Ardhi ya umma yauzwa kwa tajiri kinyemela Mwanza

Easymutant

R I P
Jun 3, 2010
2,564
1,129
Imeandikwa na Meshack Mpanda (Mwanza)

Wajumbe 27 wa Serikali ya kijiji cha Nyangho’mango katka kata ya Usagara Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza wameuza ikari 80 katika kilima cha Ntende kijiji ni hapo kwa thamani ya shilingi 1,200,000/=

Eneo hilo lenye kilima limeuzwa Desemba 2004 kwa mwekezaji KASCO MINING CO. LTD wa jijini Mwanza kwa lengo la kupasua mawe ili kuzalisha kokoto, uamuzi wa kuuza kilima hicho ulifikiwa na wajumbe hao siku ya Ijumaa tarehe 24, Desemba 2004 baada ya kufanyika kikao cha Serikali ya kijiji na mwakilishi mwekezaji huyo na wajumbe wote kutia saini na kugonhwa mihuri wa Halmashauri ya kijiji hicho chenye usajili Namba MZ/VG/389.


Uchunguzi uliofanyika umegundua kuwa siku hiyo ya kusaini makubaliano pia malipo yalifanywa ambapo serikali ya kijiji hicho ilipokea fedha hizo kutoka kwa mwekezaji na kumwandikia mwekezaji huyo stakabadhi Namba 001 ya tarehe 24 Desemba 2004 iliyo sainiwa na Charles Bulugu aliyekuwa Afisa Mtenaji wa kijiji ambaye kwa sasa ni marehemu.


Fuatilia habari hii hapa - Ardhi ya umma yauzwa kwa tajiri kiaina | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
 
Kama waliuza kwa hiari yao tatizo liko wapi?mnunuzi kama alifata taratibu zote kosalake liko wapi?
 
Hiyari ya viongozi wachache wala rushwa haiwezi kuhalalisha uuzwaji wa mali ya wananachi maelfu. Ni sawa na hiyari ya kina fulani kutaka kuwalipa Dowans si uhalali wa Watanzania wote
 
Back
Top Bottom