Apigwa, achomwa moto, auwawa kwa kutuhumiwa kuiba piki piki

Kitomai

JF-Expert Member
May 21, 2009
1,060
281

*

Wananchi wenye hasira wamemuua na kumchoma moto kijana mmoja aliyetuhumiwa kuiba piki piki, . Tukio hilo limetokea katika eneo la kimara Mwisho pembezoni mwa barabara iendayo Morogoro mita takribani 200 kutoka katika kituo kidogo cha Polisi cha kimara Matangini leo tarehe 21/8/2010 majira ya saa tano asubuhi. Mpaka habari hizi zinarushwa hewani jina la kijana huyo lilikuwa bado halijatambulika

Kwa mujibu wa mashuhuda, kijana huyo aliwasili katika eneo la Kimara king'ongo na kuiba piki piki kisha kuondoka nayo akiwa anaelekea maeneo ya Ubungo. Alipofika karibu na maeneo ya Resort akaishiwa mafuta ndipo alipoamua kuweka mafuta katika kituo kilichopo eneo hilo. Wakati akifanya hayo yote, walioibiwa walikua wakimfuatilia hatimaye wakamkuta ameshaweka mafuta na sasa anaondoka ndipo walipomkamata na kurudi naye kimara mwisho, kimara king'ongo.

Walipofika hapo wakajivisha majukumu ya uendesha mashitaka, uhakimu, hatimaye wakatoa adhabu ya hukumu ya kifo kwa kipigo, kwa kupondwa mawe hatimaye kumchoma moto mpaka alipopatikana na mauti. Polisi ambao walikuwa karibu na tukio hilo walizidiwa nguvu na raia hao wenye hasira kali, mpaka hapo baadaye kilipokuja kikosi maalumu cha kupambana na fujo, kikosi hicho kilifika wakati wauaji wameshatekeleza hukumu ya kifo.

Kunradhi nimembatanisha picha ambazo siyo nzuri lakini imebidi nifanye hivyo kwa sababu sina jinsi nyingine ya kukuelezea tukio hilo.

MAONI.

Piki piki ya kichina ina thamani gani mpaka kutoa uhai wa mtu wenye thamani kubwa isiyolingana hata kidogo na chombo cha usafiri? Kwa nini jamii inakosa subira kiasi hicho? Kumbuka huyo alituhumiwa tu, alikua mtuhumiwa, akupewa nafasi kukata rufaa! Inakuaje wananchi hao hao wanaendelea kuwatazama bila kuwagusa kwa kidole watuhumiwa wenye dhamana kubwa za uongozi ambao wanatuhumiwa kuiba mamilioni ya fedha? Nini maana yake hii, tuseme tumekosa upendo? Basi nimejiuliza maswali mengi sijapata majibu, wewe je mwana Jf huna maoni gani?
 
Attachments

  • PIC00250.JPG
    PIC00250.JPG
    45.2 KB · Views: 188
  • PIC00251.JPG
    PIC00251.JPG
    45.1 KB · Views: 188
  • PIC00236.JPG
    PIC00236.JPG
    48.3 KB · Views: 180
  • PIC00240.JPG
    PIC00240.JPG
    45.2 KB · Views: 171
  • PIC00246.JPG
    PIC00246.JPG
    47.2 KB · Views: 180
  • PIC00237.JPG
    PIC00237.JPG
    37.5 KB · Views: 149
  • PIC00249.JPG
    PIC00249.JPG
    45.7 KB · Views: 146
  • PIC00243.JPG
    PIC00243.JPG
    47.9 KB · Views: 156
  • PIC00247.JPG
    PIC00247.JPG
    46 KB · Views: 193
Sidhani kama hao waliotoa hukumu hiyo walikuwa ni wasafi.
 
Hii kitu niliiona...ilikua sio scene nzuri kuangalia!
 
Kuna kila sababu ya wahalifu kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Kuna ushahidi gani kwamba huyo aliyechomwa sie ndie aliyekuwa akizulumiwa pikipiki na hao waliomtuhumu? Na wliomuua wana haki gani ya kumhukumu mtuhumiwa kifo? Tuliombe jeshi la polisi lianze kazi ya kuwafikisha waliotekeleza hayo mauaji katika vyombo vya sheria. Hali hii ikiachwa kwa kisingizio cha watu wenye hasira kali, itafika siku watu hao hao wenye asira kali watamchoma moto rais wao. Tabia hukua na kufikia climax, na kama ni mbaya ukomavu wake ni angamizo kwa taifa.
 
hii inatokana na wao (viibaka,wezi na majambazi ) kuua raia wasio na hatia utakuta hawa jamaa wanaua kwa laki mbili ama tatu, au kuwachoma bisibisi na kuwapiga nyundo waendesha pikipiki, waendesha pikipiki ilifika point wakaandamana kwa unyanyasaji wa hawa jamaa, leo hii mtu wa namna hii unamuonea huruma. huyu alikuwa tayali kuua kwa ajili ya hiyo pikipiki.

anyway: Mungu amuhukumu kutokana na makosa au mema yake
 
Ooooooooooooooooh my God! Jamani unyama gani huu. Yahilahi toba. Mungu amrehemu huyu kijana
 
...Wanaoiba kuku na pikipiki wanachomwa moto, wanaoiba na kusababisha hospitali zetu zikose madawa na shule zetu zikose madawati tunawashangilia na kuwatukuza. Poor we.
 
*

Wananchi wenye hasira wamemuua na kumchoma moto kijana mmoja aliyetuhumiwa kuiba piki piki, . Tukio hilo limetokea katika eneo la kimara Mwisho pembezoni mwa barabara iendayo Morogoro mita takribani 200 kutoka katika kituo kidogo cha Polisi cha kimara Matangini leo tarehe 21/8/2010 majira ya saa tano asubuhi. Mpaka habari hizi zinarushwa hewani jina la kijana huyo lilikuwa bado halijatambulika

Kwa mujibu wa mashuhuda, kijana huyo aliwasili katika eneo la Kimara king'ongo na kuiba piki piki kisha kuondoka nayo akiwa anaelekea maeneo ya Ubungo. Alipofika karibu na maeneo ya Resort akaishiwa mafuta ndipo alipoamua kuweka mafuta katika kituo kilichopo eneo hilo. Wakati akifanya hayo yote, walioibiwa walikua wakimfuatilia hatimaye wakamkuta ameshaweka mafuta na sasa anaondoka ndipo walipomkamata na kurudi naye kimara mwisho, kimara king'ongo.

Walipofika hapo wakajivisha majukumu ya uendesha mashitaka, uhakimu, hatimaye wakatoa adhabu ya hukumu ya kifo kwa kipigo, kwa kupondwa mawe hatimaye kumchoma moto mpaka alipopatikana na mauti. Polisi ambao walikuwa karibu na tukio hilo walizidiwa nguvu na raia hao wenye hasira kali, mpaka hapo baadaye kilipokuja kikosi maalumu cha kupambana na fujo, kikosi hicho kilifika wakati wauaji wameshatekeleza hukumu ya kifo.

Kunradhi nimembatanisha picha ambazo siyo nzuri lakini imebidi nifanye hivyo kwa sababu sina jinsi nyingine ya kukuelezea tukio hilo.

MAONI.

Piki piki ya kichina ina thamani gani mpaka kutoa uhai wa mtu wenye thamani kubwa isiyolingana hata kidogo na chombo cha usafiri? Kwa nini jamii inakosa subira kiasi hicho? Kumbuka huyo alituhumiwa tu, alikua mtuhumiwa, akupewa nafasi kukata rufaa! Inakuaje wananchi hao hao wanaendelea kuwatazama bila kuwagusa kwa kidole watuhumiwa wenye dhamana kubwa za uongozi ambao wanatuhumiwa kuiba mamilioni ya fedha? Nini maana yake hii, tuseme tumekosa upendo? Basi nimejiuliza maswali mengi sijapata majibu, wewe je mwana Jf huna maoni gani?

MAONI.

Piki piki ya kichina ina thamani gani mpaka kutoa uhai wa mtu wenye thamani kubwa isiyolingana hata kidogo na chombo cha usafiri? Kwa nini jamii inakosa subira kiasi hicho? Kumbuka huyo alituhumiwa tu, alikua mtuhumiwa, akupewa nafasi kukata rufaa! Inakuaje wananchi hao hao wanaendelea kuwatazama bila kuwagusa kwa kidole watuhumiwa wenye dhamana kubwa za uongozi ambao wanatuhumiwa kuiba mamilioni ya fedha? Nini maana yake hii, tuseme tumekosa upendo? Basi nimejiuliza maswali mengi sijapata majibu, wewe je mwana Jf huna maoni gani

WAKATI UNAWEKA PICHA ZA MAITI ULIKUWA UJUI THAMANI YAKE NA PIKIPIKI SIKU NYINGINE USIJIHUKUMU MWENYEWE KABLA YA KUTUMA UJUMBE SOMA ULICHOANDIKA
 
Nimepata tetesi kwamba huyu bwana aliyeuwa hakuwa mwizi kimsingi....
Inasemekana kwamba alikua ameacha pikipiki yake kwa fundi....alipofika fundi akampa ile aliyokamtwa nayo (ambayo ni ya mtu mwingine) ili akununue mafuta kimara resort...wenye pikipiki yao wakamkuta na pikipiki yao.....baada ya hapo maisha ya jamaa yakawa hi
storia...
 
adhabu hii ni stahili kwao...wanauwa watu kwa kutaka kupora simu..ni watu wangapi wanakatwa mapanga kwa ajili ya kuporwa simu au mkoba ..this is job well done
 
Unachosema ni kweli roy huyo kijana sio mwizi yeye alienda kwa fundi akapewa hiyo na hakuiba -- kuna tatizo moja maeneo ya ubungo mpaka kimara wao wanaumoja wa waendesha piki piki hawa jamaa huwa wanatembelea na mapanga na silaha nyingine kazi yao ni kutoa hukumu kama hizi bila kuthibitisha
 
Back
Top Bottom