Ardhi ya chuo cha IFM iliyogawiwa itarudi vp?

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,185
79,366
Wana-JF,

Nataka kufahamu ile ardhi ya chuo cha IFM iliyogawiwa kwa waadhirika wa mafuriko Jangwani, itarudi vp? Je maadili yalitumika katika kumshauri Mh Rais? Na je Rais ametumia mamlaka yake sawa? je ardhi ya institution (educational) inaweza kugawiwa kirahisi namna hiyo? Inamaana katika kufikiria kwake koote alikosa jawabu la ardhi kwa wakazi hawa...ila tu ile ardhi iliyopaswa kutumika kupanua chuo cha IFM ambacho kingenufaisha maelfu ya wanafunzi woote wa Kitanzania? Kwa jinsi mambo yanavyoenda sishangai chuo kikaenda kujengwa Msoga maana kwa sasa kila kitu ni mwendo wa mitaa hiyo tu! Kwanini hawa jamaa wa Jangwani wasipelekwe huko Msoga instead? Tukumbuke Maamuzi hovyohovyo husababisha mipango ya maendeleo kwenda hovyohovyo pia!

NB: Ninahuzunishwa na yaliyowapata ndugu zetu wa Jangwani ukizingatia serikali imekuwa ikikaa kimya na kuacha watu wajenge mabondeni bila kuchukua hatua, mwenyezi Mungu azilaze pema roho za Marehemu wote
 
Mkuu Geza Ulole, IFM tayari wamepewa eneo la ekari elfu moja (1000) kule Msata kwa ajili ya upanuzi wa chuo na fidia tayari imeshaanza kulipwa kwa wananchi ambao maeneo yao yamechukuliwa.
 
Wana-JF,

Nataka kufahamu ile ardhi ya chuo cha IFM iliyogawiwa kwa waadhirika wa mafuriko Jangwani, itarudi vp? Je maadili yalitumika katika kumshauri Mh Rais? Na je Rais ametumia mamlaka yake sawa? je ardhi ya institution (educational) inaweza kugawiwa kirahisi namna hiyo?

Hao IFM nao hawana maana hilo eneo waligawiwa miaka mingi tu hawafanyi lolote sheria ya ardhi iko wazi ukipewa kiwanja hufanyii chochote ruksa kugawia mwingine.Miaka yote wanajibana katikati ya jiji mahali finyu hamna hata paki wakati eneo wanalo,wateja wanao kibao,maada wanachukua kwa wanafunzi kibao, wametoa macho tu hawajengi wamebakia kuongea kingereza mjini.

Hongere serikali kuchukua.Nasikia kuna mashirika na mavyuo mengine ya umma yana maeneo walipewa hawafanyii kitu chukueni serikali gawieni wengine.
 
Wana-JF,

Nataka kufahamu ile ardhi ya chuo cha IFM iliyogawiwa kwa waadhirika wa mafuriko Jangwani, itarudi vp? Je maadili yalitumika katika kumshauri Mh Rais? Na je Rais ametumia mamlaka yake sawa? je ardhi ya institution (educational) inaweza kugawiwa kirahisi namna hiyo? Inamaana katika kufikiria kwake koote alikosa jawabu la ardhi kwa wakazi hawa...ila tu ile ardhi iliyopaswa kutumika kupanua chuo cha IFM ambacho kingenufaisha maelfu ya wanafunzi woote wa Kitanzania? Kwa jinsi mambo yanavyoenda sishangai chuo kikaenda kujengwa Msoga maana kwa sasa kila kitu ni mwendo wa mitaa hiyo tu! Kwanini hawa jamaa wa Jangwani wasipelekwe huko Msoga instead? Tukumbuke Maamuzi hovyohovyo husababisha mipango ya maendeleo kwenda hovyohovyo pia!

NB: Ninahuzunishwa na yaliyowapata ndugu zetu wa Jangwani ukizingatia serikali imekuwa ikikaa kimya na kuacha watu wajenge mabondeni bila kuchukua hatua, mwenyezi Mungu azilaze pema roho za Marehemu wote
IFM ni wazembe! Wanalo hilo eneo miaka kibao! Hebu jiulize hata NBAA wameshaanza ujenzi wa Accountancy Professiona Centre(APC) huko Bunju inakuwaje IFM na ma ada yao ya mamilioni na ruzuku juu hata tofali bado? Wazembe wale!
 
Mh! eneo la geuza IFM walinyagwanya siku nyingi ndio maana wakapewa eneo nyingine Bwagamoyo, pale inasemekana pana vyanzo vizuri vya maji, hivyo lilipelekwa Dawasco kama hecta 500 hivyi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom