Apewa Huduma Mbovu Benki, Adai Fidia ya Mabilioni

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20


Tuesday, September 29, 2009 4:31 AM
Mwanaume mmoja wa nchini Marekani amefungua kesi mahakamani akidai fidia ya dola trilioni bilioni 1784 (usishangae tarakimu hazijakosewa) kutoka kwa benki moja nchini humo kwa kumuonyesha huduma mbovu. Dalton Chiscolm amefungua kesi mahakamani katika kitongoji cha Manhattan, New York, Marekani akidai fidia ya dola trilioni bilioni 1784 kutoka kwa benki ya Bank of America kwa kushindwa kumpa huduma bora kama mteja wa benki hiyo.

Chicolsom mbali na pesa hizo ameitaka benki hiyo imuingizie kiasi cha dola milioni 200 kwenye akaunti yake siku inayofuatia, limeripori shirika la habari la Reuters.

Jaji wa Manhattan, Denny Chin alisema kwamba hajawahi kuona kesi ya fidia ya kiwango hicho.

"Amelalamika kwamba alipiga simu nyingi sana kwenye tawi la benki hiyo New York na kupewa miongozo ambayo haikuwa sahihi na mfanyakazi mwanamke wa benki hiyo mwenye asili ya Hispania", ilisema taarifa ya jaji.

"Amelalamika kwamba hundi zake zilikataliwa kutokana na kutokamilika kwa taratibu za kibenki kufuatia miongozo aliyopewa na mfanyakazi wa benki hiyo".

Kiasi ambacho Chiscolm anadai kama fidia ni zaidi ya mara 1,000 ya kiasi ambacho dunia nzima iliingiza mwaka 2008 kwa mujibu wa takwimu za benki ya dunia.

Jaji Chin amempa muda Chiscolm hadi oktoba 23 mwaka huu kuelezea vizuri msingi wa madai yake.

Kama atashindwa kujielezea vizuri basi kesi yake itatupiliwa mbali na haitasikilizwa.

Source: Reuters



nifahamishe.com
 
duh;ingekuwa tanzania kila mtanzania angekuwa tajiri kwa kweli maana sijaona hata benki iliyo nafuu labda hii mpya ya wanawake tuwasubiri nao
 
I don't think this case/claim is meritorious.

It is his responsibility to annex statutory laws or case laws, to support his arguments/claim and how he came to such a conclusion that his case/claim worth such monies. Remember, BOA may file a counter claim against this person and/or cross move his claim.

Since this person is a pro se claimant/plaintiff seeking certain reliefs against the BOA, he is often be expected to construct legal arguments, cite legal authority, or draft his petition/complaint as artfully as a lawyer would. If the evidence defeats the claim, the claim is "meritless. Will be dismissed with preduce.
 
Inabidi hii benki ifilisike kama jamaa atashinda kesi. Maana kwa uhakika benki yenyewe haina hizo pesa yaani mtaji wote wa benki jumlisha na pesa za wateja sijui kama unafikia kiasi hicho cha pesa. Hivi ndo vioja vya dunia, lol!
 
Inabidi hii benki ifilisike kama jamaa atashinda kesi. Maana kwa uhakika benki yenyewe haina hizo pesa yaani mtaji wote wa benki jumlisha na pesa za wateja sijui kama unafikia kiasi hicho cha pesa. Hivi ndo vioja vya dunia, lol!

US kuna vituko mkuu,

Kuna jamaa anachagi watu hela ukigonga hodi mlango wake
 
I think huyu jamaa kakurupuka tu. It is difficult to support that claim of 1 plus 22 zeros. He want to be known in the media and perhaps his will go to history books. Let's wait and see if he can surely support his claim.
 
Back
Top Bottom