Apple yafungua Appstore na iTunes Tanzania

ManiTek TV

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
410
159
[h=3]Apple yafungua AppStore Tanzania[/h]

Bendera ya Tanzania, chini kulia ikithibitisha kuwa hii ni Appstore ya Tanzania

Kwa muda mrefu sasa tumepunguza kasi ya kuandika makala mpya kwa matayarisho ya uzinduzi rasmi wa blogi yetu ya kiingereza yaani www.gadget-one.com, lakini hili imekuwa ni vigumu kuruhusu litupite. Kampuni ya Apple watengenezaji maarufu wa simu za iPhone na gajeti nyingine wamefungua maduka yao ya mtandaoni, yaani AppStore la gajeti zinazotumia iOS (iPhone, iPod Touch, iPad na Apple TV) na Mac AppStore la kompyuta za Mac katika nchi 33 zaidi Duniani ikiwemo Tanzania. Read more »
C
hanzo: Gajetek - Gajet na Teknolojia
 
Yeah, i'm not sure if I should be happy with this. Wakifungua appstore ina maana wataanza kufuatilia bidhaa zao. Na wakifuatilia itabidi tulazimike kununua os zao za Mac na sio kudownload pirated versions ambazo haziruhusiwi. Tukumbuke 2008 Microsoft ilipowakamata watanzania wawili kwa kukutwa na pirated windows, walipekekwa court. So tuwe makini.
 
Sidhani kama Apple ni wafuatiliaji wa masuala kama haya, tofauti na Windows, Apple hupigana na masuala haya kwa kutumia teknolojia na mbinu za kibiashara, kwa mfano miaka ya nyuma walikiwa wakitoa update kuzipach pirated software, tangu Mac AppStore imeanza wameacha mtindo huu, isipokuwa wanaendelea nao kwenye iOS firmware na hasa iPhone. Hivi sasa inaelekea wanalenga kufanya Apps na bidhaa nyingine kuwa affordable ili kuwafanya watumiaji wasione haja ya kuchakachua. Kwa mfano Mac OS X Lion wameishisha bei ukilinganisha na Snow Leopard kwa $100, yaani kutoka $129 hadi $29. Pia wameondoa masuala ya keys, yaani ina maana kwamba watu 10 mkishare akaunti na kununua app na wote mkazitumia, technically hamjavunja sheria na wala sio poracy. Mbinu kama hizi zimeboost sana mauzo ua Apple katika software, kwa mfano siku ya juzi tu pekee waliopotoa Lion wameuza nakala milioni moja kwa siku moja. Hii ilikuwa ni rekodi
 
yaan kuna apps kibao tu tutakua tunakosa,tena tanzania?huh! Sio kila apps zilizopo appstore zinapatikana nchi zote hata zile za bure,bora ujiunge zako na free acc. ya US upate apps zote,thats wat i've bin doing for a longtime,na idivice yko iwe jailbroken otherwise utaumia!
 
Ha haa haa hivi application zilizokuwamo kwa simu zote zaweza tumika TZ? Unapochakachua zinasaidia kukidhi matumizi ya kifaa ulichonacho?
 
yaan kuna apps kibao tu tutakua tunakosa,tena tanzania?huh! Sio kila apps zilizopo appstore zinapatikana nchi zote hata zile za bure,bora ujiunge zako na free acc. ya US upate apps zote, thats wat i've bin doing for a longtime,na idivice yko iwe jailbroken otherwise utaumia!

Ni kweli kwamba si kila App kwenye AppStore inapatikana Dinuani kote, hata hivyo AppStore ya iOS ina apps 425,000. Na si kweli kwamba Apps hizi zote zinapatikana US Store, kwa mfano BBC iPlayer inapatikana bure UK na US ni $10 kwa mwezi. Na zipo Apps nyingi tu ambazo ni maalum kwa nchi fulani kwa hiyo hata duka la US huzipati. Pia jailbreak ni moja kati ya njia ya kupata apps za bure lakini jailbreak ina matatizo mawili makubwa.

1. Mara nyingi iOS device (iPhone, iPad, iPod Touch au Apple TV) inakuwa very unstable, na hivyo mara nyingine kukubidi kuifuta device yako yote na kuanza upya.

2. Inabidi iOS yako iwe nyuma, yaani kwa mfano sasa hivi iOS 5 beta 4 imetoka juzi, ambayo anategemea jailbreak hawezi kuitumia iOS hiyo kwa vile hakuna jailbreak yake.

Kwa hiyo Appstore itasaidia wale ambao wamechoshwa na hizi mbio za paka na panya (Hackers Jailbreaks and Apple Patches) na hasa hasa wale ambao wako tayari kutoa $3 kununua apps kama vile The Economist, ambapo hata ukichakachua huwezi kuipata app hii
 
Ni kweli kwamba si kila App kwenye AppStore inapatikana Dinuani kote, hata hivyo AppStore ya iOS ina apps 425,000. Na si kweli kwamba Apps hizi zote zinapatikana US Store, kwa mfano BBC iPlayer inapatikana bure UK na US ni $10 kwa mwezi. Na zipo Apps nyingi tu ambazo ni maalum kwa nchi fulani kwa hiyo hata duka la US huzipati. Pia jailbreak ni moja kati ya njia ya kupata apps za bure lakini jailbreak ina matatizo mawili makubwa. 1. Mara nyingi iOS device (iPhone, iPad, iPod Touch au Apple TV) inakuwa very unstable, na hivyo mara nyingine kukubidi kuifuta device yako yote na kuanza upya.2. Inabidi iOS yako iwe nyuma, yaani kwa mfano sasa hivi iOS 5 beta 4 imetoka juzi, ambayo anategemea jailbreak hawezi kuitumia iOS hiyo kwa vile hakuna jailbreak yake.Kwa hiyo Appstore itasaidia wale ambao wamechoshwa na hizi mbio za paka na panya (Hackers Jailbreaks and Apple Patches) na hasa hasa wale ambao wako tayari kutoa $3 kununua apps kama vile The Economist, ambapo hata ukichakachua huwezi kuipata app hii
US appstore ina karibia content zte zilizopo appstore....app gan utaitafuta ukose? Na kuhuhusu jailbreak tayar ios 5 beta 4 ishakua j.b tayari..
 
US appstore ina karibia content zte zilizopo appstore....app gan utaitafuta ukose? Na kuhuhusu jailbreak tayar ios 5 beta 4 ishakua j.b tayari..
Mkuu apple wanatengeneza apps kulingana na nchi husika kuna apps ya airtel ukiifunga kwenye simu yako inakuwa ni useless kwa sababu inatumika kwa Marekani na Canada tu.
 
Mkuu apple wanatengeneza apps kulingana na nchi husika kuna apps ya airtel ukiifunga kwenye simu yako inakuwa ni useless kwa sababu inatumika kwa Marekani na Canada tu.
ts true lakin point yangu ni kua store ya marekani ina karibia apps zote.
 
yeah acha nisubirie hawa nokia waanze 2mia windows Os maana symbian naona wamenichosha.. ...apple za wakubwa
 
US appstore ina karibia content zte zilizopo appstore....app gan utaitafuta ukose? Na kuhuhusu jailbreak tayar ios 5 beta 4 ishakua j.b tayari..

Nitakupa mfano wa apps 5 ambazo zinapatikana kwenye appstore ya UK lakini USA hakuna. Sky Go (ambayo ina channel 5 za skysports pamoja na sky news) na ITV Player, BBC iPlayer, Natwest na Three. Na ujue kwamba zipo nyingine nyingi tu. Kwa mfano kuna baadhi ya apps ambazo ni za kichina au kirusi kwa ajili ya mambo yao na kadhalika hizi kwa nini waziweke kwenye US store? Hii inatokana na sababu kama vile biashara ya app husika haipo USA au app inahusika na organisation fulani kama vile hospitali ambayo haipo USA, lugha mbali mbali ambazo hazizungumzwi US na kadhalika.

Katika masuala ya Jailbreak, hata kama jailbreak ya iOS 5 beta 4 imeshatoka, nilichokuwa ninataka kueleza ni kwamba mara nyingi kunakuwa na muda wa kusibiri baina ya jailbreak na firmware mpya. Nadhani hii naina ubishi.
 
Back
Top Bottom