April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

Sasa hivi imetulia kwa muda, mimi nipo maeneo ya Muhimbili lakini bado tulikuwa tunaisikia kwa nguvu sana
 
kwani hii ya leo inatofauti na ile ya jana?

maana jana i was so uncomfortable..unajua tena you never know hawa CHADEMA hawaaminiki
 
Huku maeneo ya Kipawa karibu kabisa na DIA mtikisiko ni mkubwa sana na imesikika milipuko 2 hadi sasa ikiambataa na kaupepo ka kasi
 
Boko kishindo kimesikika ...
Wanasema sasa wameweza ku-control, lakini damage iliyotokana na issue hii haijajulikana bado.

Hawakubali kuongea kwa kirefu, ni "Everything is under control... Tutaongea baadae" kisha unakatiwa simu!
 
I hope sio dalili nyingine ya uzembe wetu! Tunahifadhi vipi mabomu karibu na makazi ya watu? Tuombee kuwa hakuna aliyepoteza maisha katika tukio hilo!

Amandla......
 
Du hapa ofisini maeneo ya Masaki nimetoka nje peke yangu wenzangu wakanicheka wakidhani ni radi, tutakuja kufa kwa ku take easy kila kitu.
 
Isijekuwa kuna uvamizi

Sio uvamizi, milipuko inatokea katika maeneo ya kambi ya jeshi, kizuiani, pale penye minazi mirefu, kwa wele walopita njia ya mbagala wanaifahamu hiyo sehemu vizuri. Inawezekana kuna uzembe hapo, tutasikia baada ya muda....
 
Ni kweli kuwa kuna tatizo la kupata simu baada ya milipuko hii?

Fundi, ni watu wanajenga karibu na kambi za jeshi au silaha zinahifadhiwa kwenye makazi ya watu?
 
Ni milipuko iliyotikisa majengo mengi Dar. Jeshi limethibitisha kwamba ni silaha zimelipuka kwenye kambi moja huko Mbagala. Vijana wa kazi wanaelekea huko, tutajulishwa kinachoendelea soon.
 
Kuna jengo refu hapa Samora Kioo kimevunjika baada ya mojawapo ya mlipuko na moshi ulikuwa unaonekana kutokea maeneo ya Mbagalla.

Hata kama ni vipi inaonekana this was uncontrolled na lazima kuna impact. Trauma kwa raia wasiotegemea hii ni kubwa na inaelekea panick ni kubwa maeneo ya Mbagala.
 
Jamani ni nini hasa maana familia yangu imepanic sana..wako zakiem nami niko
Mtwara. Mwenye reliable information aseme.
 
Back
Top Bottom