Apata Utasa wa Kujitakia kwa tamaa ya kupata mtoto wa kiume!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,972
1,649
Baada ya kupata ujauzito alihangaika kujua 'sex' ya mtoto kama akiwa wa kiume basi afunge uzazi maana tayari alishakuwa na mtoto wa kike. Baada ya kufanya vipimo vya ultr-sound, akaambiwa mtoto atakayezaliwa atakuwa wa kiume. Kumbe masikini hicho kipimo hakikuwa sahihi.

Siku ya kujifungua, akamwambia daktari kwamba wakati wa operesheni ya kumtoa mtoto, ni vyema amfunge na uzazi kabisa. Bila hiana siku ya operesheni daktari akamfunga kizazi mara alipomaliza kumzalisha kwa 'siza' kama wenyewe mnavyosema.

Ajabu ni pale mdada alipogundua kuwa mtoto alomzaa ni wa kike, ilihali alielezwa mwanzo na mtaalamu kuwa kachanga kangezaliwa ka kiume. Huu ni mwaka wa tatu sasa, mdada amebaki na huzuni kwa kujua kuwa hawezi tena kuzaa, na huo ndo umekuwa mwisho wa hamu yake ya kupata walau mtoto wa kiume ktk ndoa yake na mumewe.

Jamani mtoto ni mtoto tu, hata kama jamii zituzungukazo zinapenda zaidi vitoto vya kiume, hao wa kike imeonekana wengi ndo wenye kusaidia familia zao kuliko hao wa kiume. Mpende mtoto wako irrespective of her sex, jamani.
 
iwe fundisho kwa wengine

sina hakika na haya maelezo,kwa sababu dr inatakiwa ajue kwa nn unafunga uzaz? Kuna absolute indications na patients need.If ni ombi la mama na matokeo ya jinsia siyo uliyotegemea na una watoto wawili tu mtoto akitoka atakwambia ni wa kike na we utaamua afunge au aache kwa sababu wakati wa operation unakuwa active,hata kama umepewa ga anaweza kukuachia chance if ur wish ni mtoto wa kiume. Unless alikuwa mtoto wa tano ambapo kukuongezea chance ni kuhatarisha maisha yako.
 
Ah mie sifungi hata niwazae 10 wakike haidhuri,hujui nani atakufunika nguo hao wakiume wanaweza kua mafedhuli na huyo wakike akakujali na kukupa faraja duniani mtoto ni mtoto tuu muhimu nikuomba mungu akupe mtoto mwenye kheir na wewe
sio wakukusugua roho.
 
Jamani uzazi unafunguliwa ukiwa umefungwa...sijui hao wadoctor wa wapi unless amefanya completely hyscectomy (kutoa fuko la uzazi)
 
sina hakika na haya maelezo,kwa sababu dr inatakiwa ajue kwa nn unafunga uzaz? Kuna absolute indications na patients need.If ni ombi la mama na matokeo ya jinsia siyo uliyotegemea na una watoto wawili tu mtoto akitoka atakwambia ni wa kike na we utaamua afunge au aache kwa sababu wakati wa operation unakuwa active,hata kama umepewa ga anaweza kukuachia chance if ur wish ni mtoto wa kiume. Unless alikuwa mtoto wa tano ambapo kukuongezea chance ni kuhatarisha maisha yako.

we bado mjinga sana na madaktari wa kibongo. Hujui hapo mtu alikuwa amedili na watu wawili tofauti?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom