Apson: The Beginning of TISS's Failure

Na sasa hivi wageni maadui gani wamejipenyeza?

Kama hakuna unajuaje ni wabovu?

kweli hili swali umelifikiria au umeuliza tu alimradi uulize? Nikupe mifano ya wageni waliokuja na kuingia hadi chumbani na kuondoka na vito vyetu vya thamani huku walinzi wakiwa nje wanacheza bao?
 
kweli hili swali umelifikiria au umeuliza tu alimradi uulize? Nikupe mifano ya wageni waliokuja na kuingia hadi chumbani na kuondoka na vito vyetu vya thamani huku walinzi wakiwa nje wanacheza bao?

Mkulu huyu kijana hajui anachouliza, wazungu wenyewe wanakwambia unaingia Tanzania na $1000 unatoka na mabilioni, sasa hivi usalama wa taifa hawana chochote cha maana wanachofanya sasa hivi zaidi ya kula rushwa kwa kutisha watu ambao hawajui haki zao. Hii department ilikuwa mojawapo ya best department wakati wa mwalimu, ndo maana tuliweza kuwasaidia nchi jirani kupigania uhuru wao.
Walikuwa wanaogopwa kama nini kwenye nchi za kusini mwa jangwa la sahara even mashirika ya Africa ya kusini hayakuwa na uwezo wa kupenetrate Tanzania.
 
kule kwenye podomatic kuna mtu ameniandikia ati nadhani wanashindwa kunipata hapa Marekani. Sasa, hiyo inahusiana vipi na hoja zangu. Ndio maana hii mada will take a different turn on Friday.... mlioko nyumbani jaribu kupata gazeti la "Kulikoni" mwishoni mwa juma hili.
 
Problem imetoka kwa Apson aliyelinda MAFISADI (Mramba, Sumaye, Mkapa, Yona Chenge, Mahita ......... na yeye kuwa mmoja wao.

Jamani RO hana tatizo ila anakazi ya kulekebisha idara na JK inatakiwa kumpa support
 
....eeenh, ilikuwa enzi ya cold war!! je hao CIA tuliwadhibiti peke yetu?? tuwe wakweli hapa.

Kwa ujuzi wangu mdogo wa haya mambo kuna uhusiano usio rasmi wa hizi idara especially kwenye information sharing....so tunaweza tukawa tulikuwa na back up ya KGB au DGI au MOSAD(ambao inasemekana idara yetu iliundwa kwa mfumo wao) lakini ukweli unabaki kuwa idara yetu ilikuwa na ufanisi wa hali ya juu during that period.
CIA on the other hand no comments.

Sasa what went wrong kwenye idara yetu?
 
Hivi kuna mtu humu anaamini Apson atafanya la maana pale ili twende mbele? the guy has been there forever na mawazo yake ya old Soviet union,mambo mengine ni kujitakia tuu kuwapa kazi watu kama hawa.

Koba,

Hapa unaongelea nini? Apson alishastaafu miaka miwili sasa.
 
YNIM
Huyo Mlawa ndio alikuwa nani enzi hizo? DG? na vipi aliingiza siasa TISS
 
that's obvious.....Soviet Union, Cuba, China na karibu eastern block yote ilikuwa inashare intel na sisi juu ya hao CIA na Makaburu!! hivi wataka kusema kwamba tuliweza hayo yoooote peke yetu wakati wa kilaza Mlawa??

sasa kama tulikuwa tunashirikiana na vyombo vyote hivyo enzi hizo leo imekuwaje kiasi kwamba CIA wameshindwa kutuambia kuwa Richmond ni kampuni ya Kitapeli na MI5 na MI6 wameshindwa kutuambia tumelanguliwa rada? Ni lini tulianza kukosa ushirikiano toka vyombo hivyo vingine...

** Bi mdogo asante.
 
sasa kama tulikuwa tunashirikiana na vyombo vyote hivyo enzi hizo leo imekuwaje kiasi kwamba CIA wameshindwa kutuambia kuwa Richmond ni kampuni ya Kitapeli na MI5 na MI6 wameshindwa kutuambia tumelanguliwa rada? Ni lini tulianza kukosa ushirikiano toka vyombo hivyo vingine...

** Bi mdogo asante.

Mwanakijiji,

Kwenye hili, hata tungeambiwa, je tungewasikiliza? Hao hao waliotakiwa kuambiwa ndio walikuwa wanafaidika na huo ufisadi.

Waliambiwa ya EPA, je kuna kitu walifanya?

Kama la Richmond, watu walisema mapema sana, lakini serikali haikutaka kusikiliza na matokeo yake Watanzania karibu wote wanaumia kutokana na kupanda sana kwa umeme.
 
.......nani kasema tulikuwa tunapata msaada wa CIA na hao M15/16??! nilikuwa najibu msaada tuliopata kuzuia hao CIA na makaburu(kama ambavyo Icadon alivyokuwa kauliza/kasema)!!...na si vinginevyo(unaweka maneno kwenye vidole vyangu)!
....husomi ninacho andika!! ni wewe na mawazo yako, bila kusoma/kuelewa ya wengine.

....niambie wewe basi, kabla ya Apson ni mikataba mingapi bogus ilozuiwa na taasisi hii??.
hakuna mikataba mikubwa tuliyoingia! Au wewe useme ni mkataba gani mkubwa wa nishati au madini tulioingia kabla ya hawa jamaa..?
 
Mwanakijiji,

Kwenye hili, hata tungeambiwa, je tungewasikiliza? Hao hao waliotakiwa kuambiwa ndio walikuwa wanafaidika na huo ufisadi.

Waliambiwa ya EPA, je kuna kitu walifanya?

Kama la Richmond, watu walisema mapema sana, lakini serikali haikutaka kusikiliza na matokeo yake Watanzania karibu wote wanaumia kutokana na kupanda sana kwa umeme.


Sisemi kuambiwa sisi, nina maana ya wenye kufanya maamuzi. Kama kiongozi wa Usalama ametoa ushauri na haukusikilizwa ana sababu gani ya kuendelea kushikilia nafasi hiyo? Ana ujasiri gani wa kuja kushauri baadaye kuhusu jambo jingine?
 
that's obvious.....
Soviet Union, Cuba, China na karibu eastern block yote
ilikuwa inashare intel na sisi juu ya hao CIA na Makaburu!! hivi wataka kusema kwamba tuliweza hayo yoooote peke yetu wakati wa kilaza Mlawa??

sasa tuliacha lini kushare intelligence na China, Soviet Union, Cuba na China na Eastern Block yote? ... je sasa hivi tuna share intelligence na mtu yeyote?
 
....sasa hatukuingia kwasababu gani? juu kwamba walijua ni mibovu wakaitolea mbavuni au sera za wakati huo(ujamaa wa njozi) zilikuwa haziruhusu makampuni binafsi kuendesha huduma hizo!!? kama la pili ndio jibu lako, sasa utajuaje kwamba walikuwa fit wakati deals hazikuwepo?? acha utani bwana....


Hatukuingia kwa sababu hatukuwaamini wageni kuingia nchini na kushikilia sekta muhimu. Siyo kwamba hakukuwa na watu wanataka kuja kuingia nchini. Usalama wa Taifa ulikuwa ndiyo huo zaidi yaani Usalama wa Taifa. Makampuni yaliweza kuingia lakini yalichekechwa mno na kulikuwa na uangalizi wa hali ya juu.
 
...acha utani wewe, hiyo ni kwasababu ya siasa za wakati huo na si ati kwamba tulikuwa makini!!! kama tulikuwa makini kwanini hao watu wa intel hawakujua mapema kwamba ujamaa wa njozi wa marhumu utafeli?? au nae alimbiwa akawa haambiliki kama kawaida yake?..kila mtu alipingwa mshangao soviet ilipomomonyoka, tukabaki pekeyetu kama Titanic kwenye cold waterz za Atlantic!!! halafu unashangaa kwanini hawa wa leo nao hawaambiliki.......watoto huiga baba, uozo ni ule ule sema tu nyakati ndio tofauti!!!.

si ndio maana nimekushangaa ukishangaa UDSM wakati wanachofuata ni uozo ule ule. Hakuna mtu anayewajibika kwa matatizo na makosa yake yeye mwenyewe katika ulimwengu wako wewe. Kwa matatizo yaliyopo sasa hususan kushindwa kwa intelligenstia ambako ni kufuru naamini kulianzia baada ya tu ya kuundwa kwa TISS chini ya Apson.
 
Mwanakijiji,

..inasemekana Lt.Gen Imran Kombe, aliyemtangulia Apson, naye alikuwa na mali nyingi sana. kwa hiyo inawezekana kabisa kwamba "ufisadi" haukuanzia wakati wa Apson.

..kuna habari kwamba Apson alimzawadia mwanae gari la fahari wakati wa harusi yake. Raisi na viongozi wakuu wa serikali walihudhuria harusi hiyo.

..IGP Mahita naye inasemekana alimpa mwanawe nyumba ya kifahari kama zawadi ya harusi. again, Raisi na serikali nzima walishuhudia tukio hilo.

..unajua hili tatizo la ufisadi limesambaa mpaka kwenye vyombo vya dola[polisi,cid,usalama,magereza,jeshi..]. kwa msingi huo hii vita ya mafisadi ni ngumu kweli kweli. pamoja na hayo ushindi dhidi ya mafisadi ni lazima.
 
JokaKuu, sidhani kama kuangalia mtu ana mali kiasi gani = ufisadi. Nadhani mtazamo huo ni mbaya na hauingii kwenye mantiki. Tukisema mali = ufisadi tutakuwa hatutendi haki.
 
Back
Top Bottom