April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

Ni vyema wangetoa taarifa mapema watu wajiandae, watasababisha misukumo ya mioyo isiyo ya lazima!
ndaga
 
Nimewsilana na mtu anayekaa karibu na uwanja wa sabasaba, ameniambia kweli kuna moshi na vitu vinaruka hewani tokea mbagala, tena ameona magari ya polisi yakitokea mbagala yakiwa yamewasha taa, anadhani kuna watu wameumia ndiyo wanakimbizwa hospitali.
 
nasikia barabara kilwa imefungwa na watu hawaruhusiwi kwenda huko, jamaa wangu ameshindwa kwenda kwake mbagala kuangalia familia yake. Mwweeeee!
 
Sasa huyu anaesema ni mlipuko wa matanki ya BP Kurasini na hapo hapo twaambiwa ni Mbagala ana maanisha nini? tushaanza potosha habari jama?!
 
Wakuu Kumbe jengo lililo kuwa linahifadhi siraha limelipuka siraha zinalipuka Mbagala na si mazoezi.Watu wengi wamepata madhara....
 
Sasa huyu anaesema ni mlipuko wa matanki ya BP Kurasini na hapo hapo twaambiwa ni Mbagala ana maanisha nini? tushaanza potosha habari jama?!
Hapana, nimeelezwa milipuko hiyo inayosababisha moshi mkubwa hewani ipo maeneo ya Mbagala ilipo ghala ya silaha za Jeshi.
 
Wakuu inasemekana Military base ya Mbagala got fire. Habari hizi tumezipata kutoka kwa watu wa Ultimate Security. Hapa town ni wasi wasi tupu. Tuombe mungu hivyo vinavyolipuka visilete maafa kwa watu kwani kambi ile sasa hivi imezungukwa na makazi ya watu.
 
Clouds FM Wametoa breaking news wamesema ni jengo lililokuwa na silaha za kijeshi huko mbagala ndilo limelipuka
 
tetesi zinadai hii imeokea kwa bahati mbaya ..si kitu cha kupanga hivyo isingewezekana kutoa taarifa kabla! maofisi mengi naona hayakaliki watu wako njee huku msasani
Basi kama mpaka Msasani kishindo kimewafikia milipuko ni mikubwa!
 
Clouds FM Wametoa breaking news wamesema ni jengo lililokuwa na silaha za kijeshi huko mbagala ndilo limelipuka
Kazi ipo, juzi juzi gari lilikuwa limebeba mabomu lilipofika uwanja wa ndege liliwaka MOTO, lilipelekwa mbio mbio kwenye kambi, TULITEGEMEA MILIPUKO kumbe Mungu alikuwa upande wetu.
 
Wakuu naskia kuna watu wamesha jeruhiwa na wengine kupoteza maisha stay tuned........
 
hali inayoendelea kwa sasa ni kwamba kuna hali isiyo ya kawaida inaendelea kwenye ghala la silaha za kijeshi huko mbagara. jekuna mweye habari zaidi?
 
Back
Top Bottom