watoto vitabu msisahau 'utajiri wa kiswahili'
vitabu vipo viingi
tabu ni 'specific shop' ya kuvipata

Mkuki na Nyota wapo jengo la Quality , mnaweza kuwanunulia pia watoto vitabu vya alfulela ulela series zote hapo
 
Last edited by a moderator:
Unajua kuna wakati kuna vitu viko ndani ya uwezo wetu na hatuvifanyi au tunavifanya kwa mazoea tu. Nawashauri mtakaokuwa nyumbani kusoma makala yangu ya Tanzania Daima nimeandika kwa kirefu kuhusu hili hapo kesho. Tunachotaka na kwa kweli haitaishia mara moja. I'm so tempted kuwa tukifanikiwa Ijumaa hii tufanye tena ile Tarehe 14 Oktoba 2012 kwa sababu itakuwa ni holiday na labda tunaweza kufanya zaidi kidogo.

Lets do something about it.. unajua nilikwazika sana moyoni kusikia ati kuna watoto wanaenda sekondari wakiwa hawajui kusoma na kuandika. Watu wengi walifikiria labda ni kosa la serikali au walimu... nafikiri kuna shida pia kwa wazazi jamani. Ukiondoa wazazi ambao wamepitia shule na kupenda vitabu ni wazazi wangapi huko mitaani ambao wanasoma zaidi ya magazeti ya udaku? au kusikiliza radio zaidi na kuangalia luninga.

Hili ni moja tu.. lets to it and lets continue to bring the change we want..

Kingine ni kushika fagio na kusafisha uwanja, then campaign kutotupa taka barabarani....
 
Vitabu vya kiswahili vya hadithi pale mlimanicity vipo bei si mbaya sana,

Baada ya kuandika "Majeruhi wa Mapenzi" shida kubwa imekuwa kwenye kuweza kuviweka kwenye maduka ya kawaida. Fikiria baadhi ya hayo maduka mnayotaka wanataka wakate 30% ya bei. Hawakuchangia chochote katika kuandika kitabu au kutengeneza lakini wanataka 30% ya mapato kwa kuweka dirishani mwao! Mtunzi wa kawaida atafanyaje ili aweze na yeye kutengeneza kidogo; kuweka bei ya juu! sijui kama mtindo wao wa sasa unahamasisha watu kuandika vitabu at all.
 
Nsiande, umeona ee
hii idea inashawishi sana aisee

ingekuwa sio kulinda kutotambulika, watakaoweza fanya wangeweka picha hapa ili kuwashawishi wengine kufanya kitu zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Mwanzo mugumu ila tutafika maana watanzania wengi ni wazee wa AUDIO-VISUAL hatupendi kusoma vitu kushughulisha akili kwa kutafakari kiundani

Ndilo tunalopaswa kubadili hili kwa kadiri tunavyoweza ili hawa "Watanzania wengi" wapungue kwa kweli.
 
mwalimu, tatizo ni wapi pa kupata hivyo vitabu? Mwanakijiji aliandika kitabu cha kiswahili hapa, sijui hata kama kimeuzika manake aliweka post ya kukitangaza akarushiwa mawe. Watanzania wachache sana wanaandika vitabu kwa sababu ya gharama za uchapaji na usambazaji kuwa juu, lakini pia kwa sababu walengwa hawako tayari kununua kwa bei ya sokoni.

Gharama za kuchapa na kuchapisha vitabu kuwa juu mno, isiwe ndio sababu ya kila kitabu kitakachoandikwa kwa Kiswahili tukubali kuuziwa kwa bei ya kuruka. La, hapana. Maudhui muhimu hususan kwenye enzi hizi za utandawazi na ushindani wa biashara ambapo tunaweza kulinganisha bei na maudhui kama hayo kwa lugha nyengine.

boss, nikileta vya kingereza atasoma nani?

Nadhani kuna tofauti ya kusoma nao, kuwafundisha kusoma, na kuwasomea vitabu.

Iwapo lengo ni kuwasomea vitabu ili na wao wafanye mapenzi ya kusoma, basi si lazima uwasomee vitabu vya Kiswahili.

Unachoweza kufanya ni kuweka direct translation kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili wakati unawasomea na hapo ukapata fursa ya kubadili maudhui ili kuendana na maudhui yanayolingana na Mazingira ya Tanzania

Binafsi nilikuwa nikisomewa vitabu, mara nyingi vilikuwa vya Kiingereza lakini vilikuwa customized kuendana na mazingira yetu.

Akitajwa Cinderella kuwa ni mzuri kwa sifa za Kizungu kwa mfano, Dada yangu aliyekuwa akinisomea alikuwa aki-customize na kuweka sifa zangu. Au kama kuna picha basi alikuwa akihakikisha kueleza kuwa hiyo ni sifa ya uzuri kwa Wazungu, na kwa sie atatoa sifa ambazo zinalingana na sifa nilizonazo. Hivyo hivyo kwa tabia nyengine kama adabu za kula na kuzungumza na watu waliokuzidi umri.

Kwa hiyo ninadhani kusomea watoto vitabu vilivyoandikwa kwa ajili ya watoto wa nchi za Magharibi, pia kunaweza kutumika kama fursa nzuri ya kuwafunza watoto kuelewa mapema kuwa watu hawalingani kwa muonekano na tabia iwapo fursa hiyo itatumika vyema
 
Nimekupata point yako, asante!

swali ni "are you in"? au utasubiri hadi uone wengine wakifanya kwanza?
Kujibu mi nisha jibu: I'm in and I will do it regularly going forward.
Ninacho fanya hapa nikujaribu ku-adapt initiative na mazingira yangu
Binafsi leo hii nipo in such an environment as itaniwea ngumu kidogo
Kuwasomea vitabu fulani, kwa lugha fulani, idadi fulani ya watoto etc.
So I take my time to organise it well, but differently. in brief, the point is:
On the 5th, 6th and 7th kuna watoto watafaidi kwa kusomewa vitabu!
 
La kwanza ni kuwa tayari kufanya kitu and you are showing the example..
 
I was fortune enough to have a mother who believed in me when nobody did and she refused to allow me to fail. And she only allowed us to watch small amount of television. She made us read books when everybody else was outside playing. We had to read books but in the process of reading those books, I read about a lot of people, successful people. And I came to realize that the person who has the most to do on what's happening to you, is you. It's not somebody else. It's not some outside influence. It's not some environment factor. It's you and the choices you make. ~Dr. Ben Carson
 
Back
Top Bottom