EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
unajua ndio maana nataka tuanze hivi vitu sisi wenyewe; kuangalia taasisi na serikali imeshindikana. Kwa miaka 6 iliyopita ulimuona wapi Kikwete akikaa kumsomea mtoto kitabu? au Mbunge mwingine yeyote? Lakini kukosekana kwa vitabu vya Kiswahili siyo sababu ya wazazi kutokusoma na watoto wao. Na siyo lazima usomee watoto wako peke yako. Kwenye hili zoezi tunachofanya ni kufanya sisi wenyewe.
Tayari kuna watu wameshawasiliana na shule ili waende wakasomee watoto; kuna mtu tayari kapata watoto 12 wa jirani kuwasomea jioni ile
Kuna sehemu nilimsoma Prof. Mbele akisema kuwa japokuwa hili ni jambo zuri lakini lina utata pia. Alieleza matatizo ya kimazingira kwa watoto hasa wa vijijini kuweza kujisomea vitabu ambapo upatikanaji wake ni wa shida. Hata kwa maeneo ya mijini inaweza kuwa shida kimazingira pia ukiondoa familia ambazo zina wazazi wenye uwezo na mwamko. Wapo watoto wenye moyo wa kupenda kusoma lakini hawapati changamoto.
Lakini kama alivyosema cha muhimu ni vitendo hasa kutoka kwa watoto, wazazi wa leo na wazazi watarajiwa wa kizaji kijacho. Kinachohitajika ni kujaribu kujitengenezea tena utamaduni wa kusoma vitabu, japokuwa inaweza kuwa ngumu katika ulimwengu wa sasa ambao umetawaliwa na teknologia mpya. Wapo watu watalalamikia sana ukosefu wa umeme lakini wapo waliosoma vitabu kwa kutumia koroboi na kufanya vizuri tuu.
Labda kwa kupiga hatua moja mbele zaidi ingekuwaje kama waliobahatika kufika angalao chuo kikuu wangeji-organise na kuanzisha kijimaktaba kadogo kwenye vijiji wanavyotoka au kwenye shule zao za msingi walizosomea hata kama ni kabati moja tu? Nina imani kuwa watoto wataingia humo kusoma. Nimekuwa nikifikiria hili suala kwa kina sana lakini wapo wengine pia wanaosema kuwa miaka ijayo maktaba zitakuwa "digitalised". Hata hivyo, kwa mazingira yetu naona bado tuko mbali sana, japokuwa "digitisation" inaweza kusabisha kuwepo kwa uhaba wa vitabu ambavyo ni "hard copies".
Nafikiri badala ya kuongelea sijui matatizo ya umeme, serikali mbovu, ukosefu wa vitabu vya kusoma, mawasiliano, n.k. sisi wenyewe ambao tumefanikiwa kwenda shule na kufika hapa tulipo tujaribu kufanya mikakati wa kuanzisha kijimaktaba kadogo kwenye vijiji vyetu halafu tuangalie matokeo. Nimeshaona baadhi ya watu waki-fundraise kujenga darasa kwenye shule za vijiji wanavyotoka. Hata hivyo, nimekuwa nikijiuliza which comes first. Darasa la kusomea au kitabu cha kusoma?